Naomba ushauri kuhusu ofa ya mshahara

Sasa kama hapo ulipo kukunja 40k kwa siku sio tatizo na kwa mwezi mshahara wako una range laki 6,7,mpaka 8 kwa nini ufukuzie kazi ya mhindi ya laki 5 na hapo ulipo unasema una uhuru wa kutosha hii mbona kama chai hivi.
 
Hii ndo, kutoka unakokufahamu kwenda usipokufahamu. Hapo tayari ni riski/hatari unaibeba.

Ili utoke unapokufahamu kwenye usipokufahamu LAZIMA na ni MUHIMU uwe na utofauti mkubwa wa mazingira ya kazi kati ya hivi au kwa kuviunganisha:
1: Kipato
2: Usalama wa mwendelezo wa kazi/job security.
3: Mazingira bora ya kazi
4: Matokeo ya 1, 2, na 3 kwenye maisha yako baada ya kazi.

A: Kama unayotarajia 1-4 ni bora kule unakoitwa kuliko ulipo, na huwezi kuyapata au kutengeneza mazingira ya kuyapata, nenda eneo jipya la kazi.

B: Kama 1-4 yanapatikana sehemu zote mbili basi pima kiasi chake na ujipime mazingira yako kwenye utekelezaji wa shughuli na uamue kwa kadri ya matakwa yako na kazi.

C: Kama 1-4 yanapatikana ulipo kuliko unakokwenda basi baki ulipo.
Mfano: kama mengine yako sawa, suala ni NSSF, unaweza kuboresha mwenyewe kwa kukata hela yako ya mshahara na kuweka UTT kama NSSF yako binafsi nk.

Fanya upembuzi yakinifu.
 
Baki huko Kibaha, hiyo kampuni ya Wahindi haina dalili nzuri.

Ukiwa Kibaha endelea kupiga kazi na jitahidi kusave unachopata.
 
Shukran mkuu nitatunza uaminifu
 
Shukrani mkuu nimekuelewa
 
Ahsante na poleni pia
 
Sasa kama hapo ulipo kukunja 40k kwa siku sio tatizo na kwa mwezi mshahara wako una range laki 6,7,mpaka 8 kwa nini ufukuzie kazi ya mhindi ya laki 5 na hapo ulipo unasema una uhuru wa kutosha hii mbona kama chai hivi.
Sio chai blood huu ni ukweli hapa nipo huru sana sema tu sababu sina mkataba
 
Nakushauri baki na kazi yako ya mwanzo. Wahindi, wachina ni pasua vichwa.
 
Shukrani sana chief nimekuelewa
 
True, plus na presha ya kazi.. amani inakosekana kabisa, unajikuta mtu huipendi kazi, hata kama inakupa maslahi. Kikubwa ni amani, kupitia amani utakua na moyo wa kujituma
 
True, plus na presha ya kazi.. amani inakosekana kabisa, unajikuta mtu huipendi kazi, hata kama inakupa maslahi. Kikubwa ni amani, kupitia amani utakua na moyo wa kujituma
Yes ni kweli coz siku ya pili nimeenda nikaskiza task zao halafu nikakumbuka kibaha pale mimi naishi kama boss nafanya kazi nikiwa na amani na boss ananiheshim sana pia tunapendana mno hapo hapo ham ya kufanya kazi masaki ikapotea
 
Baki hapo ulipo lakini zidisha uaminifu hiyo kazi itakupaisha na itakuwa na baraka ya ajabu.
Uaminifu, uaminifu na uaminifu ndio silaha yako kubwa katika hiyo kazi yako na utaona maajabu ya mafanikio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…