Naomba ushauri kuhusu huyu bodaboda

Naomba ushauri kuhusu huyu bodaboda

Kuna kazi ya kumsimamia bodaboda nilipewa. Makubaliano ilikua alete 280k kila mwezi baada ya miezi 10 pikipiki itakua ya kwake, sasa uletaji wa hesabu umekua ukisua sua ana malimbikizo ya almost miezi mitatu, nataka kumwambia arudishe pikipiki tuvunje mkataba ila pesa ambayo bado hajaleta ni nyingi sana almost laki 8 kwaiyo siwezi kuipotezea hela yote.

Naweza kuchukua pikipiki na nikamdai kiasi kilichobaki? Na nikishaichukua pikipiki nitamshurutisha vipi alipe angalao hata nusu ya pesa anayodaiwa?

Naombeni ushauri wenu
Kabla ya kumshurutisha muiite kaa nae chini muzungumze muulize tatizo nini...
 
Kuna kazi ya kumsimamia bodaboda nilipewa. Makubaliano ilikua alete 280k kila mwezi baada ya miezi 10 pikipiki itakua ya kwake, sasa uletaji wa hesabu umekua ukisua sua ana malimbikizo ya almost miezi mitatu, nataka kumwambia arudishe pikipiki tuvunje mkataba ila pesa ambayo bado hajaleta ni nyingi sana almost laki 8 kwaiyo siwezi kuipotezea hela yote.

Naweza kuchukua pikipiki na nikamdai kiasi kilichobaki? Na nikishaichukua pikipiki nitamshurutisha vipi alipe angalao hata nusu ya pesa anayodaiwa?

Naombeni ushauri wenu
Mbona hili sio jukwaa la madeni
 
Hiyo pikipiki ushaingia hasara. Kuendelea kumuachia huyo bodaboda ni sawa na kuipoteza.

Chagua moja. Kuipoteza kwa kumuachia ama kuikubali hasara iliyopo kwa kuichukua na kuiuza.
Sio yangu mkuu nimepewa niisimamie tu maana mwenyewe yupo mbali, kuirudisha bila angalao hata nusu ya hesabu anayodaiwa sasa mwenye mali atanielewa kweli
 
kabla ya kumshurutisha muiite kaa nae chini muzungumze muulize tatizo nini...
Nilishafanya ivyo ila sababu haziishi nilichoamua ni kuvunja mkataba ila siwezi kumwachia hela yote iyo alipe angalao nusu ya anayodaiwa nahitaji kujua namna ya kumshurutisha alete hela je nikimpeleke polisi au niende kwake nikachukue chochote nitakachokuta nishike kama dhamana ya deni? Yeye ni fundi ujenzi kuna sehemu wakijenga bado hawajalipwa ndo aliniambia wakilipwa anamaliza deni nakimshitaki kama ni kweli hajalipwa inawezakana nikapata kibali cha kuchukua yale malipo yake?
 
Sio yangu mkuu nimepewa niisimamie tu maana mwenyewe yupo mbali, kuirudisha bila angalao hata nusu ya hesabu anayodaiwa sasa mwenye mali atanielewa kweli
Sasa chagua moja hapo. Uirudishe hivyo hivyo ukubali hasara na kupata nusu Shari kutoka kwa mmiliki ama uendelee kuiacha kwa huyo boda mhuni halafu ipotee kabisa uje kupata Shari kamili toka kwa mmiliki.
 
Kwa hapo nimekuelewa nitaichukua mkuu ila kwa iyo hesabu ambayo bado hajaleta unanishauri nini mkuu ninwachie kabisa yaani laki 8+ asilete hata buku?, hakuna namna ya kumshnikiza hata kiroho mbaya poa tu. Nataka nimweke ndani mkewe ambae ndio mdhamini wake kwenye mkataba labda anaweza kuleta pesa, nitakua nimefanya vibaya hapo?
 
Bodaboda ni mtu hana kitu zaidi ya uume wake. Hana kitu kabisa. Anaendesha boda haweki hata akiba , atakupa nn?

Kama aliichukua pikipiki yako kwa mgongo wa mdhamini kambane mdhamini wake. Vinginevyo muache endelea kutafuta hela
 
Tatizo ukishamuachia dereva hesabu yeye anaipangia matumizi kama yake vile. Inatakiwa uhakikishe kila mwezi hesabu imeletwa la sivyo unavunja mkataba kabla hasara haijawa kubwa.
 
Sema na mandonga ndo awe agent wa kumdai hilo deni.Sema mpange kabisa kuwa ikitoka laki nane mbili zake ama tatu la sivo utajuta.Make mkwara wake unatokwa roho.
 
Bodaboda ni mtu hana kitu zaidi ya uume wake. Hana kitu kabisa. Anaendesha boda haweki hata akiba , atakuoa nn?

Kama aliichukua pikipiki yako kwa mgongo wa mdhamini kambane mdhamini wake. Vinginevyo muache endelea kutafuta hela
Sawa mkuu nimekuelewa, acha nifanye ivyo.. asante sana
 
Ulimuacha miezi mi3 yote ya nini?. Umefanya uzembe Sana. Kwanza siku hizi wanafanya kwa wiki Au siku kumi. Akizingua wiki moja Au mbili inachukuliwa chombo. Cha msingi wewe chukua mashine na sahau hicho kiasi.
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom