Kwanza kabisa na kabla ya yote, pole sana ndugu kwa changamoto hiyo iliyokupata.
Kwa uelewa wangu kuhusu hilo ni kwamba, kama bado ulikuwa katika majaribio na haukuwa katika mkataba wa kikazi basi unaweza usiwe na haki yoyote ile ya kudai au madai.
Kwa sababu, ili uweze kudai haki, kitu cha msingi ni mkataba uliopo baina yako na kampuni husika ambapo kama ikitokea kama hivyo kwamba hutakiwi tena basi kunakuwa na masuala mbalimbali yaliyomo kimkataba yatakayokupa uwezo wa kuyadai.
Hayo ni maoni yangu.