Naomba ushauri: Kati ya Kluger V na Harrier ni gari ipi ni nzuri zaidi?

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477

Kluger V

Harrier

Wakuu, nimejipanga kwa muda wa kutosha na sasa naona naweza kujipatia usafiri wangu wa kueleweka. Kuna gari hizi mbili zote nazipenda sana. Naomba kushauriwa na wenye uzoefu na uelewa mkubwa wa hizi gari mbili ni ipi wanaona ni nzuri zaidi? Suala la mafuta sio tatizo, lakini uimara wa gari na hadhi ya gari na gharama ya gari. Nimetenga bajeti ya milioni ishirini na tano mpaka thelathini kwa mchakato wote.

Karibuni tushauriane.


MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU:
---
Harrier (Lexus)


Kluger V


Volvo xc90


Kazi kwako. Pia zingatia na umri wako. Ila kama umri umesogea kaa humu Toyota Fortuner
---
---


MREJESHO WA MDAU BAADA YA KUSOMA MAONI YA WANA JF
 

Kluger nadhani huwa zina gia 4, so expect fuel consumption to be high. For me harrier ndio mpango mzima hasa zile zenye engine ya vvti
 
sina gari sijawai kumilika hata baiskeli ina hamuwezi kuamini ni magari machache sana sijawai kupanda.yaani machache . hizi lift hizi saa zingine ukute kuna watu wanaiba nyota yangu ya kumiliki gari wakinipa lift. kwanini nipande magari makali makali ya wenzangu na kuishia kupiga honi tu na kupungia watu? why?
 
Kluger nadhani huwa zina gia 4, so expect fuel consumption to be high. For me harrier ndio mpango mzima hasa zile zenye engine ya vvti
Kuhusu mafuta sio tatizo. Suala ni je hiyo bajeti niliyotenga itaniwezesha kulinunua?
 
Usisahau kuweka taarifa zako za kifedha karibu, TRA watazihitaji
 
Kluger itakufaa zaidi na hiyo bajeti inakutosha kabisa
 

Brother, I have been into both mess.
Kluger nyepesi, na haina matoleo tofauti tofauti kama Harrier. Kwa issue ya status hakuna wa kukuona outdated.

Fuel consumption zote zinaendana 6-8Km/lt.
Engine zote VVTI.

Harrier nzito na ipo comfortable kiasi chake kuzidi kidogo Kluger..

Generally both are good cars.
Cha msingi tafuta gari iliyotembea km chache na iliyo kwenye condition nzuri.
Make a budget of not more than 28M for Harrier and 24M for Kluger.
All the best.
 
Nina harrier, yangu naonaga ipo tofauti kidogo na harrier nyingine. Ya kwangu iko na automatic na manual gear anafanya kucontrol unachotaka. Kama mwezi hivi umepita nilitoka Dar saa 11 kwenda Kahama nilifika saa 10:30 kila mtu niliomwambia alikataa Harrier (Lexus) zinatembea sana kwa mpenda safari. Kluger kidogo ni zito. Sema consumption kidogo ni kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…