Naomba ushauri kama kuna tiba ya kunusuru mimba kuharibika

Naomba ushauri kama kuna tiba ya kunusuru mimba kuharibika

Hapo mimba inatishia kutoka Kuna dawa nimeisahau jina ingekusaidia kidonge kimoja kinauzwa alfu 15 na unatakiwa ununue doz nzima but nahic umechelewa kama Damu zmeanza kutoka !
Duphaston 10mg but asitumie bila ushauri wa daktari
 
Pole sana mamy Mungu akuponye na kukuvusha salama kwenye kipindi ulichonacho
 
Pole fettydia kwa hofu na wasiwasi ulionao juu ya dalili hatarishi kwa maendeleo ya mtoto aliye tumboni. Fuatilia maoni na ushauri murua wa wana JF na hapana shaka Mungu atakusaidia na hali itakuwa shwari.

Japo upo kwenye wasiwasi na hofu, naomba nami unifahamishe ni dawa gani ulitumia kukuponya maumivu ya tumbo na hatimaye kushika ujauzito? Umesema hapo kabla umesumbuliwa sana na maumivu ya tumbo mpaka ukahisi huna uwezo wa kushika ujauzito.

Mke wangu ana shida kama uliyokuwanayo wewe ya maumivu makali zaidi kuliko kawaida na suala la kushika ujauzito kwake limekuwa gumu licha kufanya vipimo na wote kuonekana hatuna tatizo.

Ahsante.
 
Dulphaston kidonge hakiuzw kimoja elfu 10. Na hiv mama k unameza folic acid lakin??
sipo hapa kubishana bei ya vidonge nilichojaribu ni kumtajia vidonge vinavyoweza kusave hio situation ambayo ndio highyl recommended kwa watu wenye tatizo kama lake
 
Habari wana bodi nina ujauzito wa wiki 18 ila kwa bahati mbaya ijumaa nikaona maji yananitoka ukeni, ambapo clinic niliambiwa na kiashiria kibaya nikaletwa hospital nimelazwa tangu siku hiyo.

Baada ya vipimo imeonekana maji yamepungua kwa mtoto ila yupo salama na mbaya zaidi sahivi nikienda haja ndogo inatoka na vidamu vyepesi au nikiwa nimelala naona kama bado yanatoka nifanye nn ili niweze kumnusuru mwanangu?
Sijakuelewa naomba weka sawa hili, umeambiwa mtoto tumboni hana maji au nyumba inayomuhifadhi MTOTO majina yamepungua!
 
sipo hapa kubishana bei ya vidonge nilichojaribu ni kumtajia vidonge vinavyoweza kusave hio situation ambayo ndio highyl recommended kwa watu wenye tatizo kama lake
Aiseee sijabishana na ww kuhus bei ila nimetahadharisha ulivyojibu post ya mtu alosema kuna dawa ila haikumbuk jin inauzwa elfu 10 so kuclear nikasema hii ulosema haiuzwi kidonge elfu 10 so usipende kujump sana
 
Aiseee sijabishana na ww kuhus bei ila nimetahadharisha ulivyojibu post ya mtu alosema kuna dawa ila haikumbuk jin inauzwa elfu 10 ,,,so kuclear nikasema hii ulosema haiuzwi kidonge elfu 10 ...so usipende kujump sana
Inategemea utainunua wapi mi nimeshuhudia hiyo dawa inauzwa 12000 kwa kidonge na kwenda kwingine ni 3500 tu na wengine hawaijui kabisaaa!! kwa hiyo experience yako sio final tembea ujionee!! ndio maana nikatahadharisha sipo hapa kubishana bei be wise madam!
 
Habari wana bodi nina ujauzito wa wiki 18 ila kwa bahati mbaya ijumaa nikaona maji yananitoka ukeni, ambapo clinic niliambiwa na kiashiria kibaya nikaletwa hospital nimelazwa tangu siku hiyo.

Baada ya vipimo imeonekana maji yamepungua kwa mtoto ila yupo salama na mbaya zaidi sahivi nikienda haja ndogo inatoka na vidamu vyepesi au nikiwa nimelala naona kama bado yanatoka nifanye nn ili niweze kumnusuru mwanangu?
Pale ulipo hospitalini wanamajibu ya matatizo yako yote,kama huna imani na hospitali ya hapo hamia kwingine penye huduma bora. Humu jamii forum utapotea bure kwa sababu unaweza hata ukaambiwa kunywa mkojo wa ngiri.
 
Nyumba inayo muhifadhi mtoto mkuu ndio haina maji
Kama ni hivyo sababu huwa ziko nyingi cha msingi hapo nenda hospital ukafanyiwe uchunguzi wa vipimo ambavyo vitachunguza damu yako kujua kama kunatatizo la maambukizi ya bacteria hapo tutajua chakufanya kwa maalezo yako inaonekana baada ya wewe kwenda hospitali ulipotoa maalezo Daktari aliokupokea hapo alizingatia saana maelezotu na ndio maana uchunguzi alioufanya ulikua ni wa kumchunguza MTOTO mwenyewe humo tumboni na uchunguzi huo ulikia ni wa kumsaidia yeye Daktari wako baada ya hapo angekupima vipimo vya Damu kutafuta sababu ya kwanini maji katika pango la MTOTO yapungue, Vipimo vya damu vingebainisha ni wavamizi gani wamepelekea kuvuruga uiano sahihi wa maji kwani ikumbukwe kukauka au kupungua maji mwilini au sehemu yoyote ya mwili Sio ugonjwa Bali ni tishio la hatari hivyo inapotokea hali hiyo Daktari anatakiwa aichukulie kua ni hali ya dharula ya hatari hivyo achukue hatua haraka ya kujua chanzo ili aweze kuitokomeza haraka hivyo Pima vipimo vyote vya awali na pia vipimo vinavyoendelea kucheki full blood
 
Maji yalipungua sababu chupa ilipasuka na mpaka muda huu nipo hospital cjaruhusiwa bado nimewekwa bed rest pia wananipa dawa ya kuondoa infection ila mtoto akipimwa yupo active na anacheza vzr tu sasa shida ni hayo maji na nimeambiwa mtoto anajitengenezea maji mwenyewe
 
Pia nilipima vipimo krb vyote hata hvyo vya damu
 
Back
Top Bottom