Naomba ushauri kulingana kipato changu na maisha ninayoishi

Naomba ushauri kulingana kipato changu na maisha ninayoishi

Vyaa bure gharama, chumba cha bei ndogo, utapanga foleni ya chooni, kuna uti, unakosa privacy, usalam wako na vitu na mambo kibao, mantiki ya hela ni kurahisisha maisha .
Daah mkuu hii point yako nimeielewa sana nitafanyia kazi ushauri wako hakika ulichokisema ni ukweli mtupu.
 
Maisha ya kujitegemea nimeyaanza january mwaka huu na kipato changu kwa mwezi kina range 400k mpaka 600k.

Nimepanga chumba kimoja na choo ndani kodi nalipia 80k kwa mwezi,
Usafiri natumia 2k kwa siku...
Naomba niweke ukweli ambao sikuwahi kuuelezea kokote pale wala kumwambia yoyote japo sina hakika kama formula hii ina apply kwenye maisha ya kila mtu.

Mimi kwa upande wangu nlikuwa napata 300k mpaka 400k kwa mwezi nkawa naishi chumba kimoja tu na kujibana mno full tumihogo mda mwengine napiga desh.

But nkasema haya maisha ninayoishi now si maisha ya umri wangu bali ni maisha ya kuishi kijana wa 18 to 20s yrs.

Nkapata kiasi fulani nkachukua upande mzima nkahamia ajabu kila nilchokua nakipata kwa mwezi nikawa nakipata kwa week na mda mwengine hata kwa siku inshort kipato changu kikakua.

Sikushauri uwe mtu wa anasa lakini kwa upande wangu naona kinachokuza uchumi wangu ni wingi wa majukum na investment's ninazojiwekea/tengeneza.

Hivyo ukijiwekea limit kuwa mimi kiasi changu ni kiasi kadhaa na kuridhika nacho basi usijekushangaa miaka nenda miaka rudi ukawa hapo hapo
 
Mkuu kama unataka ushauri na hakika unataka utoboe kimaisha fanya haya maamuzi.

a) Toka umepanga mpanga sasa una miezi 6. Lets say 6*80,000.. kodi tu vyeyewe umetumia 480,000 just 6 months.

Inaonekana we ni mtu mwenye expenditure kubwa sanaaaa. Cha kukushauri, kulingana na kipato chako, tafuta chumva yenye gharama nafuu zaidi ie singke ya 40,000. Hivyo kodi ya miezi 6 unatumua mwaka huku.

Kisha kwenye suala la chakula, nunua kibedi na hotpot. Jioikie chakula usiku cha kula mchana kazini. Pia kwenye manunuzi ya chakula nunua stick ya kutosha atleast 2 months.

Ishu ya usafiri pia angalia. Tenga peesa ya usafiri, jibane to the maximum. Jifunze kusave fedha, jiunge kwenye vikundi vya vijana huwa wanaita mchezo.

Ni hayo mdogo wetu, muda wako kupanbana
 
80 elfu kubwa, angalau 60 elfu, pia nunua vyakula uweke ndani uwe unajipikia , kupunguza kununua msosi usiku...
 
Jiulize una malengo gani ya kiuchumi ya muda mrefu na muda mfupi kisha jiulize utahitaji kiasi gani kutimiza malengo hayo halafu piga hesabu unatakiwa kusave kiasi gani ili kufikia malengo hayo.

Ukipata jibu utaamua uishi kwa kujibana au lah.

Sent from my SM-N950U1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom