Naomba ushauri kulingana kipato changu na maisha ninayoishi

Naomba ushauri kulingana kipato changu na maisha ninayoishi

Melancholic

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
3,076
Reaction score
5,483
Maisha ya kujitegemea nimeyaanza january mwaka huu na kipato changu kwa mwezi kina range 400k mpaka 600k.

Nimepanga chumba kimoja na choo ndani kodi nalipia 80k kwa mwezi,
Usafiri natumia 2k kwa siku,
Kula natumia 6k mpaka 10k

So nikipiga hesabu pesa ya usafiri na kodi pamoja kula nakuwa natumia 300k kwa mwezi.

Sasa wakuu nlikuwa nauliza kulingana na kipato changu nikweli nastahili kuishi hivi au matumizi yamekuwa makubwa sana? Na kama ni makubwa je nastahili kuishi kwenye gharama za kiwango gani ili pia niweze kufanya maendeleo.

NB: sina nyumba wala kiwanja na hata aset za ndani pia sijanunua zaidi ya kitanda tu.
 
Atleast umepata uthubutu wa kuanza. Hongera sana.

Katika uchumi, ikija topic ya "Money Management" tuna options mbili:
  1. Kucontrol matumizi au
  2. Kuongeza kipato
Sasa wewe kwa kusoma maelezo yako naona unataka kutumia option ya kwanza (1).

Tukianza na usafiri, unamaanisha kutoka nyumbani kwenda kibaruani. Ingawa haujaweka wazi ni upo mkoa gani, na umbali upi, ila unaweza kutafuta option ya pili kama vile kutafuta baiskeli, ila kutegemea unapokaa (jiografia).

Kula kwa siku 6-10k ni pesa ya kawaida ila unaweza kucontrol hapo. Jitahidi usivuke hapo.

Pahala pa kulala naona sawa, lazima tupumzushe fuvu mahala pazuri.

USHAURI:

Mbali na iyo nafasi yako inayokupa kipato, nashauri upambane uongeze source nyingine ya kipato (option 2).

Tuendelee kupambana, karibu kwenye maisha ya kujitegemea.
 
We tumia pesa, uweke unamuwekea nani?

Hapo naona huna matumizi mabaya, kula vizuri lala vizuri, usijibane bane, kinachobaki ndio ufikirie mengine, maisha mafupi haya.
 
We tumia pesa, uweke unamuwekea nani?

Hapo naona huna matumizi mabaya, kula vizuri lala vizuri, usijibane bane, kinachobaki ndio ufikirie mengine, maisha mafupi haya.
Sawa mkuu shukrani sana nimeelewa sana ushauri wako na nitaufuata
 
Hiyo ni anasa mkuu, kwa hicho kipato inabidi ushindie biscuit za tiffany na mo energy.
Mkuu sasa pesa nitakuwa naitafuta yanini kama afya yangu nitakuwa siijali
 
oa mkuu,, wanawake n wachumi wazuri sana😌
 
Nenda uswahilini kapange chumba cha 20,000 kwa mwezi. Kwa kipato chako chumba cha 80,000 kwa mwezi ni bonge la anasa
 
Maisha ya kujitegemea nimeyaanza january mwaka huu na kipato changu kwa mwezi kina range 400k mpaka 600k.

Nimepanga chumba kimoja na choo ndani kodi nalipia 80k kwa mwezi...
Mambo mengine yanategemea ukomavu wa ubongo kulingana na umri! Umri huu kimbizana na vibinti, disco, jichanganye ongea na watu upanue uelewa wa walimwengu! Hata tukikushauri yataingia sikio hili na kutokea sikio lile! Kwa umri wako umakini (concentration) ni sifuri!
 
Atleast umepata uthubutu wa kuanza. Hongera sana.

Katika uchumi, ikija topic ya "Money Management" tuna options mbil...
Shukran sana mkuu nilikuwa dar but kwasasa nipo kibaha maili moja ndiko nakofanyia kazi zangu. Nitajitadi pia kufanyia kazi ushauri wako.
 
Vyaa bure gharama, chumba cha bei ndogo, utapanga foleni ya chooni, kuna uti, unakosa privacy, usalam wako na vitu na mambo kibao, mantiki ya hela ni kurahisisha maisha .
 
Mambo mengine yanategemea ukomavu wa ubongo kulingana na umri! Umri huu kimbizana na vibinti, disco, jichanganye ongea na watu upanue uelewa wa walimwengu! Hata tukikushauri yataingia sikio hili na kutokea sikio lile! Kwa umri wako umakini (concentration) ni sifuri!
Sawa mkuu nashukuru pia
 
Back
Top Bottom