Wakuu, nimejipanga kwa muda wa kutosha na sasa naona naweza kujipatia usafiri wangu wa kueleweka. Kuna gari hizi mbili zote nazipenda sana. Naomba kushauriwa na wenye uzoefu na uelewa mkubwa wa hizi gari mbili ni ipi wanaona ni nzuri zaidi? Suala la mafuta sio tatizo, lakini uimara wa gari na hadhi ya gari na gharama ya gari. Nimetenga bajeti ya milioni ishirini na tano mpaka thelathini kwa mchakato wote.
Karibuni tushauriane.
Hongera kwa hatua uliyoifikia ya kununua gari. To clarify; binafsi sijawahi kumiliki haya magari, usiscroll down kwanza! Nisikilize, but nina experience na Kluger na nitakupa mtazamo wangu wa Toyota Harrier.
My cousin anatumia Toyota Kluger V, nilishaiendesha mara kibao tu, since yeye hata hawezi kuendesha ana dereva wake, so most of the time unalikuta home tu. And this is my review:
Toyota Kluger ni gari zuri, heshima mjini. Ndani lina nafasi kubwa, ukipata yenye sunroof utaenjoy maana zinakuwaga na bonge la sunroof. Speakers are loud enough, seats are high enough kukupa high visibility ya barabara. Though sidhani kama interior italingana na Harrier.
Mafuta linakula vizuri, 1l/10km, ila naona umesema mafuta sio issue. Acceleration is fine for a huge vehicle, mimi sio mtu wa speed so siwezi zungumzia kuhusu hilo. But lina hundle vizuri barabara zetu za Boko. Though at some point nahisi lipo chini sana, maybe its just me.
Nina doubt sana 4WD yake though kwa hapa Dar haitakuzingua unless wewe ni engineer wa REA. So expect it to take you anywhere. Barabarani linatulia mpaka raha. Vidimbwi havisikiki, wewe ni kunesanesa tu. At night, taa zake nazipa salute, stock lights. Overall handling yake imetrump Rav4 na Suzuki Escudo. Its an SUV that handles like a Sedan.
Conclusion:
Like I said Harrier sijawahi kuliendesha wala kulipanda. Zaidi nalionaga kwa majirani na barabarani, but I can tell you, kama wewe ni bishoo chukua tu Harrier, lile gari lina turn heads. Kwa looks Kluger haliiwezi Harrier. Kluger lina sura ngumu kama limao, Harrier limekaa kama Qatar Airways. Also, Harrier linaonekana liko juu in terms of ground clearance, so I think lita handle vizuri zaidi Barabara za vumbi.
Just to remind you unacompare Harrier latest kidogo na Kluger la zamani, so obviously Harrier litali trumplify Kluger. Mtazamo wangu kama hela sio ya mawazo chukua Harrier uongeze Instagram likes, ila kama unataka hizo extra 2-4m uweke heshima bar chukua Kluger.
Hope I answered your question. Enjoy your new car.
-callmeGhost