Naomba ushauri kama kuna tiba ya kunusuru mimba kuharibika

fettydia

Senior Member
Joined
Aug 31, 2016
Posts
116
Reaction score
81
Habari wana bodi nina ujauzito wa wiki 18 ila kwa bahati mbaya ijumaa nikaona maji yananitoka ukeni, ambapo clinic niliambiwa na kiashiria kibaya nikaletwa hospitali nimelazwa tangu siku hiyo.

Baada ya vipimo imeonekana maji yamepungua kwa mtoto ila yupo salama na mbaya zaidi sahivi nikienda haja ndogo inatoka na vidamu vyepesi au nikiwa nimelala naona kama bado yanatoka nifanye nini ili niweze kumnusuru mwanangu?
 
Dah pole sana epuka kazi yoyote kwa sasa hivi yani hata sex stop kabisa "bed rest" yani wewe ulale ukiamka ni kula na kwenda haja tu usipande boda boda wala kufanya mazoezi yoyote yale Mungu akuvushe salama staki kukumbuka yalonisibu
 
Dah pole sna epuka kazi yoyote kwa sasa hiv yan hata sex stop kabisa "bed rest" .....yan ww ulale ukiamka n kula na kwenda haja tu ,,usipande boda boda wala kufanya mazoez yoyote yale Mungu akuvushe salama staki kukumbuka yalonisibu
Asante mpenzi mwenyezi Mungu anivushe salama maana nabakia kulia tu, bora haya maji yakate kabisa sitamani kupoteza hichi kiumbe na hii hali inaniumiza mno sahivi nipo bed rest pia
 
Epuka tunda la nanasi lione kama sumu kipindi hiki
 
Asante mpenzi mwenyezi Mungu anivushe salama maana nabakia kulia tu, bora haya maji yakate kabisa sitaman kupoteza hichi kiumbe na hii hali inaniumiza mno...sahv nipo bed rest pia

Pole mpenzi Mungu akutie nguvu katika shida hii punguza mawazo/ stress, jaribu kuwa bize na kusomasoma vitu kaa vitabu au hata story mitandaoni, mana najua hufanyi kazi so muda mwingi unakua umekaa or kulala hii itakusaidia kutowaza sana hii ni hatari pia kwa mtoto
 
Wa kwanza mpendwa
Sawa, kuna baadhi ya maswali inatakiwa uyajibu ili kujiridhisha kuwa ni kweli mfuko mtoto umetoboka( preterm premture rupture of membrane or PPROM) na kusababisha hali hiyo, hii itaendana sambamba na uchunguzi kwa Speculum. Katika wiki ya 18 bado ni mapema sana, inawezekana kufika mwisho japo kuna risks nyingi.

find me Pm
 
Umewahi kuzichoropoa kabla hujapanga kuzaa kama jibu ni YES katubu kwanza. Kwasababu tumbo lako linajua hutaki mimba
 
Asante my nitajitaidi
 
Umewahi kuzichoropoa kabla hujapanga kuzaa ? Kama jibu ni YES Zkatubu kwanza. Kwasababu tumbo lako linajua hutaki mimba
Sikuwahi hata kushika ujauzito huko nyuma mpaka nikawa nahc sina uwezo coz nilikua nasumbuliwa na tumbo sana
 
Asante mpenzi mwenyezi Mungu anivushe salama maana nabakia kulia tu, bora haya maji yakate kabisa sitaman kupoteza hichi kiumbe na hii hali inaniumiza mno...sahv nipo bed rest pia
Mawazo ,stress n mbaya mno + lishe mbovu +maradhi mfano UTI n.k hakikisha unakunywa maji ya kutosha na chakula kwa mpangilio
 
fettydia,
Nakushauri kamuone Dr kapona katika clinic yake chanika buyuni naamini kwa uwezo wa mungu atakusaidia sababu alimsaidia mtu mwenye tatizo kama hilo na akajifungua salama tu
 
Hapo mimba inatishia kutoka Kuna dawa nimeisahau jina ingekusaidia kidonge kimoja kinauzwa alfu 15 na unatakiwa ununue doz nzima but nahic umechelewa kama Damu zmeanza kutoka !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…