Ni rahisi sana. Ukishamudu kuinyoosha na kukata kona vizuri basi zingatia namna rahisi za kuwasha na kuzima kama hivi hapa chini:
KUONDOA AU KUENDESHA GARI.
Unapokuwa umekagua gari lako na kulikuta liko katika hali nzuri sasa unataka kuliendesha na kuanza safari na gari lako, unapoingia kwenye gari na kuikuta iko katika gea namba moja basi sasa unapaswa kufanya maswala yafuatayo.
i. Weka switch/ yaani ufunguo wa gari katika sehemu yake
ii. Kanyaga clutch mpaka mwisho
iii. Ondoa gea namba moja na kuliweka gari huru yaani free
iv. Ondoa mguu kwenye clutch
v. Anza kuwasha ufunguo wa gari Satrt/Switch gari
vi. Sikiliza muungurumo kidogo
vii. Kanyaga clutch mpaka mwisho/pamoja na brake kulisaidia gari lisiweze kurudi nyuma
viii. Ondoa gari kutoka kwenye free mpaka kwenye nambari moja gea hii mara nyingi hujulikana kama gea ya kuondokea
ix. Legeza mguu wa kwenye clutch mpaka unasikia gari kama inaondoka hivi mlio unakuwa umebadilika na unakuwa constant
x. Kumbuka kutoa handbrake
xi. Ongeza mafuta kidogo na na kulegeza clutch na gari litaanza kuondoka na linapoondoka achia clutch, lakini usiachie ghafla, taratibu baada ya kuona baada ya kuona gari liko kwenye mwendo wa kawaida
xii. Lipe gari nguvu kwa kuongeza mafuta na badilisha gea nambari moja kwenda nambari mbili, unapobadilisha gea hakikisha kuwa unaachioa accelerator na kukanyaga clutch na baada ya gea kuingia unaachoia clutch na unakanyaga acceleretaor
xiii. Utaendelea na safari kwa kubadilisha gea nambari mbili mpaka tatu na kuendelea
Kumbuka gea nambari moja sio ya kutembelea hivyo usiiache kwa muda mrefu bila ya kuibadilisha