Naomba ushauri: Kati ya Kluger V na Harrier ni gari ipi ni nzuri zaidi?

Naomba ushauri: Kati ya Kluger V na Harrier ni gari ipi ni nzuri zaidi?

Mkuu nunua Harrier, vvTi 4cylinder ni nzuri kuliko Kluger. Pia inastahimili safari ya mbali.
 
Hiyo pesa unaweza kupata Volvo XC90 ya mwaka 2007 au 2008 kabisa! Hapo unakuwa umeweka mkataba. Achana na mazoea ya gari za Kijapani.
Nimeicheki ni gari nzuri sana, vipi kuhusu spear Mkuu.
 
Kuhusu mafuta sio tatizo. Suala ni je hiyo bajeti niliyotenga itaniwezesha kulinunua?
Kulinunua inategemea na unataka la namba gani ila kama bei yapo mpaka ya M16. Ila kama ni new model andaa kuanzia 35 na kuendelea mkuu.
 
Wakuu, nimejipanga kwa muda wa kutosha na sasa naona naweza kujipatia usafiri wangu wa kueleweka. Kuna gari hizi mbili zote nazipenda sana. Naomba kushauriwa na wenye uzoefu na uelewa mkubwa wa hizi gari mbili ni ipi wanaona ni nzuri zaidi? Suala la mafuta sio tatizo, lakini uimara wa gari na hadhi ya gari na gharama ya gari. Nimetenga bajeti ya milioni ishirini na tano mpaka thelathini kwa mchakato wote.

Karibuni tushauriane.

Harrier ni nzuri na imara na hadhi kuliko Kluger
 
Mbona bei imesimama hivyo mkuu while za zamani sana?

Mkuu hivyo vyuma ni mkataba isitoshe vipo kikazi zaidi. By the way hadi 16.5M unaweza pata za 97. Tafuta dealer mzuri tu.
 
Harrier (Lexus)
6c9e834b9c486246b0a32976c016ef81.jpg


Kluger V
f0c638ecda4daa9a678197f3f35335a4.jpg


Volvo xc90
50bb30c9b4d1dca9f53a951eaab9f3c9.jpg


Kazi kwako. Pia zingatia na umri wako. Ila kama umri umesogea kaa humu Toyota Fortuner
9e66bcfc126d59ba3860e0ef9e103e1d.jpg
 
Wabongo bwana, unataka kuongeza uniform mjini? Yaani kila
sehemu Harrier au IST. Be different chukuaCommodore V6
Sasa hiyo Commodore haifahamiki hata mafundi hawaifahamu labda jaribu kuielezea zaidi.
 
Back
Top Bottom