Bi Mkubwa anataka gari akiwa ni mstaafu je ataishi mjini au shamba? je atakuwa anasafiri nayo mbali au atapigia misele town? je baada ya kustaafu atategemea pensheni tu au atakuwa na njia zingine za kuongeza kipato? je ana familia ya ukubwa gani? lakini kwa mie vyovyote iwavyo "TOYOTA" inabaki kuwa bora number moja hasa Rav4, Noah Liteace (sio Voxy kimeo), Raum, Starlet, IST, Allex, Fielder, Runx na zinginezo zote familia ya Corolla kwani hatajutia matumizi ya mafuta, upatikanaji wa spare, Bei rahisi kwa vipuri na hata mafundi wa gari hizo ni wengi hivyo hawezi kukwama porini