Naomba ushauri kuhusu ofa ya mshahara

Naomba ushauri kuhusu ofa ya mshahara

Tulia kwenye kazi yako ya sasa. Tafuta namba nzuri yakuongeza mapato kwenye hiyo kazi yako. Mshahara wa wahindi bado mdogo achana nao.
 
Mbona hesabu inakubakisha kwa ulipo una laki sita hadi saba...

Ni vipi uende kwenye laki nne, tano hadi sita?, na makato juu🤯🤯🤯🤯!????
 
Uko wapi ungesogea hapa nikutandike kofi la utambuzi kwanza kabla ya kukushauri. Umeajiriwa Kibaha na unataka uache kazi yenye uhuru uende kufanya kazi Masaki kwa Muhindi kisa laki tano.

Umbali wa Masaki na Kibaha gharama yake kwa mwezi utaiweza? Kuunganisha magari.

Utaweza afford gharama za kufanya kazi Masaki zenye tofauti kubwa sana na Kibaha?

Pressure ya kazi kwa Wahindi utaiweza, utawahi kazini, utaweza kuondoka umechelewa zile overtime, utaiweza foleni ya kutoka Masaki mida ya kazi wanyonge wote mnagombea daladala kuondoka?

Kuna mtu kakuroga unachukulia kazi yako kienyeji na mazoea. Ukiiacha hiyo bila kazi nyingine yenye mazingira mazuri zaidi unaweza poromoka kimaisha ukapiga zako miaka hata 15 hujawahi pata nafasi kama hiyo.
Shukrani nitazingatia ushauri
 
Usiende kwa muhindi ata akilanda dau akasema 700k.

Huko ulipo Kibaha mbali na mshahara mnono, jamaa anaonekana ana utu. Imagine hadi alikubaki uishi kwake, ni nni anaweza kufanya ivyo?

Hao wahindi siku ukipata ata emergency haujaenda kazini weeknlets day unaumwa au matatizo ya kifamilia watakata siku za malipo.

Endelea kufanya kazi Kibaha, hauna gharama kubwa za maisha na unazidi kujenga CV nzuri.

Endeleza pia uhaminifu si unaona wenyewe wameanza kukutafuta kwasababu ya uhaminifu na uchapa kazi.
Yeah mkuu jamaa ni zaidi ya ndugu na tuliunganishwa kariakoo na kampuni fulani ambayo mimi nilikuwa nachukua mafunzo hapo ila bado sikuwa nimepata ajira ndio jamaa alivyokuja akataka kuingia nao mkataba wakamwambia kama huna mtu ambae ayupo trained bac sisi tutakupa mtu wetu mtakubaliana nyinyi wenyewe ndio tukakutana na jamaa tukaanza kufanya kazi pamoja sasa hv ni miez kama 10 na tayari kaniamini mpaka kaniachia pesa za kuzungusha huo mradi nikae nazo mimi yeye nampa report tu jamaa ni sana kwa sasa ni zaid ya ndugu
 
Yaani hapo ulipo minimum ni 500K na hiyo hiyo minimum ndiyo unawaambia watu wakulipe kwa mkataba?

Hata hujawaambia kama utapata bima na allowance zingine?

Kazi hujaisema ili tujue kama inaweza kukupa kitu zaidi ya mshahara.

Kwa mtu ambaye una sehemu unatengeneza pesa ambayo determinant ni jinsi unavyofanya kazi 500K ni ndogo mno kulipwa kwa mkataba.

I hope utaona hili
Sawa mkuu nitazingatia hili
 
sasa Melancholic mbona unapotea umesema hapo unapofanya kazi sahivi kwa siku hukosi 40,000 hii ukikusanya kwa wiki moja unapata kama 200,000 ukifika mwezi ni kama 700,000..wahindi wanataka wakupe mkataba wa mwaka mmoja (wanaweza wasikuongeze tena) kwa mshahara wa 400,000 kwa mwezi..utakuwa bonge la mjinga ukikubali ofa yao yaani uache zaidi ya laki saba alafu ukachukue laki nne kwa mwezi.! mm nakushauri hao wahindi achana nao ukiona wanakung'ang'ania sana basi jua mambo ya nyota yanahusika lazima utakuwa na kipawa unacho ujijui tu washakuchunguza kiroho
Duuh inawezekana bro siwez bisha pia
 
Usinijibu kijingq, mimi sijaenda shule kusomea ujinga.

Kajisome upya, umesema "...mimi nachukua 60% na... kwa mwezi huwa inarange laki 7, laki 6 au laki 5 inategemea na mzunguko"..."kukunja 40k kwa siku ni jambo la kawaida."

Sasa 40 kwa siku ndiyo hesabu yake hiyo laki 5 au 6 au 7 uliyoandika?



Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Wewe bibi una matatzo sio bure
 
Wakuu hope mmeamka salama.

Nina jambo kidogo nahitaji ushauri ndugu zangu, Mimi ni kijana wa kiume ni mkaz wa Dar es salaam ila kwa sasa nipo mkoa wa pwani kibaha nimejiriwa na mtu binafsi tunalipana kwa % yeye anachuka 40% mimi nachukua 60% na pia kaniamini kwa kiasi kikubwa sana na kabla sijapata room huku kibaha kwa siku za mwanzo nilikuwa naishi kwake mpaka nilivyopata pesa ya kutosha ndio nikapanga room mpaka sasa tunafanya kazi pamoja na upendo.

Pale malipo kwa mwezi huwa inarange laki 7, laki 6 au laki 5 inategemea na mzunguko wa wateja kifupi kukunja 40k kwa siku ni jambo la kawaida.

Sasa tukiachana na hilo pia kuna kampuni X ya wahindi ipo masaki kuna mtu aliwapa info zangu wakanichek lengo ni kufanya kazi nao basi nikaenda ofisini kwao tukazungumza wakanifanyia interview mbili nikafaulu vzr wakasema wameridhishwa namimi so wanaomba tufanye kazi nikawambia sawa ila mjue mimi nimeajiriwa mahali so ni vema mnipe offer yenu nione kama ina maslahi wakasema aina tatzo nirudi tu home HR atanichek kwa Email yangu nikasema poa.

Kesho yake asubuhi HR akanichek anaomba nimtumie details zangu aniandikie mkataba nikawauliza why ntume taarifa zangu mniandikie mkataba wakati bado sijaskia offer yenu nikawaambi kwa navyofaham mimi hizi huwa ni process za mwisho kabisa baada ya kukubalia wakasema sawa tutakupa offer yetu.

Baadae HR akanichek akaniambia offer yao ni 400k kwa mwezi nikachomoa sasa baadae simu zikawa nyingi wahindi wanapiga simu hao wakiniomba nikubali kufanya nao kazi sababu hata kama mshahara sio mkubwa sana ila wananipa mkataba wa mwaka mmoja nikachomoa nikawambia wekeni 500k mezani wakasema ngoja wakadiscus jibu likaja kuwa sababu ndio kwanza ninaanza na utendaji wangu wa kazi awaujui so ni vema nianze tu na hiyo 400k nikakataa.

Ikapita kama siku tatu jana meneja wao wa mauzo ni mdada akanipigia tena anaomba niende kufanya nao kazi na niseme pesa nayotaka kulipwa ukiachana na hiyo 400k. Nikamwabia nitakutafuta nkitulia sasa wakuu ebu naombeni mnishauri nipange mshahara kiasi gani sababu hata hiyo 500k naiona ndogo kulingana na kazi nitakazokuwa nafanya halafu kwa huku nilipo naiingiza tu wala siangaiki sana na kazi ni chache japo ni kweli sina mkataba.

Naombeni ushauri wa mapana hapo kazi ipi ni bora zaidi hata hata kama mishahara inaweza kuwa sawa.

Na vp kwa watu mnaofanya kazi kwenye taasisi mbalimbali au serikali mtu anaelipwa 500k ukitoa makato ya serikali na Nssf sijui unaweza kubaki na bei gani? Poleni kwa maelezo marefu nipo hapa nasubiri maoni yenu.
Yani mshahara unashuka, kazi ni kwa Mhindi bado ni Masaki.
Dogo achana na mambo ya wahindi kwanza kazi utaiona Chungu
 
Back
Top Bottom