Naomba ushauri kuhusu contemporary

Naomba ushauri kuhusu contemporary

TZ-1

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
4,321
Reaction score
7,501
Habari wadau , kwanza nadhani wengine ndio itakuwa ni mara yao ya kwanza kuona Tofali nyekundi ya block.

Nirud kwenye mada jengo limejengwa kwa mchoro wa kupaua kikawaida ila sasa kutokana na hali kuwa ya ukata/ngumu na bati zipo juu hamna uwekezano wa jengo hili likapauliwa kama mtindo wa ki south (kuficha bati ) lakn pia isipotezi muonekano.

Polen kwa muandko m-baya.
Nasubiri comment zenu.

IMG_20210124_142559_4.jpg

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
wala usijaribu Contempo utalia,
atakuja fundi hapa na kusema 'ooh, mara ipate close supervision nzuri', blah blah kibao,
akimaliza kazi unamlipa HUMUONI tena
ikija Vuli na Masika, aah mbona utaipata fresh
 
Mvua zinanyesha n atuloi Mbona. Ukipata fundi mzuri akuna shida hata tone.
 
Ushauri wangu,

1. Kunabidilisha muonekano wa nyumba yako na kuifanya iwe contemporary kwa kigezo Cha kukwepa gharama naona sio sahihi Kwani contemporary inahitaji nondo nyingi pamoja na cement kwaajili ya slab (gutters) hivyo gharama hukalibiana isipokuwa tu utapunguza idadi ya bati na kuongeza nondo na cement. ( Jenga contemporary kwa kigezo Cha kuipenda sio kupunguza gharama).

2. Nyumba yako imedizainiwa kuwa na bati za kawaida utakapo amua kuibadilisha na kuwa contemporary haitokuwa na mvuto sana kwani, contemporary inatips zake za kuidesign kuanzia kwenye floor plan mpk juu ikupata muonekano mzuri. Aidha upate mtaalam mbobezi wa kudesign contemporary itakuwa vizuri zaidi
 
Tuanzie kwenye location ya site yako unaijenga sehemu gani yenye mvua za kiasi? au mvua y kutosha? . Kwa kuangalia aina ya matofali uliyotumia inaonyesha unaijenga sehemu yenye mvua nyingi na mpaka kwenye stage ya ujenzi uliyofikia ni dhahiri kua mjengo umedesigniwa kuwa na pitched roof na sio flat roof .
Kama unataka kwenda na option ya contemporary kwa ajili ya kusave construction cost mpak hapo ulipofikia kwenye ujenzi wako hio itakua ni wrong approach kwa sababu itakutaka kutumia gharama nyingine ya kubadilisha structure ya nyumba yako iweze kuruhusu upitishaji wa maji toka kwenye paa mpka ardhini na pia itahitaji uiongezee urembo zaidi ili kuvutia maana contemporary inaitaji urembo mwingi.
Kama unataka contemporary kwa kua umezipenda kulingana na location ya site yako inaonyesha ni sehemu yenye mvua nyingi inaweza kuwa ni nyanda za juu kusini .Hivyo maamuzi ya kuezeka na flat roof hayatakua sahihi saana ikiwa hata kama utapata fundi mzoefu akafanya kazi hio basi jua kabisa ujiandae kwa maintainance cost kila baada ya kipindi fulani ili upake tena water proofing material ili uzuie isivuje pia uliende kuta zako.
NB. Nenda na option ya paa la kawaida kwa faida zaidi.
 
Blessed
Tuanzie kwenye location ya site yako unaijenga sehemu gani yenye mvua za kiasi? au mvua y kutosha? . Kwa kuangalia aina ya matofali uliyotumia inaonyesha unaijenga sehemu yenye mvua nyingi na mpaka kwenye stage ya ujenzi uliyofikia ni dhahiri kua mjengo umedesigniwa kuwa na pitched roof na sio flat roof .
Kama unataka kwenda na option ya contemporary kwa ajili ya kusave construction cost mpak hapo ulipofikia kwenye ujenzi wako hio itakua ni wrong approach kwa sababu itakutaka kutumia gharama nyingine ya kubadilisha structure ya nyumba yako iweze kuruhusu upitishaji wa maji toka kwenye paa mpka ardhini na pia itahitaji uiongezee urembo zaidi ili kuvutia maana contemporary inaitaji urembo mwingi.
Kama unataka contemporary kwa kua umezipenda kulingana na location ya site yako inaonyesha ni sehemu yenye mvua nyingi inaweza kuwa ni nyanda za juu kusini .Hivyo maamuzi ya kuezeka na flat roof hayatakua sahihi saana ikiwa hata kama utapata fundi mzoefu akafanya kazi hio basi jua kabisa ujiandae kwa maintainance cost kila baada ya kipindi fulani ili upake tena water proofing material ili uzuie isivuje pia uliende kuta zako.
NB. Nenda na option ya paa la kawaida kwa faida zaidi.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Habari wadau , kwanza nadhani wengine ndio itakuwa ni mara yao ya kwanza kuona Tofali nyekundi ya block.

Nirud kwenye mada jengo limejengwa kwa mchoro wa kupaua kikawaida ila sasa kutokana na hali kuwa ya ukata/ngumu na bati zipo juu hamna uwekezano wa jengo hili likapauliwa kama mtindo wa ki south (kuficha bati ) lakn pia isipotezi muonekano.

Polen kwa muandko m-baya.
Nasubiri comment zenu.

View attachment 2050253

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
Nakushauri upauwe kawaida tu
 
Unataka uweke swimming pool au bwawa la kufugia samaki juu ya nyumba. Paua kawaida.
 
Ushauri wangu,

1. Kunabidilisha muonekano wa nyumba yako na kuifanya iwe contemporary kwa kigezo Cha kukwepa gharama naona sio sahihi Kwani contemporary inahitaji nondo nyingi pamoja na cement kwaajili ya slab (gutters) hivyo gharama hukalibiana isipokuwa tu utapunguza idadi ya bati na kuongeza nondo na cement. ( Jenga contemporary kwa kigezo Cha kuipenda sio kupunguza gharama).

2. Nyumba yako imedizainiwa kuwa na bati za kawaida utakapo amua kuibadilisha na kuwa contemporary haitokuwa na mvuto sana kwani, contemporary inatips zake za kuidesign kuanzia kwenye floor plan mpk juu ikupata muonekano mzuri. Aidha upate mtaalam mbobezi wa kudesign contemporary itakuwa vizuri zaidi
Naunga mkono hoja!

Contemporary zinajengwa kwa sababu mtu anaipenda na siyo kwa ajili ya kupunguza gharama. Inawezekana gharama ikawa kubwa kujenga contemporary imara kuliko kuezeka kawaida.

Kama mtu anataka kuokoa gharama na kupata pa kujihifadhi imara, basi aezeke slope tu, yaani analaza mbao kadhaa na kupiga bati!

Uchunguzi ambao nimeufanya kwa macho, contemporary inatakiwa kujengwa kwa tofali imara, kupigwa plasta kwa simenti kali, na kupakwa rangi bora, tena baada ya kila muda mfupi. Hii ni kwa sababu ( wataalamu mtanisaidia), katika contemporay, ukuta unapambana na maji ya mvua kiasi kikubwa tofauti na muezeko wa kawaida, ambapo maji ya mvua yanaugusa ukuta kwa chini tu, kwani sehemu ya juu ya ukuta inakingwa na bati!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom