Naomba ushauri kuhusu kuachishwa kazi

Naomba ushauri kuhusu kuachishwa kazi

Queen Priya

Senior Member
Joined
Jul 15, 2018
Posts
100
Reaction score
97
Mimi ni mwajiriwa kwenye kampuni ila nilikuwa bado sijapewa mkataba na niliambiwa baada ya miezi sita ndio muda wa majaribio utaisha.

Kabla ya miezi sita kuisha, ikiwa ndio kwanza nina miezi miwili inaenda mitatu boss kaniita na kuniambia sijafikia kiwango cha utendaji mzuri wa kazi hivyo napaswa kuondoka kazini kwasababu hanihitaji tena.

Je, kuna haki yoyote natakiwa kudai? Naombeni ushauri wenu kwani nipo kwenye mawazo mazito sana.
 
Kwanza kabisa na kabla ya yote, pole sana ndugu kwa changamoto hiyo iliyokupata.

Kwa uelewa wangu kuhusu hilo ni kwamba, kama bado ulikuwa katika majaribio na haukuwa katika mkataba wa kikazi basi unaweza usiwe na haki yoyote ile ya kudai au madai.

Kwa sababu, ili uweze kudai haki, kitu cha msingi ni mkataba uliopo baina yako na kampuni husika ambapo kama ikitokea kama hivyo kwamba hutakiwi tena basi kunakuwa na masuala mbalimbali yaliyomo kimkataba yatakayokupa uwezo wa kuyadai.

Hayo ni maoni yangu.
 
Queen Priya, Kwanza napenda nikupe pole kwa changamoto iliyokukuta, lakini utambua njia moja ikifungwa, kuna njia nyingine inafunguliwa, kuwa na imani.

Tukirudi kwenye mada:

Kwa haraka haraka ni kwamba huna uthibitisho kuwa ni mfanyakazi wa hiyo kampuni, ni kama ulikuwa unajitolea ili uwashawishi wakupe kandarasi bahati mbaya umeshindwa kuwashawishi.

Binafsi sioni kama huna haki hapo maana hata waliopo kwenye uangalizi wanakwa na mkataba ambao unaelezea makubaliano ya muda wa kuwa kwenye uangalizi na vipengele vyake.
 
Unapoajiriwa na kisha ukakubaliana na muajiri wako kwamba utakuwa kwenye kipindi cha matazamio kwa muda wa miezi tatu ama sita, na ndani ya muda wa matazamio kwa bahati mbaya uka underperforme, hapo hautokuwa na haki ya kulipwa chochote zaidi ya mshahara wako wa siku ama muda uliofanya kazi.

Pole sana binti.
 
Kipindi cha probation ni kipindi cha unafiki, yaani inabidi uwe mfanyakazi bora kubembeleza ajira. Kama ni underperformance ndio basi tena.
 
Hebu weka sawa hapa please.

Ulikuwa kwenye probation ya miezi sita, je ulikuwa nao mkataba wa hiyo probation ya miezi sita? Kama hata huo mkataba wa probation hawakukupa basi upo upenyo unaweza ukapitia
 
Pole sana. Kama hautojali unaweza kuniambia ulisomea nini? Na upo mkoa gani?
 
Back
Top Bottom