Naomba Ushauri Matumizi Mashine Ya Kufulia

BANGO JEUPE

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2015
Posts
3,079
Reaction score
2,152
Habarini Ndugu
Nyumba Ninayoishi haina miundombinu rafiki ya kutumia washing mashine , ingawa nyumba ina choo ndani na jiko na maji yanaflow ndani

Naomba nijue mashine ipi itakua rafiki kwa matumizi ya familia kwa bajeti Isiyozidi laki 7

Pia nakaribisha mawazo mbadala mmefanyaje wadau
Asante
 
Laki 7 mmmhh? For washing machine, labda ukatafute used ya kufua sijui hata kama utapatapesa

kula chuma hiki , ni brand inayojulikana kwa kutotoa famba,
kama unachukua brand nyingine nzuri iwe front-loader ie: nguo unatupia kwa mbele, siyo juu
nakukumbusha, rahisi aghali
Hiyo inafaa kwa mimi nisiye na chemba ya maji taka
Au ni lazima nijengee system wezeshi
 
Habarini Ndugu
Nyumba Ninayoishi haina miundombinu rafiki ya kutumia washing mashine , ingawa nyumba ina choo ndani na jiko na maji yanaflow ndani

Naomba nijue mashine ipi itakua rafiki kwa matumizi ya familia kwa bajeti Isiyozidi laki 7

Pia nakaribisha mawazo mbadala mmefanyaje wadau
Asante
Nimenunua Hisense huu ni mwezi wa 9, haijawahi nisumbua. Ni Top Load ya 7Kg, inasuuza na kukamua tu, ni nzuri sana. Namna inavyokamua nguo, kukiwa na jua la kutosha ni nusu saa hadi saa 1 tu nguo imekauka, nguo nyepesi unaweza zipiga hata pasi zikakauka vizuri tu, bei ilikuwa 750,000 tu
 
Mkuu, mimi nilinunua aina ya PMC, top loader 8Kg kwa 450,000 tangu Mwaka Jana mwezi wa 9, hadi leo haijawahi kunisumbua. Ina low energy consumption, ina sehem ya kufulia na kukamulia, ni manual. Kwenye kukamua inategemea na mda utakao set. Kwa experience yangu kwa nguo nyepesi inakamua hadi mithili ya kuelekea kuwa dry kabisa. Inafaa kwa matumizi ya familia.

Haiitaji miundombinu ya gharama, Just kuhakikisha pipe ya kutolea maji unaielekeza kwenye channel ya maji taka (kama ni chooni, basi ielekeze kwenye mkondo wa kupokea maji ya kuoga). Kwenye kujaza maji, unaweza ukatumia pipe ya kawaida, au hata kujaza kwa kutumia ndoo.

Kwa ushauri wangu, kama ni kwa ajili ya matumizi ya familia, kwa budget yako unapata mashine nzuri tena yenye guarantee.

Uimara wa hizi mashine unategemea sana na kufuata masharti ya namna nzuri ya kufua na kuhakikisha nguo zako hazina objects ambazo zinaweza kuharibu mashine, mfano coins, kufua nguo kama sox ai leso bila kuziweka kwenye washing bag.
 
Hii itanifaa mkuu
Maji machafu Unatoaje
Umechimbia chemba kwa chini ya kutoa maji
 
PMC hiyo kampuni ya wapi mkuu nasikia za Uturuki na Ulaya ndo uhakika
 
Hapo mmenipa mbawa, sasa ngoja wiki hii Nikawacheki wafanyabiashara wa uhuru
 
Nimenunua Hisense huu ni mwezi wa 9, haijawahi nisumbua. Ni Top Load ya 7Kg, inasuuza na kukamua tu, ni nzuri sana. Namna inavyokamua nguo, kukiwa na jua la kutosha ni nusu saa hadi saa 1 tu nguo imekauka, nguo nyepesi unaweza zipiga hata pasi zikakauka vizuri tu, bei ilikuwa 750,000 tu
Tatizo la top load matumizi ya maji na sabuni ni makubwa sana.
 
Nunuwa Bruhm washing machine manual.

Hii ni wash and spin.(Inafua na kusuuza nguo ila haikaushi)

Kg 7 ni 450000/400000 new.

Brand German.
Ina matumizi madogo ya umeme na maji.

Uzuri wa manual washing machine inahamishika popote unaweza ukafua..
 
Back
Top Bottom