Hakuna namna unaeza pambana na changamoto kama hii isipokuwa kukubali kuwa huo ndio uhalisia wa maisha, pia kubali kuwa hauwezi kutoka kny hiyo ndoa ikiwa tayari mna watoto.
Na jukumu ulilo nalo kwa sasa nikujitransform kimtazamo (mindset) kutoka wewe wa zamani na kuwa wewe mkomavu.
Tafuta muda umuite, uongee nae au unaeza kumchartisha kwa watsap kishkaji like,
"Mke wangu, nimeona tuongee juu ya maisha yetu, la kwanza nimeona hapa swala si kukusamehe, bali kuongea mm na ww kwa pamoja tuone tunatoka wapi tunaenda na wapi."
"Jambo la msingi ni kwamba lazima sote tujue tayari tuna watoto ambao harakati zozote za maisha yetu ziwe positive au negative zinawaathiri moja kwa moja watoto wetu vivyo hivyo, ndio kusema hapa tungekuwa hatujazaa basi ilihitaji dakika chache kuachana kila mmoja wetu akashika lake"
"Lakini kwa vile tumeshazaa haiwezekani tena tukaachana, lazima tutafute njia ya kuondokana na sintofahamu iliyopo sasa na tuendelee kuwa positive baina yetu ili matunda yake yawe ni kuwalea vyema watoto wetu."
"Kwa kuanzia nashauri tusiongelee kabisa hiki kilichotokea, tuongelee tu hatima yetu, tujitafute tulipopoteana tujipate halafu maisha yaendelee"
Ishia hapo usiongeze neno tena bali muulize yeye ana maoni gani, kisha endelea kuchart nae kupitia maoni yake.
La kuzingatia:
Mwelekeo wa mazungumzo yenu yanaweza kuwa ya ufanisi sana ikiwa mtayafanya kwa kuchart kwa kuwa inakupa uwezo wa kufikiri kwa ndani na kuongea kutoka ndani kabisa pia itawasaidia kutafakari cha kusema hivyo kufanya mazungumzo yenu yawe ya ufanisi zaidi.
Pia shika usukani wa mazungumzo yenu yawe ya kutengeneza bond na si kutengeneza tension.
Hatua ya pili,
Kama baada ya kuchart kwa muda mtakosa cha kuongea bas ANZA MAISHA YA VITENDO, fanya vitu vya kumuonyesha upendo mkeo, fanya vitu km vile hakuna kilichotokea.
Mfano nakupa mmoja bure mwingine utalipia 😆,
-unaeza chukua embe na kisu ukamfata jikoni ukaanzisha story fupi au kuulizia chochote mradi unamsemesha ukaosha na kukata embe vipande na kuanza kula huku unamsemesha then ukacoment kuhusu embe kuwa ni tamu then ukacoment kumpa na yeye, akikataa mwambie umlishe, akikataa mwambie kwa utani "maembe yanasaidia kuongeza nyege", hapo utaanza kumvutia kingono.
Niendelee hapa au nije DM?