Naomba ushauri juu ya biashara ya Uber, Bolt

Kwan huna muda wa service mara kwa mara?
Mimi kwa upande wangu niliwahi kuendesha Uber kwa miezi 6 kila ikifika 3,000kms naenda service baada ya miezi 6 nikaenda service, spare na kila kitu nikaletewa invoice 1.2m Hapo ndo niliaga mashindano maana faida yote ililipa gharama za kutengeneza gari

Rating za abiria wa Uber nao pasua kichwa.
 

Inaonekana ana matatizo na graduates, sijui walimfanyeje. Pengine mimi ni Form Four Leaver tu.
 
Shukrani sana Mkuu. Hakika nitayafanyia kazi uliyoyaelezea hapa. [emoji120]
 
Pumba ya mwaka. Vijana mmekuaje siku hz hiv kwa nn usijiongeze ukajaribu mwenyewe mpaka uombe ushauri?

Siwezi kufanya biashara yoyote kichwa kichwa ndugu yangu kwasababu kuna watu wanaifanya, kufanya hivyo ni km kutest kina cha maji na miguu yote miwili utazama au kuvuka main road huku umefunga macho utagongwa tu
 
Shukrani kwa mchango mkuu, nitayafanyia kazi uliyoyaelezea hapa.
 
Thank you for the insight bro, I appreciate [emoji120]
 
Utakuta na wewe unajiita Graduate kumbe kichwani empty set. Endelea kula kwa Shem

Acha uoga Bwege wew [emoji1787][emoji1787][emoji12][emoji12]

#Yaaani kwakua Jamaa kapangilia uzii wake vizuri nakuuliza vitu anavyoataka kujua kwa Ustadi na utashi basiii Umekimbilia Kumuona nia #Graduate /

Kwani @Joshua_ok:Xhida nini mpaka Umejamba bila Kutarajiaa[emoji23][emoji23][emoji23]Ona xaxa aibu yakooo hii

Au hutaki muwe wengi kwenye Hzoo Uber & Na Bolt
 
Hizi wenzetu mbele wanaaziita side hustle.

Hata mimi natamani siku 1 nifanye hii kazi kuongeza kipato, ili hata ukiwa na gari lisiwe tu liability, liingize pesa
 
Mkuu ilkuwa unaendesha gari aina gani, je lilikuwa la kutoka showroom/japan au kununua kwa mtu ?
 
Mkuu ilkuwa unaendesha gari aina gani, je lilikuwa la kutoka showroom/japan au kununua kwa mtu ?
Gari (IST) Ni yangu private. Ilikua na miezi 3 toka iingie from Japan. Uber/Bolt kwa Dar italipa ukiwa selective kama huendi Mabondeni na unaepuka foleni. Zaidi, Jitahidi kuwahudumia wateja Kama watoto wachanga kwa vijizawadi eg. Pipi, bubble gums wakupe rating nzuri.
NB: Bundle Bei juu jiandae kwa hilo
 
Mkuu ukiondoa gharama za uendeshaji... faida kwa siku ni kama kiasi gani?

Mtaji uwekezaji utachukua muda gani kurudi
 
Mkuu ukiondoa gharama za uendeshaji... faida kwa siku ni kama kiasi gani?

Mtaji uwekezaji utachukua muda gani kurudi

Faida inategemea na jinsi siku ilivyo changamka, na sehemu unazopita. Kuna siku unaweza ukapata ela nyingi mpaka raha na kuna siku unaweza ukapata pesa kidogo tu. Lakini ni biashara ambayo ukiwa na nidhamu unaweza kuingiza faida nzuri. 50, 60,70 wakati mwingine mpaka laki hukosi kwa siku.

Nna uzoefu na biashara hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…