Naomba ushauri, girl friend wangu amepata ujauzito miezi 3 baada ya kujifungua

Naomba ushauri, girl friend wangu amepata ujauzito miezi 3 baada ya kujifungua

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Wakuu, naombeni ushauri wa kitaalamu, mpenzi wangu alijifungua mwezi Januari mwaka huu.

Mwezi wa 4 katikati akaomba game kwani ameimisi muda mrefu(hatuishi pamoja).

Ajabu mwezi huu hajaona siku zake na ameenda kupima amekutwa na mimba tayari.

Naombeni ushauri, je hii mimba anaweza kuibeba na huku ananyonyesha na akawa salama kiafya?

Naomba kujua madhara ya hii hali.

Ahsanteni sana.
 
Ushauri no 1. Mwanamke akijifungua relax kwa miaze hata mi5 pia, kama unataka kupiga tumia mpira.

2. Huna namna lazima uutoe huo ujauzito maana afya ya mama na mtoto itakuwa mbovu mno, and most likely one of them gonna die. Kuepusha hayo madhara aitoe, japo pia ni Risk maana unacheza na Kamari ya kufa na kupona. Wanawake wametofautina wengine wakitoa mimba wanaumwa vibaya sana na wengine fresh tu.

3. Uchaguzi ni wako, usuke au unyoe.
 
Usishangae hiko kilichotangulia kikapata maradhi ya ovyo toa tu kiastaarabu
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Wakuu, naombeni ushauri wa kitaalamu, mpenzi wangu alijifungua mwezi Januari mwaka huu.

Mwezi wa 4 katikati akaomba game kwani ameimisi muda mrefu(hatuishi pamoja).

Ajabu mwezi huu hajaona siku zake na ameenda kupima amekutwa na mimba tayari.

Naombeni ushauri, je hii mimba anaweza kuibeba na huku ananyonyesha na akawa salama kiafya?

Naomba kujua madhara ya hii hali.

Ahsanteni sana.
Just Fanya Abortion Tu

Wewe hata Hauoni AIBU Kwa hiil hali
 
Jiandae gharama za maziwa ya kiwandani ya watoto vinginevyo utapoteza mtoto mmoja au wote.
Hasa huyo wa kwanza.

Pili mwanamke aanze kliniki chini ya daktari bingwa wa akina mama maana yupo hatarini sana kushika mimba muda mfupi baada ya kujifungu/kuzaa mtoto.
 
Ok, We Kidume Cha Mbegu..! Umemjaza Mimba nyingine Wakati Katoka kujifungua Karibuni.

Sikushauri uue kwa Kuitoa Mimba..Usijaribu abadan. Ila sasa take full responsibility onyesha uanamme wako Usikimbie tatizo ulilolisababisha wewe Mwenyewe.

Kama Ulikuwa hujamuoa! OA sasa weka ndani.Tafuta Wasaidizi wasaidie kulea Kichanga na Mama aendelee kulea Mimba soon Unakuwa na watoto wawili.

Hapo hata Sisi wanaume Wenzako Utakuwa hujatuangusha Kbs bali utakuwa umetujengea Heshima. Mambo ya kukimbia kimbia tuwaachie wavulana..!! Uanaume sio Kuisimamisha tu kama Marioooooooo! bali Majukumu Baba..
 
ndugu ustoe hio mimba hicho kiumbe hakina hatia nayou never know pengine akawa msaada wako badae kama uzima utakuepo

mwache alee mtot na mimba

nina ndugu yangu alijifungua kwa op mtoto wake ana miezi mitatu na hivi n mjamzito
 
Pole sana! Najua pande zote husika vichwa ni vya moto 🔥 sana toka hii hali ibainike.

Muoneni daktari mezani ili kupoza vichwa kwa uhakika
 
Sioni Shida.
Mbona ni jambo la kawaida?
Miezi 3, mimba mwezi mmoja! Ananyonyesha mpaka miezi 6! Unamwachisha anapiga misosi hapo mimba ina miezi 3.

Mbona huko mtaani watoto waliotofautiana Mwaka kuzaliwa wako kibao?
 
Wasiwasi wangu ni kama mwili wa mama utakuwa umepata nguvu ya kuhimili mikikimikiki ya ujauzito tena, ila kesi hizi zipo kwa watu ninaowafahamu na walizaa na watoto wanaishi.

Cha kufanya mtoto aanzishiwe maziwa kulingana na uwezo wenu, ya kopo (prefarably lactogen) ni mazuri zaidi maana yamewekwa vitu vingi kutokana na umri wa mtoto ili asinyonye kwa mama. Na mama mpe vyakula vingi vya kuujenga mwili.
Mtoto wangu alianza kutumia maziwa haya akiwa na miezi mitatu baada ya maziwa ya mama kukata. Ni gharama kiasi maana kila wiki alikuwa anatumia kopo 2 hadi mbili na nusu, lakini mtoto ana afya njema kabisa na haugui kila mara.

Akijifungua tena, avoid sana ku sex na mkeo miezi mitatu baada ya kujifungua, maana kipindi hicho hormones zinakuwa zimevurugika sana, na mzunguko wa hedhi unakuwa haueleweki. Kama ikibidi sana tumieni safe sex au tumieni kinga kabisa.

Binafsi sikushauri utoe hiyo mimba, mbali na imani yangu kidini, inaweza leta madhara sana kwa girlfriend wako... Anyway, mbadilishe title, kutoka girlfriend awe mke.
 
hapana asitoe mimba hii ni njia ya kupunguza matatizo kwa majibu mepesi. humu ndani wapo watu wamezaliwa hivyo na maisha yanaenda
Wengi.
Nina mshikaji wangu wa karibu First Born na Second born wanatofautiana miezi 12 tu.

Means 1st alipokuwa na miezi 3, mimba ya Second ikaingia na wanaendelea poa kabisa na afya njema kabisa.
 
Wengi.
Nina mshikaji wangu wa karibu First Born na Second born wanatofautiana miezi 12 tu.

Means 1st alipokuwa na miezi 3, mimba ya Second ikaingia na wanaendelea poa kabisa na afya njema kabisa.
🤣 🤣 🤣 🤣 sasa angeendelea angekwambia mama alikuwa anaenda shamba baada ya wiki mbili kujifungua akirudi na mzigo wa kuni juu
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] sasa angeendelea angekwambia mama alikuwa anaenda shamba baada ya wiki mbili kujifungua akirudi na mzigo wa kuni juu
Very normal hiyo ipo mpaka sasa hivi.
Nenda huko Mwamashele uone.
Kujifungua! Kidonda kikipona ni nje, only 40 days zinatosha kabisa
 
Very normal hiyo ipo mpaka sasa hivi.
Nenda huko Mwamashele uone.
Kujifungua! Kidonda kikipona ni nje, only 40 days zinatosha kabisa
sasa ukutane na hawa wanawake tuliokutana nao kwenye chips lazima unyooke!
 
Back
Top Bottom