Naomba ushauri kwa mdogo wangu kuhusu ajira ya Tutorial Assistant

Naomba ushauri kwa mdogo wangu kuhusu ajira ya Tutorial Assistant

Habarini ndugu zangu nilikuwanaomba ushauri kuna dogo langu anafundisha chuo kikuu cha Dar es Salaam kama Tutorial Assistant na kaitwa kufanya interview TRA kama Tutorial assistant.

Yuko anauliza je kuna umuhimu wa yeye kwenda TRA kufanya interview na akaachana na UDSM maana salary scale ya TRA ni nzuri na hajui kama kutakuwa na fursa mbalimbali kama allowances etc.

Nimeshindwa kumshauri moja kwa moja…naomba mawazo yenu wadau.

Ahsanteni.


Kama kweli ni tutorial assistant UD sizani kama hana uwezo wa kuamua hili, labda kama, au kujua la kufanya.
 
Mwambie akapige masters apate PUT 2 Sio salary mbaya kibongo bongo.

Na sidhani kama wanatofautina sana TRA interm of basic salary figures.

Ishu inakuja kwenye maokoto ya ziada.

Hayo Sasa apambana ayatafute kitaa.

Mtaa ndio wenye Hela.
 
Ndo maana yake. Ukishakua na ile check namba, kuhama kwake serikalini ni kwa kupitia mchakato ambao ni lazima uihusishe taasisi yako uliyopo (mkuu wa idara) kuanzia wakati wa kuomba kazi.

Na lazima mchakato uwe rasmi, na huko anakoenda wawe wametangaza nafasi za TRANSFER kutoka kwa watumishi walio taasisi zingine za serikali. Mchawi hapo ni hiyo check namba.

Asipoteze muda wake bure na kutafuta uhasama kwa wakuu wake wa kazi hapo UDSM.
Acha tu mzee hio check namba hizo ndio hasara zake.

Na wakuu wa kazi hawawezi kumpitishia barua yake kirahisi labda wawe wanajuana. Watamfanyia UKUDA na UNAA na UKAKSI hadi aichukie kazi.

Wakishajua tu dogo Yuko over ambitious (which is ok money wisely.)

Kuna bachelor Degree na masters ziko aspired kufanya kazi hizi Taasisi zenye maokoto mazuri zime stuck Huko Halmashauri zinakula TGS, TGTS, TGHS kwa manunung'uniko sana[emoji1]

HOD na ma-DED full UNAA na UKAKSI.
 
Kama nafasi zote ni za u-tutorial assistant iwe ni UDSM au TRA abaki hapo UDBS

Aendelee kupiga pindi, kuongeza elimu, afanye research papers na academic thesis za kutosha

Hatajuta. UDSM kunalipa
 
TRA kuna maokoto kibao mwambie aende TRA kule pesa unajiokotea tu hadi raha
Utaratibu ni kwamba kama anaweza kupata nafasi ya kwenda kufanya usaili anaweza kwenda kufanya usaili. Ikitokea amepata, (kwake haitakuwa ajira mpya, na hatapewa check number nyingine). Itabidi aombe uhamisho kwa kuandika barua kwa Katibu mkuu utumishi kupitia mwajiri wake wa sasa. Hapo comments za mwajiri wake wa sasa zitazingatiwa. Ukipata ajira kwenye utumishi wa umma hauwezi ukautelekeza halafu ukapata tena kwenye utumishi wa umma. Mfumo utakutema!! Kwa mfano kama akipata ajira TRA halafu akaamua kwenda huko kinyemela kwa kuacha kazi nyingine ya umma, hatafanikiwa.
Kama aliomba hizi nafasi huku akiwa ni mwajiriwa tayari wa UDSM na hakupitishia barua yake kwa mwajiri, hapo wala asijihangaishe kwenda huko kwenye usaili. Lakini kama alipata hapo UDSM wakati alikuwa ameomba TRA hapo hana kosa lolote na anaweza kufanya kama nilivyoshauri hapo juu. Tutorial assistant ni kazi kwenye mkondo wa kitaaluma na kuendelea kwake lazima aendelee kupiga kitabu hadi PhD huku ukiandika papers!! Ni mkondo mgumu!! Huko TRA ni mkondo wa kula asali tu ya nyuki wadogo!!​
 
Hapana maokoto yapo ila kuna kuzidiana pia scale za TRA naona zipo tofauti na hizi za serikali…yaani TRA ni kama wana scale zao wenyewe na wanajiendesha….tofauti na udsm iko chini ya mishahara ilopangwa na wizara ya elimu
Udsm maokoto yatoke wapi mzee?. Kama associate lecture aliyekomaa miaka zaidi ya 10 anasimamia USD 2500 si Bora ukomae upate InGOs
 
Hata TRA wenye maokoto ni wale wanakaa mezani kuongea na walipa kodi hawa wengine ni ngumu labda seminar na overtime
 
Habarini ndugu zangu nilikuwanaomba ushauri kuna dogo langu anafundisha chuo kikuu cha Dar es Salaam kama Tutorial Assistant na kaitwa kufanya interview TRA kama Tutorial assistant.

Yuko anauliza je kuna umuhimu wa yeye kwenda TRA kufanya interview na akaachana na UDSM maana salary scale ya TRA ni nzuri na hajui kama kutakuwa na fursa mbalimbali kama allowances etc.

Nimeshindwa kumshauri moja kwa moja…naomba mawazo yenu wadau.

Ahsanteni.
UDSM ukiondoa salary kuna posho yeyote wanayopewa?
 
Back
Top Bottom