Naomba ushauri juu ya biashara ya Uber, Bolt

Naomba ushauri juu ya biashara ya Uber, Bolt

Kwan huna muda wa service mara kwa mara?
Mimi kwa upande wangu niliwahi kuendesha Uber kwa miezi 6 kila ikifika 3,000kms naenda service baada ya miezi 6 nikaenda service, spare na kila kitu nikaletewa invoice 1.2m Hapo ndo niliaga mashindano maana faida yote ililipa gharama za kutengeneza gari

Rating za abiria wa Uber nao pasua kichwa.
 
Kuwa Graduate haimaanishi umegraduate katika maisha.

Baba Richard anahitaji kujua experience kwa waliowahi kufanya hii biashara. Kwenda ofisini kwao haiwezi kumsaidia kupata anachokitaka .

Hebu jaribu kwenda ofisi za Forever Living uone watakavyokupamba, halafu njoo huku mtaani na hiyo biashara uone utakavyosaga soli.

Inaonekana ana matatizo na graduates, sijui walimfanyeje. Pengine mimi ni Form Four Leaver tu.
 
Mm nimewah tumia bolt kama abiria, ni cheap sana baada ya kumaliza safar zangu nikapata kumuhoji dereva wa bolt, ilikuwa ni boda kuwa unapata faida? Alichonijibu ni kuwa hii kazi bro ni nzur kwa sababu si sawa na kukaa kijiweni na kusubir mteja, mfano mm nimekuleta hapa mbagala ww, hapa mm sirud mtupu, program inanitafutia abiria ambae anatoka mbgla hapa kwenda sehemu nyengine, kwa hyo kutwa nzima kazi ipo hvyo hadi inafikia hatua una log off ww mwenyewe, kwa sababu usipokuwa makini utakesha !! Kutwa nzima , nikamuuliza kuhusu malipo akasema mfano kwenye hii 18000 yao jamaa ni kama 1000 au 1500 , so nilichojifunza kutoka kwa yule dereva kutokana na maoni yake ni profitable business kwa upande wake!! Ndio hvy ndg
Shukrani sana Mkuu. Hakika nitayafanyia kazi uliyoyaelezea hapa. [emoji120]
 
Pumba ya mwaka. Vijana mmekuaje siku hz hiv kwa nn usijiongeze ukajaribu mwenyewe mpaka uombe ushauri?

Siwezi kufanya biashara yoyote kichwa kichwa ndugu yangu kwasababu kuna watu wanaifanya, kufanya hivyo ni km kutest kina cha maji na miguu yote miwili utazama au kuvuka main road huku umefunga macho utagongwa tu
 
Bolt ndio iko cheap zaidi na ina ofa sana kwa wateja na wengi wanatumia hiyo kuliko Uber, madereva wanazo hizi apps zote. Madereva wa Bolt wanaingiza hela nyingi kuliko wale wa vijiweni. Yani hujutii kuilipia, uzuri wake kuna siku unapiga kazi mpaka unaamua kupumzika.

Wapo watu anafanya kazi mchana, jioni anapiga Bolt mpaka saa tano usiku anarudisha kagari kake kazuri nyumbani anapumzika. Mmoja alinambia hela ya kula na bills zote nyumbani anaipata kwenye Bolt, mshahara wake haulishi familia hata siku moja.
Shukrani kwa mchango mkuu, nitayafanyia kazi uliyoyaelezea hapa.
 
Mimi kwa upande wangu niliwahi kuendesha Uber kwa miezi 6 kila ikifika 3,000kms naenda service baada ya miezi 6 nikaenda service, spare na kila kitu nikaletewa invoice 1.2m Hapo ndo niliaga mashindano maana faida yote ililipa gharama za kutengeneza gari
**Rating za abiria wa Uber nao pasua kichwa.
Thank you for the insight bro, I appreciate [emoji120]
 
Utakuta na wewe unajiita Graduate kumbe kichwani empty set. Endelea kula kwa Shem

Acha uoga Bwege wew [emoji1787][emoji1787][emoji12][emoji12]

#Yaaani kwakua Jamaa kapangilia uzii wake vizuri nakuuliza vitu anavyoataka kujua kwa Ustadi na utashi basiii Umekimbilia Kumuona nia #Graduate /

Kwani @Joshua_ok:Xhida nini mpaka Umejamba bila Kutarajiaa[emoji23][emoji23][emoji23]Ona xaxa aibu yakooo hii

Au hutaki muwe wengi kwenye Hzoo Uber & Na Bolt
 
Bolt ndio iko cheap zaidi na ina ofa sana kwa wateja na wengi wanatumia hiyo kuliko Uber, madereva wanazo hizi apps zote. Madereva wa Bolt wanaingiza hela nyingi kuliko wale wa vijiweni. Yani hujutii kuilipia, uzuri wake kuna siku unapiga kazi mpaka unaamua kupumzika.

Wapo watu anafanya kazi mchana, jioni anapiga Bolt mpaka saa tano usiku anarudisha kagari kake kazuri nyumbani anapumzika. Mmoja alinambia hela ya kula na bills zote nyumbani anaipata kwenye Bolt, mshahara wake haulishi familia hata siku moja.
Hizi wenzetu mbele wanaaziita side hustle.

Hata mimi natamani siku 1 nifanye hii kazi kuongeza kipato, ili hata ukiwa na gari lisiwe tu liability, liingize pesa
 
Mimi kwa upande wangu niliwahi kuendesha Uber kwa miezi 6 kila ikifika 3,000kms naenda service baada ya miezi 6 nikaenda service, spare na kila kitu nikaletewa invoice 1.2m Hapo ndo niliaga mashindano maana faida yote ililipa gharama za kutengeneza gari
**Rating za abiria wa Uber nao pasua kichwa.
Mkuu ilkuwa unaendesha gari aina gani, je lilikuwa la kutoka showroom/japan au kununua kwa mtu ?
 
Mkuu ilkuwa unaendesha gari aina gani, je lilikuwa la kutoka showroom/japan au kununua kwa mtu ?
Gari (IST) Ni yangu private. Ilikua na miezi 3 toka iingie from Japan. Uber/Bolt kwa Dar italipa ukiwa selective kama huendi Mabondeni na unaepuka foleni. Zaidi, Jitahidi kuwahudumia wateja Kama watoto wachanga kwa vijizawadi eg. Pipi, bubble gums wakupe rating nzuri.
NB: Bundle Bei juu jiandae kwa hilo
 
Mkuu ukiondoa gharama za uendeshaji... faida kwa siku ni kama kiasi gani?

Mtaji uwekezaji utachukua muda gani kurudi
 
Mkuu ukiondoa gharama za uendeshaji... faida kwa siku ni kama kiasi gani?

Mtaji uwekezaji utachukua muda gani kurudi

Faida inategemea na jinsi siku ilivyo changamka, na sehemu unazopita. Kuna siku unaweza ukapata ela nyingi mpaka raha na kuna siku unaweza ukapata pesa kidogo tu. Lakini ni biashara ambayo ukiwa na nidhamu unaweza kuingiza faida nzuri. 50, 60,70 wakati mwingine mpaka laki hukosi kwa siku.

Nna uzoefu na biashara hiyo
 
Back
Top Bottom