mkuu nilikuwa naamanisha gari hii kama unavyoiona kwenye picha. Ni suzuki kei na sio zile za kubeba mizigo carry.
Nice Car Selection...ni nzuri iko imara na ni modification ya Swift isipokuwa uwe makini usii-overload kwenye milima. Naamini unataka ya 660cc ili uwe na gari yenye fuel consumption ya pikipiki? chukua ambayo haina Turbo lakini ukitaka yenye bai ndogo ndani ya 6.0Mil tafuta ile ya mwaka 2005. Best wishes
ahsante kwa ushauri, nakaa jiran na main road na pia mizunguko yangu ni ya mjini naamin itanifaa. Pia nimeipenda kwa ajili ya fuel consumptions biashara yangu ndio inakuwa kwa hiyo nilikuwa nahitaji gari ambayo itanisaidia niweze ku save pesa.
Acha ubahili wewe.., kwanini usinunue Suzuki Escudo V6 yenye 4WD ili hata siki moja moja ukasalimie kijijini kwenu.., au mna lami huko kijijini kwenu..?!
Habari wakuu,...
Suzuki carry na sio Suzuki kei,spare zake zipo nyingi tu hapa mjini,kama unanunua, nunua yenye four wheel.
Nimekuja mkuu.
NUNUA GARI HIYO. Chukua non turbo (tena ningekushauri manual, sema watu wanaiogopa), hako ndugu yangu mafuta kananusa tu, ukiweka full tank unaendesha mpaka unakaonea aibu mwenyewe. Kako imara pia, hakaharibiki ovyo, hata spare parts sku hizi siyo tatizo mkuu gerezani hauwezi kukosa spare.