Ushauri:
1. Mchukue huyo Girlfriend wako na Kachanga muende Hospitalini tena kwa wataalamu haswa (Jiandae Kisaikolojia kupokea Matusi, Aibu, Lawana na mengine yote).
Serikalini: Muhimbili National Hospital, Hospitali ya Mkoa au Wilaya.
Binafsi: Regency Hospital, Aga Khan & Kairuki na nyingine zenye Majina Makubwa.
2. Hakikisha Familia yako wote watatu mna Bima ya Afya. Hata kama ni Bima ya Kazini lakini Mama na Mtoto wakatie NHIF. (This is no. 1 priority and it's must)
3. Hakikisha hatoi Mimba na uwe nae karibu mara nyingi kwa kumtia Moyo na kum support; USIMLAUMU!
4. Tenga Fedha za kutosha kwa ajili yao kama unazo. Kama huna ANZA KUZIKUSANYA KWA BIDII maana wakati unakuja zitatumika na hazitatosha.
5. Zingatia kwa ukaribu Afya ya Kiakili ya Mama na Msosi mzuri (Balanced Diet) kwao wote.
"Ukichelea kulia mwana, utalia wewe."