Naomba Ushauri katika ufugaji wa nguruwe

Naomba Ushauri katika ufugaji wa nguruwe

Mimi ni mfugaji ila nimepitia changamoto ya magonjwa mwaka 2022 na mwaka huu nilipoanza upya ufugaji nimepata hasara ya magonjwa, sasa nahitaji kujua njia sahihi ya kuepuka haya magonjwa cos baada ya mwaka 2022 kupitia changamoto hiyo nilistisha hadi mwaka huu ndio nilianza kufuga na nimekutana na changamoto hile hile, ni jinsi gani ninaweza kusafisha banda ili nianze upya kwa muda huu, kuna dawa za kupulizaia na je ni mambo gani niepuke ili kuepuka changamoto ya magonjwa kwa wanyama hawa?
Pole sana ndugu je ulijaribu kuwashirikisha maafisa ugani sehemu unayo fugia? ulijaribu kuangalia maeneo ya jirani unapofugia labda kuna wafugaji wenzako amabao maambukizo mnapokezana bila kufanyia utabibu wa eneo hilo? umejaribu kumuuliza vyema vet aliyekuwa anakuja shambani kukukagulia mifugo? Mtumainie Mungu atakuonyesha njia ya kupita ktk hilo.
 
ufugaji-wa-nguruwe-e1661585920832-1024x1024.jpg
 
Back
Top Bottom