Wadau na wataalamu nawasalimu kwa pamoja,
Nina kashamba kangu mahali mkoa wa pwani Kama heka 20.
Nafikiria huu msimu wa mvua nipeleke huko miti michache nikaoteshe kuzunguka eneo lote sasa mm nimewaza niioteshe miti aina ya eucalyptus.
Je, Inastawi eneo la pwani?
Pia miti hiyo imeruhusiwa kuoteshwa na mtu yeyote?
Kwa yeyote mwenye ushauri wa ziada namkaribisha
View attachment 2034387View attachment 2034388View attachment 2034389
Kuna kipindi hii miti ilipigwa marufuku hususani karibu na maeneo ya maji
Kwanini usioteshe Miche ya matunda....fikiria ...MACHUNGWA,,,NDIMU.....LIMAO....hii itakupa tija kwa muda mfupi
Pambana kidogo kidogo....utatoboa
Ila mkuu, kilimo na ufugaji kwa scale ya mkulima au Mfugaji Mdogo na wakati ni changamoto saana.. tena saana unatakiwa ujipange sio kidogo,,,,otherwise utafilisika
Nikushirikishe machache
1- Kuna wafugaji kuingiza shambani kwako mifugo..
2-Kuna viongozi wa ......vijiji....... na vitongoji......majirani..... ukishaanza shughuli hawachoki kila siku kukupigia simu na kuanza kukuomba uwape bila kukufanyia lolote.
3. Waangalii wa shamba ...hawa wamekuwa ni changamoto saana wengi ni waongo..wezi ......wanatamaa..usipokuwa makini unaweza filisi mshaaaaaaahara wako....kama unawekeza kwa kutumia Mshahara
4.Kama Eneo lako lipo isolated.. kuna changamoto ya MOTO kipindi cha kiangazi..wafugaji lazima wachome moto ili wapate majani ya mifugo
Mengine wazoefu zaidi watasema
Kila la kheri .....ila tambua akili za kuambiwa changanya na za kwako
Ushauri wangu...kuwa na malengo dhabiti pambana kidogo kidogo