Naomba ushauri kuhusu ofa ya mshahara

Naomba ushauri kuhusu ofa ya mshahara

Boss mzungu sana huyu ataki kunibana sababu bado anavyanzo vingine vya mapato
Kwakifupi we ndo boss haf uache kua boss ukaajiriwe?? Unless utakua umetudanganya!!!! Kwamba kwa siku unaweza kupata 40k means mwez una uhakila wakupata si chini ya 1m halafu uache ukaajiriwe Tena kwa mshahara wa 500k does it make sense to you??
Em tuambie ukweli tukushauri vizuri hayo maelezo uliyotoa sio sahihi period!
 
Wakuu hope mmeamka salama.

Nina jambo kidogo nahitaji ushauri ndugu zangu, Mimi ni kijana wa kiume ni mkaz wa Dar es salaam ila kwa sasa nipo mkoa wa pwani kibaha nimejiriwa na mtu binafsi tunalipana kwa % yeye anachuka 40% mimi nachukua 60% na pia kaniamini kwa kiasi kikubwa sana na kabla sijapata room huku kibaha kwa siku za mwanzo nilikuwa naishi kwake mpaka nilivyopata pesa ya kutosha ndio nikapanga room mpaka sasa tunafanya kazi pamoja na upendo.

Pale malipo kwa mwezi huwa inarange laki 7, laki 6 au laki 5 inategemea na mzunguko wa wateja kifupi kukunja 40k kwa siku ni jambo la kawaida.

Sasa tukiachana na hilo pia kuna kampuni X ya wahindi ipo masaki kuna mtu aliwapa info zangu wakanichek lengo ni kufanya kazi nao basi nikaenda ofisini kwao tukazungumza wakanifanyia interview mbili nikafaulu vzr wakasema wameridhishwa namimi so wanaomba tufanye kazi nikawambia sawa ila mjue mimi nimeajiriwa mahali so ni vema mnipe offer yenu nione kama ina maslahi wakasema aina tatzo nirudi tu home HR atanichek kwa Email yangu nikasema poa.

Kesho yake asubuhi HR akanichek anaomba nimtumie details zangu aniandikie mkataba nikawauliza why ntume taarifa zangu mniandikie mkataba wakati bado sijaskia offer yenu nikawaambi kwa navyofaham mimi hizi huwa ni process za mwisho kabisa baada ya kukubalia wakasema sawa tutakupa offer yetu.

Baadae HR akanichek akaniambia offer yao ni 400k kwa mwezi nikachomoa sasa baadae simu zikawa nyingi wahindi wanapiga simu hao wakiniomba nikubali kufanya nao kazi sababu hata kama mshahara sio mkubwa sana ila wananipa mkataba wa mwaka mmoja nikachomoa nikawambia wekeni 500k mezani wakasema ngoja wakadiscus jibu likaja kuwa sababu ndio kwanza ninaanza na utendaji wangu wa kazi awaujui so ni vema nianze tu na hiyo 400k nikakataa.

Ikapita kama siku tatu jana meneja wao wa mauzo ni mdada akanipigia tena anaomba niende kufanya nao kazi na niseme pesa nayotaka kulipwa ukiachana na hiyo 400k. Nikamwabia nitakutafuta nkitulia sasa wakuu ebu naombeni mnishauri nipange mshahara kiasi gani sababu hata hiyo 500k naiona ndogo kulingana na kazi nitakazokuwa nafanya halafu kwa huku nilipo naiingiza tu wala siangaiki sana na kazi ni chache japo ni kweli sina mkataba.

Naombeni ushauri wa mapana hapo kazi ipi ni bora zaidi hata hata kama mishahara inaweza kuwa sawa.

Na vp kwa watu mnaofanya kazi kwenye taasisi mbalimbali au serikali mtu anaelipwa 500k ukitoa makato ya serikali na Nssf sijui unaweza kubaki na bei gani? Poleni kwa maelezo marefu nipo hapa nasubiri maoni yenu.
Jichanganye kwa Muhindi ulie kilio cha Mtema kuni
 
Nenda tu Shaban ukitoka hapo kwa Muhindi utaweza kufanya kazi popote duniani
 
Kwa wahindi inabidi uwe mtu wa kujipendekeza sana
 
Umesema wahindi!!
Fanya na huyo mbongo tuu.
Nasikia Wana Mambo mengi,siku ukitaka kuacha unaweza zushiwa kesi ukagaramikia Sana,yaani wakikubali kuja kutoka kwo utatoka ukiwa umechoka sana
 
Wahindi wana akili sana, kukupita wewe usiye mhindi. Hata ukiwaibia wanajifanya hawajui, kumbe washapiga hesabu mpaka za kuibiwa, wanakutumikisha ni lazima ulipe japo indirectly.

Ndiyo maaana mnaopenda wizi hamuwapendi wahindi.
Na ukizingua watakutengenezea kesi ,utalipa hadi akili ijae kichwani
 
Back
Top Bottom