Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Sasa baada ya kupokea lile fungu la kwanza
30m, mimi haraka sana nikaenda kupunguza madeni yangu, hata hivyo Hays kwisha,

Na yeye nikamwita kwamba tukae chini ili ile 15m yake tuipangie matumizi ya kwanza kabisa,

Ushauri wangu ilikuwa tununue kiwanja kwanza,

Sehemu ambayo sio ghari sana, Hapo sasa ndio kimbembe kilipoanza,

Ila kufupisha story nilimwambia basi wewe unataka tuanze na nini? Akanijibu hiyo pesa anataka afanyie biashara wakati ujenzi unaendelea, nikamwambia biashara mbona tumefanya na tunasnguka, hata hivvyo sio mbaya wewe kutaka kufanya biashara lakini ni bora tuwe na kiwanja kwanza.

Kusema kweli zogo lilikuwa kubwa ananipayukia na mimi natumia ubaba wangu sasa kulazimisha, ndio alipoamka kwenye kiti(tulikuwa tumekaa nje na watoto wanacheza hapo nje).

Alichoniambiakwa sauti kuu na kali ni kwamba

TOKA HAPA NA VISENTI VYAKO UNAVYONIPAGA,

Du ! Leo naambiwa visenti, yaani huyu mwanamke nimekopa pesa, nimempeleka ufundi cherehani, nimemfungulia saloon , grocer, mghahawa, dala dala, mtaji wa kuku wa kisasa.

Anaanguka namyanyua, anakopa vicoba anashindwa kumaliza nammalzia,

Nalipa watoto karo kwa mwaka jaribia Mil 6 na bado watoto ndio kwanza wanasafari, kwa nini ananivunjia heshima namna hii?

Kusema kweli sikujua kama niliokota jiwe au mti au ufagio, nimpige nao akawahi kukimbia, na mimi nikaanza kumfukuza, kama sijamrushia kila kitu ambacho mpaka leo sikijui, nikaanguka chini, yeye akaendelea sijui wapi , kusema kweli sikumwona,
Kuangalia nyuma naona watoto, kumbe na wenyewe wakawa wameshika mawe wanataka kunipigia nayo, nikaamka ili niwafukuze nikaenda chini tena , sasa hapo ndio nikaanza kusikia maumivu, na watoto wale kule wamesimama, sasa na wenyewe wanapaza sauti,
KWA NINI UNAMPIGA MAMA YETU SI UENDE KWENU!!!!!

Nitaendelea

Alooo, kabla hujamaliza kuhafithia kisa chako ila ww ni ndezi! (Samahani sana kwa ukali wa maneno ila nimelazimika) ww ni ndezi mkuu au ulirogwa?

Nisomeshe watoto, nikujengee, nikufanyie yote hayo alafu unitamkie hivyo. Na watoto wanashabikia si uende kwenu, (hivi hao watoto ni wako, ulipima DNA?)

Ningekua mimi ndio wewe huyo mwanamke ningempasua ubongo, na hao watoto ningewachinja kama kuku [emoji3545][emoji3545][emoji3545][emoji1421]
 
Tatizo lako lilianza ulipokua kijana ulijifanya umeokoka sanaa, ukaja kujulia mbunye ukubwani, ikiwa alikupa dawa hapo ni sawa ila vinginevyo ulikua na unazeeka bado mshambaa wa mapenzi, na limbukeni wa wanawake... ww kenge mmoja akusumbue maisha yako yote haushtuki???msijifanyege walokole wakuu, k za ukubwani ndio shida zake hizo,
 
Eish nimeanza story toka mwanzo


Yani kwa akili hata ya mtoto wa chekechea wewe ungeona dalili zile za kwanza kutoka kwa bi mdogo ungebaki na plan ya kumuwekea mil 30 za awamu ya pili tena kwake si angebadili aweke account yake mpaka abaini ukweli

Hatupo hapa kumpigia makofi huyu baba kuna sehemu alikosea na sisi tunatoa tu maoni kama ingekuwa mimi ningefanyaje we endelea tu kusoma hii story sisi wa kudandia hatuachi tupo hapa mpaka iishe na sehemu nikiona sio ntaweka comment sipangiwi [emoji6]
Hapana Maya, sometimes lazima ubinadamu uchukue nafasi regardless ya mapungufu ya bi mdogo. Ile nyumba na kiwanja kilichouzwa ilikuwa ni kwa ajili ya bi mdogo. Kumnyang'anya hela bi mdogo inayotokana na nyumba yake na wanae sio ubinadamu. Jamaa alikuwa anajaribu kuwa muungwana kuendelea kuyaheshimu makubaliano ya mwanzo kwa sababu nature ya hiyo hela ni ya bi mdogo. Yeye kama baba alikuwa anahakikisha anatoa mwongozo wa matumizi sahihi ya hiyo hela.
 
Semeni nyie tukisema sisi mnasema tunamuonea
Hivi unawezaje kumpa tena 30m jamaniiii mbona nimetamani kutoa chozi
Huyu baba alikuwa under madawa sio kawaida[emoji19][emoji19]
Iko tatizo mahali aisee duh
 
Sure kwa wanaume strictly woooi hutoboi walah tena hili swala angelifikisha kwa ukoo wanaume wangemsaidia shaona kwetu tena bila kuathiri nyumba kubwa

Kweli kabisa.
 
Amesema "Ila tatizo lingine kubwa ni nalo liona nyinyi wanawake mna chuki na husuda kwa wenzenu wenye maisha mazuri, na hayo maneno yenu ndio chanson cha kuwaingiza chaka na kuharibu kabisa maisha yao" ambapo kwa asilimia kubwa ni kweli.

Sababu iliyopelekea bi mdogo akaishia kwa mtoa mada ni baada ya kubeba ujauzito na kuzaa mtoto wa kwanza. Unamshauri bora angemchuna halafu atafute mwanaume mwingine.

Sio kila mtu anaona ni vizuri watoto wake kuwa na baba tofauti tofauti hiyo ni moja.
Mbili, sio kwamba mtoa mada alikuwa hamlei vizuri, mtu kamchukulia kama mke wake halali kamjengea nyumba , watoto wamesoma, watoto wana pata haki zao zote za msingi halafu unamuona huyo mwanamke ni mjinga? Bora angemchuna huyu mwanaume wakaolewe akiwa tayari ana mtoto?

Ni wanawake wangapi wamezaa na wanaume za watu na wametelekezwa wanalea watoto wao wenyewe?

Ni wanawake wangapi wapo kwenye ndoa lakini waume zao hawalei watoto wao kwa mapenzi?

Kwanini huyo Dada afanye unyama wa kumchuna mtoa mada na kukimbia? Una uhakika gani huko ambapo angekimbilia angeenda kupata furaha zaidi ya anayoipata kwa mtoa mada?

Tena na vile angekuwa single mother angeteseka sana na kutamani kurudi kwa mtoa mada. Ushauri ambao ungemshauri huyo bi mdogo ungemwangamiza. Ni ushauri mbaya.
Ahsante sana, ndugu.
 
Hapana Maya, sometimes lazima ubinadamu uchukue nafasi regardless ya mapungufu ya bi mdogo. Ile nyumba na kiwanja kilichouzwa ilikuwa ni kwa ajili ya bi mdogo. Kumnyang'anya hela bi mdogo inayotokana na nyumba yake na wanae sio ubinadamu. Jamaa alikuwa anajaribu kuwa muungwana kuendelea kuyaheshimu makubaliano ya mwanzo kwa sababu nature ya hiyo hela ni ya bi mdogo. Yeye kama baba alikuwa anahakikisha anatoa mwongozo wa matumizi sahihi ya hiyo hela.

Hapana huyu mwanamke alishaanza kuonyesha ni mshenzi tu
Mimi kwakweli hio roho ya huruma huwa sina haswa mtu akitanguliza ujinga siwezi kumsamehe mtu anae nikanyaga makusudi akitarajia akiniomba msamaha nimuelewe ndio situation kama ya huyu baba
Pale pale alipoanza kununua magodoro ndio ingekuwa mwisho wake
Kuna wanawake wanatamani mwanaume Kama huyu yeye analeta ujinga
 
Sure kwa wanaume strictly woooi hutoboi walah tena hili swala angelifikisha kwa ukoo wanaume wangemsaidia shaona kwetu tena bila kuathiri nyumba kubwa
Kafeli sanaa, tena pakubwaaa
 
Wenyewe wanaume watakwambia ni nguvu ya papuchi ujinga tu

Ujinga ujinga tu
Mwanaume anae hangaika na michepuko akitulia akajenga na mkewe anakuwa mbali zaidi nguvu anayo igawa huku na huku
Huyu mzee angewekeza kwa familia yake angekuwa zaidi ya hapa alipo now naamini
Kwanza mchepuko kapewa mtaji zaidi ya mara mbili kafeli aisee aaargh
 
Back
Top Bottom