Wasiwasi wangu ni kama mwili wa mama utakuwa umepata nguvu ya kuhimili mikikimikiki ya ujauzito tena, ila kesi hizi zipo kwa watu ninaowafahamu na walizaa na watoto wanaishi.
Cha kufanya mtoto aanzishiwe maziwa kulingana na uwezo wenu, ya kopo (prefarably lactogen) ni mazuri zaidi maana yamewekwa vitu vingi kutokana na umri wa mtoto ili asinyonye kwa mama. Na mama mpe vyakula vingi vya kuujenga mwili.
Mtoto wangu alianza kutumia maziwa haya akiwa na miezi mitatu baada ya maziwa ya mama kukata. Ni gharama kiasi maana kila wiki alikuwa anatumia kopo 2 hadi mbili na nusu, lakini mtoto ana afya njema kabisa na haugui kila mara.
Akijifungua tena, avoid sana ku sex na mkeo miezi mitatu baada ya kujifungua, maana kipindi hicho hormones zinakuwa zimevurugika sana, na mzunguko wa hedhi unakuwa haueleweki. Kama ikibidi sana tumieni safe sex au tumieni kinga kabisa.
Binafsi sikushauri utoe hiyo mimba, mbali na imani yangu kidini, inaweza leta madhara sana kwa girlfriend wako... Anyway, mbadilishe title, kutoka girlfriend awe mke.