Mmmh!! Huyo ndugu yako ni mtata sana.
Siku zote akiwa Tanzania asiwe mwanamasumbwi hafla anafika marekani amekuwa Boxer!!
Take care, huyo anatafuta pesa ya haraka haraka na hataki kusoma.
Tatizo la Boxing Tanzania kwa ujumla hailipi unless uwe superstar kwelikweli na pia unayumba sana, hivyo sidhani kama huyo ndugu yako anaweza ghafla akawa superstar wa boxing.
Ushauri wangu mwambie huyo ndugu yako afanye kile kilichompeleka Marekani kwanza, hayo ya Boxing yawe extra kwake.
Mwisho, nchi za wenzetu kama USA wanaunga mkono sana michezo katika vyuo na Taasisi, hivyo mtu anaweza akawa anasoma na hapo hapo anaendeleza kipaji chake cha michezo, hivyo huyo ndugu yako ifanye hivyo. Pia ni rahisi sana kufukuzwa USA kama unaamua kufanya kitu tofauti kabisa na kile kilichokupeleka kule.