miss pablo
JF-Expert Member
- Jul 9, 2018
- 5,411
- 11,025
Bado halioni hilo. Maana hakua na backup yoyote ile. Ambayo ingekuja ndo hiyo2 ingecover up kila kituAliona kuna fursa akachangamkia
Binamu nakusalimu katika Jina la BWANA.Samahani km ntakwaza watu lakini mi naupenda uislamu wangu uliohalalisha wake wanne. Kwa kweli toka dunia ianze wanaume hawajawahi kutosha huyo Dada Leo miaka 20 na zaidi anaishia kuitwa mchepuko wakati angekua muislam angemuoa.
Kingine mbona wakurya wana mitala nnao huku kanda maalum yaani mitala kama zote .
Huyo demu nae kimeo 20yrs unakubali kufichwa km Arv vile...!!! Au ndo tamaa ya pesa mweee!pole yake aseh
Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo nyumba mwachie yeye na watoto. Mkatie eneo kiasi la kiwanja cha kwenye nyumba, eneo linalobaki weka fensi kisha kaendelee na maisha yako mengine.Kuhusu mimi nimeshaamua huyu mwanamke simtaki lakini wasiwasi wangu ni hii nyumba?
Niifanyeje
Mambo ya polisi na ustawi wa jamii nataka kuyaepuka mapema sana,
Ingawa binafsi ningejua hatma ya nyumba,
Ingependeza kama ningeimalzia vizuri,
Niongeze vyumba kama 15 vya wapangaji, ili niipige bei nzuri
Uhakika baada ya hapo hapo 300 m
Nitakunja
Wa kiislamu mbona wameruhusiwa lakini nao ndio wale wale tu?[emoji2369][emoji2369][emoji2369][emoji2369][emoji2369]Mama weweeee....mjini hapatakalikaa utashangaa mke mkubwa analetewa wake wanne na watoto wawili kila mmoja yaani![emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji3][emoji16][emoji16]!!!Wanaume wa kikristoo wana watoto njee!na wanachepukaa haswaaa na wanaoa siku Hizi wake wawili wawili mpk watatu!hyo sheria wanatamaani iondolewe
Sent using Jamii Forums mobile app
Fukuza pumbavu huyu , wewe ni mwanaume Nasema FUKUZAHuyu mwanamke simtaki tena, lakini naona kama anawapambe,
Nipeni ushauri wapendwa,
Maana ninachokiona siku moja huyu mwanamke anaweza rudimentary hapa kwa gia ya watoto
27- namwomba yule rafiki ajaribu amwambie nina maongezi naye lakini, anajibu sisi tumekuja kwa shughuli ya mtoto, nikamwomba basi naomba niongee na wewe,
Akasema lakini nikupe simu ya mzee ili alinipe ruhusu ya kuongea na wewe,
Yule rafiki yangu alinivuta shati kwa ghafla bila kutegemea,
Akaniambia tuondoke, ‘kumbe mwanamke mwenyewe ndio huyu, mbona yupo,(primitive sana) mmm yaani mke wangu Primitive, aliishia tu kuniambia yule sio mwanamke wa kunisumbua mimi, yaani sio hadhi yangu kabisa, kwamba ana mwonekano wa kishamba hasa, acha tabia yake.
Mkuu uza nyumba endelea na mishe zakoHuyu mwanamke simtaki tena, lakini naona kama anawapambe,
Nipeni ushauri wapendwa,
Maana ninachokiona siku moja huyu mwanamke anaweza rudimentary hapa kwa gia ya watoto
Very true. Yaan najua kabisa fulani anaye mtu wake ambaye anajulikana officially halafu eti aseme na yeye ni first priority.Nimevumilia kutocomment ila nimeshindwa kwa hii comment yako. Wewe una uzoefu hakika. Hakuna mwanamke anayerisk maisha yake asilani. Mwanamke yeyote anaishi na mwanaume kama anajua kuna faida iwe leo au kesho (future). Mawanamke projector (projection) mzuri ingawa anaweza kuwa estimator (estimates) mbaya.
Kwa kutambua wanawake walivyo, nilikataa kuoa binti nikaoa aliyemuita bibi kizee kwa vile tulipishana miaka 20.
Demu wenyewe kimeo huyo umeona eeh!Mme wa MTU anakuheshimisha analeta us....e!!Lofa sana.Nafikiri waganga wake sasa wameisha nguvu ndo maana baba anajitambua Mme wa MTU anakupa hadhi yooote hyooo!mfyuu zake huyo mama NHapana huyu mwanamke alishaanza kuonyesha ni mshenzi tu
Mimi kwakweli hio roho ya huruma huwa sina haswa mtu akitanguliza ujinga siwezi kumsamehe mtu anae nikanyaga makusudi akitarajia akiniomba msamaha nimuelewe ndio situation kama ya huyu baba
Pale pale alipoanza kununua magodoro ndio ingekuwa mwisho wake
Kuna wanawake wanatamani mwanaume Kama huyu yeye analeta ujinga
Jan mwanzoni wanarudi tena naamua ngoja tu wakae,
32-Jan hiyohiyo wote wanarudi shuleni kwao
33- January nasikia amerudi analadhimisha apewe funguo, akakataliwa mpaka mimi niwaambie kwa mdomo wangu hao majirani zangu akagombagomba hapo mwishoe aondoke
34 - kesho yake mchungaji akaniita na mke wangu kuomba arudi ndani,
35,-baada ya mazungumzo marefu, anatamkia mchumgaji hii nyumba ni yake, mimi nilishachukua fungu langu, yaani ile mil 15
Hiyo ni family yako. Huhitaji kumuonea aibu bi mkubwa. Mueleze ukweli.Ushauri wenu ni muhimu sana.
Umri wangu ni miaka 50, nimeoa mke kanisani huu ni mwaka wa 25 naishi naye na tumejaliwa watoto wanne, wa kwanza na wapili wamemaliza tayari chuo kikuu na wa tatu yupo chuo kikuu mwaka wa pili. Wa nne kamaliza kidato cha 4 mwaka jana, katikati hapo miaka 18 iliyopita bahati mbaya nikajiingiza kwenye mahusiano na binti wa miaka 20 wakati huo na akapata ujauzito, nilipomwambia nimeoa ili aitoe mimba ile na kwa kuwa bado ni binti mdogo anaweza kupata wa kumwoa, alikataa katakata. Na mimi kwa kuogopa maana alinitamkia kuwa atajiua kama nitamlazimisha kutoa mimba na kuwa yupo tayari kuishi na mimi kama mke wa pili na ujauzito ule hawezi kutoa kamwe.
Niliendelea kumshawishi atoe, matokeo yake akakimbia akaenda kwao mpaka akajifungua huko.
Lakini kiufupi zaidi, alirudi tena na kunitafuta na kunitishia kumwambia mke wangu, hivi ninavyoandika ilibidi nirudishe nyuma majeshi na kuanza kuishi naye kama mke wa pili.
Nilimpangishia chumba na maisha yakaendelea, baada ya muda alipata mtoto wa pili, wote ni wa kike, baada ya muda nilianza kuwasomesha kuanzia chekechea mpaka sasa hivi wa kwanza anafanya mtihani wa form Six mwaka huu na wa pili anafanya wa form 4 mwaka huu na wote wamesoma shule za Private toka chekechea mpaka sasa hivi na kwa wastani kila mmoja alikuwa ananigharibu 2.5m hasa shule za msingi mpaka secondary. Hapo bado michango mbalimbali na usafiri, kwa maana walikuwa wanasoma mikoani.
Baada ya kumpata mtoto wa kwanza akiwa kwenye chumba cha kupanga, niliona sina budi watoto wangu na mimi binafsi niwe na uhuru maana maisha ndio yalishaanza hivyo, na mimi upendo tayari ulishaingia na kuona ni maisha kama maisha mengine.
Ndipo nilipoamua kununua viwanja, kama unakumbuka miaka ile ya 2000 nadhani kuanzia 2006 serikali ilipima viwanja 20,000 maeneo mbalimbali ya DSM, mimi nilichukua viwanja viwili, wakati ule nakumbuka kimoja nilinua 1,800,000 na kingine 1,300,000 ml. Ukubwa ni sq m 1200 na 1000. Kimoja kikubwa nikamjengea nyumba ya mgongo wa tembo, vyumba 2 na sebule katikati na choo kizuri cha nje, nikaacha eneo kubwa tu kwa ajili ya kujipanga na kujenga nyumba kubwa baadaye, kumbuka huo ni mwaka 2007 alipohamia hapo au tulipohamia hapo.
Baadaye nimfungulia biashara ya saloon, akafanya kama miaka 2 vibaka wakaingia nakuiba kila kiatu, nikaona isiwe shida nikamfungulia mghahawa ambao ulikuwa na vitu 16 na meza nne kubwa, bado na wenyewe haukufanya kazi vizuri, nikamfungulia grocery ya bia na kuweka kila aina ya kinywaji kwa kutumia viti na meza za mghahawa.
Nayo haikufanya kazi vizuri, nikamnunulia Hiace iliyotumika tayari kama dala dala.
Na yenyewe usimamizi ukawa mgumu.
DA NITAENDELEA, MAANA DA SIPO VIZURI KABISA KIAKILI NI NIMECHANGANYIKIWA SASA HIVI.
SEHEMU YA 2
MUENDELEZO WA TUKIO HILI SOMA HAPA CHINI:
SEHEMU YA 3
SEHEMU YA 4
SEHEMU YA 5
SEHEMU YA 6
SEHEMU YA 7
SEHEMU YA 8
SEHEMU YA 9
SEHEMU YA 10
SEHEMU YA 11
SEHEMU YA 12
SEHEMU YA 13
SEHEMU YA 14
SEHEMU YA 15
SEHEMU YA 16
SEHEMU YA 17
SEHEMU YA 18
SEHEMU YA 19
SEHEMU YA 20
SEHEMU YA 21
Amen[emoji120][emoji120][emoji120]Binamu nakusalimu katika Jina la BWANA.
Uislam ni mzuri kuhusu issue ya wake wanne; kwa wanaume ambao hawajaamua kuridhika; na kwa wanawake ambao wanaenda kuolewa mke wa 2, 3 au 4. Ila kwa mke wa kwanza, suala la wanawake wanne kwake laweza kuwa shubiri;au kwa mke wa 2 na 3 pale anapoongezewa mke mdogo na yeye ndiyo utajua sasa kama wanafurahia kuongezewa wake wenzao.
The bitter truth; mtu asipoamua kuridhika hakuna idadi ya wanawake itakayomridhisha. Kwa sababu kuoa wake wanne haimaanishi ndiyo kwamba wakifika wanne tu na tamaa ya mwanaume inakufa. Ataendelea kutamani, na since hawezi kuoa mke wa 5,6..... basi atawafanya michepuko.
Na huo uke wenza uliohalalishwa; kwa kweli hekaheka zake tunaziona humu mtaani na duniani(especially insta). Hata wanawake tumeumbwa na ubinafsi, kilicho changu sitopenda kushare na mwingine period. Majority wanaolewa wake wenza kwa sababu tu ndiyo dini inataka hivyo na hawana option; lakini hawapendi. Ila most likely kadri unavyoongeza idadi ya wanawake, ndivyo unavyoongeza stress. Mara nyingi kila mwanamke atavutia upande wake na watoto wake ili wapendelewe zaidi wao. Na unaweza kuwatreat wake wote sawa; ila huwezi kuwapenda the same kuna sehemu tu upendo utazidi. Muda sio muda mabifu yanaanza, mara kukamatana uchawi n.k.. kwa zile hekaheka za wake wa mzee Yusuph au Queen Darleen na Sabra; kwa kweli naushukuru Ukristo. Na wanawake wanapeleka chuki zao hadi kwa watoto wa mke/wake wengine; watoto wengi wa kutoka kwenye familia za mitala hawapendani kwa sababu ya sumu wanazolishwa na mama zao.
Binadamu haturidhiki kwa sababu kiuhalisia kila siku kuna matamanio mapya; ni vile inafika hatua unasema na kuamua ngoja tu niridhike. Ni sawa tu na idadi ya partners; usipoamua kuridhika utaoa na kuacha kila siku. Usipojua/jifunza kuutiisha mwili wako; hakuna idadi ya wanawake itakayokutosheleza. Na kwa familia zetu hizo za uchumi wa kuvumiliana: wanawake wengi=umasikini
Na kwa shuhuda chache tu za watu walizozileta humu kuhusu ndugu zao waliokuwa na wake wengi; unaona kabisa jinsi fainali uzeeni inavyo-apply kwa wanaume. Mpende na kumuheshimu mke wa ujana wako.