Naomba ushauri kuhusu hili la kufukuzwa kazi na utumishi

Kwa taratibu za utumishi wa umma anaposhutumiwa kuwa ametenda kosa huwa mamlaka ya nidham inampa notes ya mashtaka ikiambatana na makosa uliyo yafanya na vifungu vya sheria ulivyo vunja katika utumishi wako na utaombwa upeleke utetezi wako ndani ya siku 14 ukishapeleka utetezi wako utasubir tume ya uchunguzi ije ikuhoji (kama utakuwa umekataa makosa lakini kama umekubali tume ya uchunguzi itaamua kukupa adhabu kutokana na makosa yko) sasa wewe ilikuwaje?
1.Uliletewa hati ya mashtaka?
2. Tume ya uchunguzi ilikuja kukuhoji kutokana ña makosa uliyo yafanya?
3. Kama ulijibu hiyo hati ya mashtaka uliomba ushauri kwa wataalam wanaojua taratibu na sheria za kiutumishi?
Hayo yote yalifanyika mkuu. Nashukuru
 
Kwan mwalimu sio mtumishi wa uma, hivi cwt ipo wapi
cwt, haina uwezo wa kumsaidia Mwl. Makatibu wa wilaya na mikoa ndio walipaswa kuwasaidia walimu kama hatua ya kwanza wanaposhitakiwa lkn cha ajabu wamejikalia tu ofisini na kusubiri mishahara mwisho wa mwezi hakuna wafanyalo kumsaidia mwalimu....

Ushauri wangu walimu achaneni na hicho chama cwt hakina msaada kwenu, ni tawi la ccm na kwa utawala huu wa magu ndio kabisa wamejifunika shuka hawataki hata kuona haki za walimu zinavyosiginwa.....
 
Pole sana. Ulifanya nini mpaka ukafukuzwa kazi na serikali? Utaratibu wa serikali kumfukuza mtu/mwajiriwa huwa ni mgumu sana. Ulifanya nini kilichokubuhu?
Asalam aleykum,

nilifukuzwa kazi na utumishi na mamlaka yangu ya nidhamu. TSD kwa sasa TSC. Mimi ni mwalimu, nilikata rufaa Tume ya Utumishi wa Umma. Nao walikataa rufaa yangu. Nikakata rufaa kwa Rais. nako rufaa ilikataliwa. Nimeenda mahakama kuu division ya kazi.

Je nikishinda kesi hii naweza rudishwa kazini!? Na utaratibu wa kesi ukoje?
Maana nasikia eti shauri likitoka hapo linakuja CMA.

Nawasilisha mnisaidie
 
Una maana gani kusema wanajua huna pakwenda
Utaenda kulalamika wp upate haki yako, Mf: TSC wilaya wakikupiga chini rufaa unakata TSC makao makuu Dodoma ambako % ya kutoboa ni ndogo sn kama ngamia kupenya tundu la sindano, ni sawa Na kesi inayomuhusu tumbili aiamue nyani,

Ukitoka hapo kama huko bado hujatoboa unakata rufaa kwa Rais, huyu ambae kwake watumishi ni kama vibaka tu, ikumbukwe zamani rufaa zilikuwa zinaenda Tume ya utumishi wa umma ambao walikuwa wanazingatia maadili ktk kushughulikia rufaa,

So survival chance ya kutoboa kwa presidaa ni ngumu zaidi kwanza sababu yy sio anaye deal na rufaa bali watu tu wakawaida waliopo ikulu, embu nambie unapakwenda hapo???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TSC wilaya alinambie siwezi toboa kokote. Ni kweli mpaka ikulu sikutoboa. Alivosikia nimeenda mahakamani amechkia kweli. Siku tumeonana na yule katibu kanambia mi msumbufu!!
 
Kama presidaa nae atazingua nenda high court ukaombe judicial review, ni heri kesi kwenda kumalizikia court kuliko kwenye vikamati uchwara vya TSC ambavyo mostly vinaangalia posho za kikao na kukandamiza maticha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiko iliko mkuu. Nashukuru kwa ushauri
Pambana mkuu, najua unapitia kipindi kigumu sana kwenye maisha, ila kwa kuongezea kidogo ungemtafuta wakili akawa anakupa miongozo ya kisheria, pia sio mbaya ukawatafuta hao viongozi privetly kuongelea swala lako kwa kina.
I feel your pain.
 
Mkuu nashukuru. Kiukweli nina wakili.
Pambana mkuu, najua unapitia kipindi kigumu sana kwenye maisha, ila kwa kuongezea kidogo ungemtafuta wakili akawa anakupa miongozo ya kisheria, pia sio mbaya ukawatafuta hao viongozi privetly kuongelea swala lako kwa kina.
I feel your pain.
Nashukuru mkuu. Ndio nina wakili
 
Hawakuniita
Kwa nini Ofsi ya Rais hawakukusikiliza? Walisema uamuzi wa TSC ulikuwa sahihi au walisema rufaa yako ni incompetent?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilipopeleka tu rufaa niaambiwa nisubiri uamuzi. Nilisubiri mwaka mzima kimya. Nilipoenda ikulu nikaambiwa barua zangu hazipo. Bahati nzuri nilikuwa na risiti ya kutuma. Nilituma kwa EMS. kuna mtu pale mapokezi ikulu alinihurumia sana. akasema kama kuna nakala nikatume. so nikafanya hivyo. hukumu ikakubaliana na maamuzi ya awali mkuu.
 
Vipi hukumu yako kaka nitafute INBOX
 
Hawakuniita

Nilipopeleka tu rufaa niaambiwa nisubiri uamuzi. Nilisubiri mwaka mzima kimya. Nilipoenda ikulu nikaambiwa barua zangu hazipo. Bahati nzuri nilikuwa na risiti ya kutuma. Nilituma kwa EMS. kuna mtu pale mapokezi ikulu alinihurumia sana. akasema kama kuna nakala nikatume. so nikafanya hivyo. hukumu ikakubaliana na maamuzi ya awali mkuu.
Wanadai mara nyingi ngumu maamuzi kutenguliwa
 
Back
Top Bottom