Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2


Sio kujionea huruma thamini sana familia uliyopewa na Mungu vile viapo tunavyokusemaga wakati wa ndoa huwa vinaandikwa mpk kwa Mungu ndio maana tunapata kichapo tuki geuka kile kiapo. Wapo wanaume waliozeeka vizuri na familia zao wanatunzwa na watoto na wajukuu kwa heshima zote.

Kuna rafiki ya baba yangu yeye ana story kama yako bahati mbaya mke mkubwa alifariki but yeye alimjali sana mke na watoto wa bi mkubwa mbaya zaidi wale watoto wa bi mdogo wote ni wavuta bangi maana alizaa two boys na bi mdogo. Hawa two boys wamekuwa mwiba kwake yaani mpk last month kamwambia baba yangu ktk dhambi ambayo ninetenda hii imeniumiza maisha yangu yote.

Bahati yake watoto wa bi mkubwa wanamtunza sana. Binti yake mmoja yuko huko kwa wazungu mara nyingi huwa anamtumia ticket at least twice a year aende kukaa na wajukuu.

So usiogope watoto wako watakupenda kama uliheshimu mama zao.
 
NILIVOMPATA!

Alikuja mjini DAR akiwa binti mdogo tu na karembo kweli kweli, nikimkuta kwa shemeji yangu mke wa wa rafiki yangu wa kazini.

Baada ya kutoka kazini huyu rafiki yangu aliniambia nimpitishe kwako kuna kitu anachukua halafu tuendelee na mishe zetu, mimi nilikuwa na kagari kangu yeye hana, na mara nyingi alikuwa anapenda kunitumia mimi, na Vibia nikawa navipata vya bure, sasa baada ya kufika kwake shemeji akawa katoka na funguo, ikabidi tumsubiri kwa muda, alipofika hata plan yetu ya kutoka tena ikawa imeishia hapo.

Lakini alikuja na hako kabinti, sasa kukaa tena nyumbani rafiki yangu akaona hapana, akatukaribisha wote kwenye glocery ya karibu na nyumbani, tukanywa pale binti alikuwa hanywi baadaye naye akaanza kidogo kidogo, muda ukaenda na miadi ikaianzia hapo.

Amesoma kiasi, siku hiyo sikuuliza, kaja Dar kufanya nini, nikapewa jibu.

Basi weekend iliyofuata tukakutana na kuelewana zaidi kwenye bar fulani hivi. Na mahusiano yakaanzia hapo!

Mara nikasikia kakorofishana na yule shemeji yangu, na kaamua kupanga chumba chake maeneo ya huko uswahilini. Akanikaribisha, nikamuuliza utawezaje kuishi mwenyewe binti mdogo hivi? Akasema atajua.

Basi nikaona mara akajiunga na wadada fulani hivi kwenda viwanja kufanya vibarua.

Kipindi ameshajua nafanya kazi wapi, sasa kila baada ya siku mbili au tatu nikawa namtembelea kwake, lakini mazingira ya pale kwake yalikuwa hayanifurahishi, kwa sababu kwanza nilimkuta analala chini kwenye mkeka na kagodoro kikuu kuu hivi na jiko la mchina na madumu dumu ya maji.

Kwa kifupi ni kisera sana, sasa kusema kweli niliingiwa na huruma tu, nikamnunulia baadhi ya fanicha, kwa sababu nilimwona kabisa huyu ndio kaamua kuja Dar.

Nilipojitahidi kujiondoa kwenye huo uhusiano kwa kumweleza nina mke, hakutaka kunielewa, nikizidisha siku bila kwenda kumwona nashtukia kaja ofisini. Nikaendelea kununua vitu vyake vya matumizi mpaka chumba kikajaa. Sasa na mimi mdogo mdogo nikawa najisahau nalala kule, lakini mara ya kwanza kabisa kulala kwake alinichezea mchezo, tulipotoka kupata kinywaji nikapitia kwake kidogo, sasa ule uchovu mara kausingizi kakanipitia, hakuniamsha ng’oo kwamba niende nyumbani, kaja kuniamsha karibia kunakucha niende kazini!

Ndio kwa mara ya kwanza nikawa nimelala nje! Nilimwelezaje mke wangu, hiyo ni story ninyingine tuiache.

Sasa mwaka umepita nimenogewa mtoto wa watu ana ujauzito wangu.

Mungu wangu sasa mimi nifanyeje, mume wa mtu tena wa ndoa. Kusema ukweli nilichanganyikiwa, lakini hata hivyo nilikuwa nategemea nini?

Basi baada ya muda akaenda kwao kujifungua na akajifungua salama, nikaenda kumtembelea na kuona wazee. Na nilienda kwa gari langu na rafiki mwingine. Tukalala pale asubuhi nikaona tunachinjiwa mbuzi. Tukala na majirani na ndugu kama 16 hivi walikuwepo, kusema kweli sasa dalili zote kwamba mimi ni mkwe tena wa heshima niliziona pale, ilipofika jioni tukaondoka kwenda kulala mjini yeye bado tukamwacha pale na mtoto wake
 

Mimi pia Kuna ndugu yangu ujanani amemsumbua sana mkewe,ametoka mpaka na shemeji yake yani mdogo wa mkewe na wakazaa mambo mengi sana watoto wa nje usiseme,mke alikuwa anavumilia tu.

Picha likaanza baada ya watoto kuanza kufanikiwa,wa kwanza kamsaidia wa pili mpaka wa mwisho wote wameenda marekani,huku bongo wamemuacha kaka yao mmoja ambae ni mwizi miaka yote,wamemvuta na mama yao now full bata.

Mzee yupo huku peke yake afya yake sio nzuri kwakweli anaelekea 90 hivi hana wa kumuuguza mke anasema amekwama kurudi huku sababu ya corona mwaka unaelekea wa tatu huu[emoji28][emoji28][emoji28].

Yule mzee amebaki mkiwa kama vile hana watoto au mke na ni mtu pamoja na mabaya yake lakini alikuwa very responsible father
Mifano ni mingi kiufupi mwishoni mwanamke nguvu yake huwa ni watoto basii
 
Mzee umesema ukistaafu una Kama 250m? Naomba nikufariji pindi utakapostaafu umehangaika Sana na majukum ya hapa na pale unahitaji kutulia Sasa na kula mema ya nchi...mi sihitaji kuzaa ucjal

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]aah jamani muwe na huruma atii utamuongezea stress mzee wa watu muache tu kwa sasa atulie ajilie pesa yake na bi mkubwa
 
Baada ya muda akarudi Dar, sasa kile chumba tena ni kidogo na hakina hadhi, nikampangia chumba kikubwa zaidi,
Nilisahau, baada ya kuona ile kazi anayofanya haina future nilimtafutia chuo, lakini baada ya kumuliza anapendelea kupata ujuzi gani? Akasema unesi, lakini sifa hazikumruhusu, akata usecretary, vilevile sifa hazikumruhusu, wakati nimeenda kule kwao niliona kama kile kijiji kuna kama kashughuli fulani ambako kila ukikutana na msichana au hata mdada yupo Bize anfuma,

Ndio nikamwambia akienda chuo cha ushonaji sio mbaya, nikampeleka kwenye chuo fulani kule mikocheni, sijui kama bado kipo huu ni mwaka wa 20 sasa.

Kusema kweli baada ya miezi michache alikuwa ni fundi mzuri sana. Hasa hasa kudarizi, nikamnunulia cherehanii ya kudarizi akawa sasa yupo nyumbani anafanya kazi hiyo huku abamwangalia mtoto, mala sasa kwenda kutembeza mitaani na kukopesha na kufuatilia nadeni, kazi ikawa ngumu ikabidi aagize msichana wa kazi, sasa kawa mama mwenye kuleweka na maisha yake, mala mtoto wa pili

Sasa matibabuna kutambulika ofisini nikapiga moyo konde ofisini wakatambulika kama watoto wengine wangu, na wakapewa bima ya afya, tena ya hadhi ya juu, wakati nadhani ilikuwa una thamani ya million 15 kwa mtoto mmoja, Ila mama hapana, Nakumbuka hata watoto wa mwisho wa bi mdoga na bi mkubwa walizaliwa siku moja, ila jinsi a tofauti mmoja agakhan mkoanii na wa bi mkubwa hapa Dar.

Sasa ndio kawa Mke , na watoto ndio hao, haraka haraka nikaanza kutafuta kiwanja, Bahati nzuri ni msomaji mzuri wa magazeti nikaoona viwanja vya serikali vinauzwa huko,

Wakati watu wengine wamelala, mimi nikapata viwili. Ikabaki kufuatilia hati, na kwa sababu ulikuwa ni mradi wa kimkakati, hati zilitoka mapema tu, lakini kwa jina langu mimi.

Baada ya muda kidogo mdogo wake wa kike naye akuja, baadaye tena akaja binamu yake wa kike,mala ndugu mwingine,

Lakini pale ilikuwa kama njia tu ya kupitia, ila pakaheshimika kama kwa dada mkubwa,

Mala akaongezea vibiasharavingine hapo nyumbani kama ice cream, maji, ubuyu, wakati ni mwingine anabeba mwenyewe mpaka shule,

Kwenda kuuza, kusema kweli nilikuwa najionea maajabu tu, ila alikuwa analipa, !!! Mpaka sasa nikawa naanza kuona wivu, sitaki kukaribuwa karibiwa na watu ovyo ovyo au matani ya kijinga na watu wa mtaani pale,

Nikisema sasa nilianza kumpenda kwa dhati sio siri, yaani nilikuwa na wivu hatari,!!!!
 
Biashara hizo hizo nikaanza kuona kuona kama zinamshushia hadhi na kusema kweli sikuona kama zinalipa sana, nikamwambia aache ndio akaanza na glocery ambayo aliichagua mwenyewe baada yakuona jirani yetu kama anaingiza sana, lakini wanasema utamu wa ngoma ingia ucheze, kusema haikulipa na ilikuwa ni ya kisasa hasa,

Tukabadilimfumo sasa tukaingia kwenye dala dala, hiyo ndio kabisa bure kabisa, ufuatiaji ulikuwa mgumu hasa,ilikuwa ni hiace (punk)

Kule kwa bi mkubwa mpaka nampata huyu bi mdogo tayari nilikuwa na nyumba yangu maeneo ya kama km 5 kutoka mjini kati,
Na ni nyumba ndogo ya cyumba vitatu na jiko choo cha common na dining room, ambapo bi mkubwa alikuwa na wadogo zangu watano wakisomea hapo kwangu, kwanza wawili kuamzia darasa la tano mpaka kidato cha nne hapahapa dar, baadaye wawili tena, la nne mpaka kidato cha tano mkoanihuko, na wote sec za kulipia, wakifika hapo hawaendelei naona wanakuwa wahuni napiga xhini wanaondoka, mala mtoto wa kaka yangu mana yake alifariki akiwa hata chekechea hajaanza , naye amesoma hapo kwangu mpaka amemaliza chuo miaka mitatu iliyopita,

Baadaye tenna msichana wa kaka, darasa la nne mpaka form , baadaye certifiate na diploma kamalizia mwaka juzi, ila Hana kazi,

Kaenda kuhangaika huko.

Sasa miaka kama mitano kabla sijampata bi ndogo nilinunua eka 2 nje ya mji kama 25 km
Hivi na 1.5 km toka bara bara kuu, kipindi hicho huoni nyunba karibu, na dala dala a
Zinaishia kama km sita hivi mpaka hapo shambani(enzi hizo)

Nilipanunua kwa sh 300000 tena kwa kulipa kidogo kidogo,
Nikawa nimeanza nyumba ndogo kwanza kwanza baadaye nikaona upuuzi nikaanza mdogo mdogo nyumba kubwa hmkabisa, ambayo kusema mpaka sasa hivi ndimo naishi,
Na ni kubwa hasa maana nilijenga kama kanisa, vyumba vinne ikiwemo master na sebure yake,

Mpaka sasa toka nimeamia ni mwaka wa 8,
Na nilitumia miaka 6 kuijenga, mpaka nahamia hakuna tiles wala gypsum, tumehamia hivi hivo baada ya kuweka umeme,
Kilichochrewesha ni kwa sababu tayari nilikuwa na nyumba mjini, ambayo nakula 280000 kwa mwezi, na pesa hiyo anachukua bi mkubwa wala hata sijawahi kuigusa na toka nimehama huko sijawahi kwenda, huu mwaka 8,

Sababu nyingine ya kuchelewa ni ujenzi wa nyumba ya bi mdogo,

Nimezungumza kidogo mambo ta bi mkubwa hapo kutokana na junbe za kunishambulia, mala jarma ya bi mkubwa hiyo, mala nilimsahau? Hapana yupo poa tu,
 
Mimi pia Kuna ndugu yangu ujanani amemsumbua sana mkewe,ametoka mpaka na shemeji yake yani mdogo wa mkewe na wakazaa mambo mengi sana watoto wa nje usiseme,mke alikuwa anavumilia tu...
Sawa kabisa, mifani ni mingi, wanaume tutimize majukumu kama baba wa familia, lakini tuangalie na future yetu sisi wenyewe, tusijisahau kwa kutegemea kuangaliwa na watoto,
Wazungu hilo waliliona muda mwingi tu.
 
Tunyime tu usingizi.
Hahaa, ndugu yangu, utaendelea asubuhi, mimi nilivyo sasa najiona kama sio mtu,
Sina usingizi, sili, hata nilvyosema naenda kula wala sikula chakula chenyewe kiliungua,

Hawa wanawake hawa we acha tu, Mungu atawageuzia kibao tu, yaani mimi ni mtu wa kukesha kabisa, hata kula sili, kwa shida gani hasa yarabi,?

Haya ngoja nikaoge nijiandae kwenda kazini, labda nitasinzia huko.
 
Da ngoja nikaoge ndugu, angalau ni Ali na kibarua changu, nisije nikakosa vyote,

Baadaye kabisa, nitaenda nilipoishia au nilivyomuhamisha bi mdogo kwenye nyumba yake.
 
Da ngoja nikaoge ndugu, angalau ni Ali na kibarua changu, nisije nikakosa vyote,

Baadaye kabisa, nitaenda nilipoishia au nilivyomwamisha bi mdogo kwenye nyumba yake.

Baba ungetusaidia tu muendelezo baada ya kuuza nyumba na bi mdogo kutaka ashike pesa mpaka hapa ulipofikia imekuaje
 
Ahsante sana,
Ndio lengo langu kumpata mtu wa kunishauri zaidi, maana naona tulipofikia sasa ni kutafutwa nifanyiwe kitu mbaya
Mzee samaki hukunjwa angali m'bichi!
Hapo ulipo hu kunjiki tena!
Amini hivyo maisha ni masaa na kumbuka masaa hayarudi nyuma, muhimu sana kumbuka hivyo na mabaharia wote wajuwe hivyo!
Tafakari maana ya mchepuko?
Njia yenye kona kona nyingi na vi Chepuko vingi Muda wowote unaweza potea kwenye njia hiyo!
Barabara kuu kukiwa na foleni madereva wote watapita huko kwa mchepuko!

Eti tunajidanganya ndugu zake wananijua ndio wanakujua kuwa una mke na watoto na yeye ni mchepuko!
Na wanajua pia wapo wengine kwa ngazi tofauti tofauti!
Ushauri number moja corona ipo jikinge kwanza!
Number 2..
 
Hakika Mi nakuelewa Sana ujue ingawa wengine hawatokuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
What?!! Pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ulianza vizuri, sasa hapa unaleta ubinafsi. Ulifanya makosa wewe mwenyewe kwa kujibebesha mizigo, somesha uwezavyo tunza familia yako angalia future yako na familia yako kwa ujumla. Nina imani kati ya hao wanao kuna aliyekuwa/waliokuwa na wasiwasi na mwenendo wako, sema tu ndo hivyo mtu mzima hakaripiwi na mtoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…