Naomba ushauri katika hili

Naomba ushauri katika hili

Zeroiez

Senior Member
Joined
May 2, 2013
Posts
181
Reaction score
201
Nimegundua vinywaji nilivyonunua jana kutoka dukani kuwa vimekwisha matumizi yake (expired).

Je, naweza kufungua kesi au wapi mahala husika pa kupeleka malalamiko yangu?

expire.jpg


IMG_9586.JPG
 
Mrudishie aliyekuuzia akupe hela yako, lakini pia jenga tabia ya kusoma kifungashio kabla haujatoka kwa muuzaji
 
Anaweza kukana hajakuuzia huo mzigo,cha kufanya mrudishie na umpige mkwara angalau akulipe na fidia pia
 
Nenda Kanunue tena vinywaji uthibitishe vimeexpire umbananishe hapo hapo. Uwe Na shahidi lakini
 
SI busara kila kitu kufungua mashitaka mrudishie akupe fedha yako akigoma labda
 
Kufungua kesi utahitaji kudhibitisha mambo yafuatayo:-
* Kwamba aliyekuuzia ni mtengenezaji au wakala wake.
* Kwamba bidhaa uliyonunua hungeweza na mtu yoyote kama wewe hangeweza kugundua hitilaft hiyo ila mtengenezaji au wakala TU.
* Kwamba kutokana na kutumia bidhaa hiyo umepata madhara yanayoonekana na kupimika
* kwamba Madhara hayo yanatafakarika kwa uelewa wa mtengenezaji.
 
Back
Top Bottom