Ukipata mbao ambazo zimezoeleka kwa jina la mlingoti utakuwa umefanya jambo la maana mno. Zenyewe haziwekwi dawa. Upate zilizokomaa na utazifuta kwa rangi yake kuwa nyekunyekundu hivi.
Hapo hautawahi kulia juu ya wadudu. Bati zitaisha, utaezeka tena bati huku mbao zako zikiwa vilevile. Mafundi wengi hawawezi kukuombea juu ya hilo ingawa wanazijua ubora wake kwani wanataka mbao laini.