Naomba ushauri: Kati ya Kluger V na Harrier ni gari ipi ni nzuri zaidi?

Kwa nijuavyo Harrier na Kluger:

Ni kitu kimoja, ukiwa na Kluger, jua kwamba ni sawa na una Harrier tu maana ni gari ile ile tu, ila wameitofautisha kwenye muundo wa nje tu pamoja na majina basi!

Lakini kila kitu ni kile kile yaani. Kuanzia engine capacity & machenically etc

So, ni wewe tu uchague ni aina ya muundo unaouopenda. (I mean, muundo wa Harrier au Kluger)

By the way, okoa fedha nyingi kwa kununua gari yoyote unayohitaji kupitia ecarstanzania
Sisi ni waingizaji wa magari bora na kwa gharama nafuu kabisa.

Tupo Kinondoni, Ada Estate.

Email : ecarstanzania@gmail.com

Karibu
 
Mkuu, siku hizi kuna Subaru Forester SUV, engine 2.0L iko juu kama Kluger.
Tatizo lingine la Subaru ni kuwa se-sale value yake iko chini. Kwa hiyo siku ukitaka kubadilisha gari, litanunuliwa kwa bei ya chini.
 
Nimewahi panda Kluger, Harrier sijawahi. Ila kwa muonekano zile Harrier new model zinaita sana
Hivi hizi new model zinaanzia mwaka gani? Je bajeti yangu ya 30M itaweza kunipa hiyo new model lakini kilometa zake zisizidi 100,000?
 
MAGARI7, Hapo umetupa kitu tofauti ambacho sikuwa nakifahamu kabisa! Ina maana tofauti ya Harrier na Kluger ni body tu? Zina injini sawa, gear box sawa, nk? Hebu fafanua kidogo. Ina maana kwa kiasi kikubwa hata spea zake zinaingiliana?
 
Hapo umetupa kitu tofauti ambacho sikuwa nakifahamu kabisa! Ina maana tofauti ya Harrier na Kluger ni body tu? Zina injini sawa, gear box sawa, nk? Hebu fafanua kidogo. Ina maana kwa kiasi kikubwa hata spea zake zinaingiliana?
Trust me, hizi Harrier na Kluger, kila kitu ni kile kile, kuanzia engine na kila kitu. Wametofautisha majina na muundo tu basi.
 
Kluger nadhani huwa zina gia 4, so expect fuel consumption to be high. For me Harrier ndio mpango mzima haza zile zenye engine ya vvti
Kluger 4 ni very economical kwenye mafuta, ina piston nne! Sawa na Carina
 
Kwa sababu unawakimbia
 
Kluger 4 ni very economical kwenye mafuta, ina piston nne! Sawa na Carina
Ila mimi sipeni tu body yake. Harrier ipo vizuri ila issue ni kwenye fuel consumption, ila kwa kuwa mwenyewe kasema fuel sio tatizo, achukue tu.
 
Kasimame pale Tazara au Magomeni au Salender Bridge. Angalia gari ipi kati ya hizo zipo nyingi barabarani, Nunua hiyo. Harrier wamemuacha mbali sana Kluger. Kluger haina mvuto, bodi yake ni kama gari ndogo tu (saloon).
 
Mrejesho: Baada ya kupitia post nyingi humu na kwa kuzingatia ushauri wa family members tayari nimeshanunua Kluger V nyeusi: Cylinder 6, CC 3,000. Nimeshaitumia kwa zaidi ya miezi 5.

Kwenye highway haitumii sana mafuta, japo huwezi kuilinganisha na utumiaji mafuta wa gari ndogo. Kwenye mizunguko ya mitaani na mjini hapo ulaji wake wa mafuta uko juu kidogo. Ila nimeipenda sana na sijajuta.

Nashukuru sana kwa michango yenu.
 
Kila gari ina matatizo kwa muda wake ukitaka kununua gari amua mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…