Naomba ushauri kuhusu gari aina ya Suzuki kei

Naomba ushauri kuhusu gari aina ya Suzuki kei

red apple

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
778
Reaction score
1,212
Habari wakuu,

Kwa wenye uzoefu wa magari naomba mnisaidie, nina bajeti ya shilingi milioni sita na ninafikiria kununua gari ya Suzuki kei. Nimechukua uamuzi huu kwa sababu kwa sasa ninafanya biashara ambayo hunilazimu kuwazungukia clients mjini mara kwa mara, na hivyo nimeona wengi wanalisifia gari hili kuwa linatumia mafuta vizuri.

Swali langu ni kuwa je ni vipi upatikanaji wa spea zake? na ubora wake je?

1583148902971.png

1583148931313.png
 
spea zake nyingi tu mkuu...na ni gari bora ziko za 4 wheel drive na 2 wheel drive, na zipo zenye gia 4 na zingine zina gia 5...kwa kazi yako inakufaaa sanaa maana zile ni kama shuttle vile...chukua tu mkuu...
 
nmeshakupataa mkuu....na mm nmeioana hiyo hiyo
 
Nice Car Selection...ni nzuri iko imara na ni modification ya Swift isipokuwa uwe makini usii-overload kwenye milima. Naamini unataka ya 660cc ili uwe na gari yenye fuel consumption ya pikipiki? chukua ambayo haina Turbo lakini ukitaka yenye bai ndogo ndani ya 6.0Mil tafuta ile ya mwaka 2005. Best wishes
 
Nadhani hamjamulewa,yeye anamaanisha Suzuki kei,inaonekana ndogo zadi ya raum old model
 
Nice Car Selection...ni nzuri iko imara na ni modification ya Swift isipokuwa uwe makini usii-overload kwenye milima. Naamini unataka ya 660cc ili uwe na gari yenye fuel consumption ya pikipiki? chukua ambayo haina Turbo lakini ukitaka yenye bai ndogo ndani ya 6.0Mil tafuta ile ya mwaka 2005. Best wishes

ahsante kwa ushauri, nakaa jiran na main road na pia mizunguko yangu ni ya mjini naamin itanifaa. Pia nimeipenda kwa ajili ya fuel consumptions biashara yangu ndio inakuwa kwa hiyo nilikuwa nahitaji gari ambayo itanisaidia niweze ku save pesa.
 
Acha ubahili wewe.., kwanini usinunue Suzuki Escudo V6 yenye 4WD ili hata siki moja moja ukasalimie kijijini kwenu.., au mna lami huko kijijini kwenu..?!
 
CYBERTEQ njoo huku. Ushauri wako ulinisaidia sana, naomba umpe na huyu avutiwe zaidi
 
Last edited by a moderator:
Acha ubahili wewe.., kwanini usinunue Suzuki Escudo V6 yenye 4WD ili hata siki moja moja ukasalimie kijijini kwenu.., au mna lami huko kijijini kwenu..?!

Muelewe jamaa bana, ANAHITAJI GARI YA MIZUNGUKO YA MJINI KWA AJILI YA KUHUDUMIA WATEJA WAKE, kwa maana hiyo anataka economical, sasa unavomwambia anunue V6 umejuaje kama hana V8 au hana shida na kwenda na gari kijijini kwao anapanda basi tu. Tumshauri kulingana na mahitaji yake.
 
Habari wakuu,...

NUNUA GARI HIYO. Chukua non turbo (tena ningekushauri manual, sema watu wanaiogopa), hako ndugu yangu mafuta kananusa tu, ukiweka full tank unaendesha mpaka unakaonea aibu mwenyewe. Kako imara pia, hakaharibiki ovyo, hata spare parts sku hizi siyo tatizo mkuu gerezani hauwezi kukosa spare.
 
Ahsante sana kwa ushauri mkuu, nimepata kitu hapa, kweli nimeamini Jf ni kisima cha maarifa.
 
Nataka ninunue hii suzuki kei nikaona nipite JF kama naweza pata chochote kuhusiana na suzuki kei, nashukuru nimepata
 
Hivi vigari ni vya ajabu sana, kama suala ni fuel consumptions bora uchukue vitz ya cc 990 maana inapishana kidogo mno ulaji wa mafuta halafu spea za kumwaga, hizo kei spea zile ndogondogo huwa zinasumbua sana, km vile fan belt na vitu vidogovidogo, na ujinga wa Suzuki kadri unavyoitumia ndio matumizi ya mafuta yanavyoongezeka tofauti na toyota
 
Back
Top Bottom