Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Pole kaka kwa masumbuko kwa mwanamke asiyekuwa na utu wala fadhila.Anataka nyumba iuzwe tafuta mteja aje kuinunua kwa pesa ulizompa wewe ili mgawane yeye aondoke uchukue nyumba yako.Tafuta mteja wa bei rahisi umpe nusu ya total amount ambayo itakuwa half the real amount.

Kwa mfano tafuta mteja wa 45 million usrme inalipwa installment 4,kumbe unatoa wewe pesa zake 22.5 m kwa instalment mbili akuondokee.Achana na kumfuatilia anaenda wapi anarudi lini,acha kujua nyendo zake.

Wewe ni MTU mzuri na strong you can survive this.pia watoto usiwatupe hawajui wanachofany kwa sababu ya mama yao.Walipie ada kama unaweza,hilo ni jukumu lako.kama unaona huwezi wahamishie kayumba wajue mama yao hana msaada kwao.
LA mwisho kaka ukishanunua nyumba iache kwa muda usikae hapo imalizie kidogokidogo.

Muda mwingi kaa na shemeji mkubwa ila uwe unaweka vikao vya familia na watoto uwaambie mapungufu yao yote ya kukutumia 120,000/ kwa miaka yote.Mwambie shemeji mkubwa aongee na watoto wajue wewe ni baba yao na umehangaikia hapo walipo.Mwisho kwa utaratibu na upole ukiona nyumban pametulia mueleze shemeji mkubwa kuhusu hao watoto wengine maana,shemeji mdogo akipigwa na maisha atataka kurudi aje akuharibie maisha nyumbani.

Hadi ulipofikia una mapungufu ya kibinadamu,.Amini kaka Mwitore humu muna watu wanamajanga wakiyasema utaona wewe huna shida.

Kuwa makin na single mother's ambao ni opportunist's watakufuata inbox ambao ni wafuatao:
1 Shunie..
2 Espy.
3 Carha.
4 Witness J
5 Mandenyi.
Maya Angelou ni mja mzito msamehe ni hiyo hali yake
 
Baba uza hiyo nyumba urudi kwa mke mkubwa,kama mke mkubwa hafahamu huu upande wa pili wa maisha yako rudi kwake.utulie tulii,usisubiri umwagiwe maji ya moto ndio mke mkubwa ayajue haya ukiwa hospitali.pia naona kuna kifo cha mmoja wenu kikisababishwa na haya mapenzi.

Unapompiga mara kwa mara kuna siku inaweza kutokea ajali ukaua,au yeye kuna siku anaweza kujihami kwa kitu kibaya akakumaliza.

Jitihada zako kwa huyo mke mdogo naona ni sifuri.
 
Dah wewe umesema umezaa hovyo why kunimalizia stress?
Huu Uzi wanaume wenye makando mna hasira
Hata hasira ninazo basi mamiloo...

Huwa makasiriko yako kwenye nyuzi za watu huwa ni makubwa....
Au kuna shida kisaikolojia????
 
Haufi bwana ila utavumilia tu
Kufa sifi Ila Cha Moto nitakiona ... Wajua sisi wengine hata kudumu ktka mahusiano huwa hatuwezi kwa sababu ya kuepuka kuumia [emoji16][emoji16][emoji16]

Imagine hata huyu baba yetu ameamua kuikatisha story baada ya kuona negative comments zimekuwa nyingi dhidi yake' na kakiri kabisa kuwa zina maongezea Maumivu ... So sad [emoji26][emoji26][emoji26]
 
We mzee nimefatilia hii story sanaaa ila kuna kitu nadhan unaficha kuna uwezekano mkubwa mke mkubwa ulimtelekeza na watoto wake maana mtiririko wote huu unaonesha ulikuwa unaspend muda mrefu na mchepuko kila tukio upo mpaka ya usiku alfajir upo unalala hukohuko sasa mke mkubwa hajui kama una mke meingine ulikuwa unamuaga vp????
 
Sa si mgawane tu,atakukodia watu wakuue ili aipate peke yake.kwani kwa mke wako wa ndoa ulifukuzwa?
 

FANYA MPANGO WA KUPATA UHALALI WA KUUZA HIYO NYUMBA NA ENEO LOTE AMBALO ANALIFAHAMU NI LAKO PIGA BEI UTAFUTE ENEO JENGINE UJENGE ASIBAKI NA KITU NA HAO WATOTO WANAONESHA TABIA ZA MAMA YAO KWA MBALI NI WATOTO WAKO WANA HAKI WATENGEE KIASI FULANI CHA PESA WAJITEGEMEE WABAKI NA MAMA YAO UACHANE NA MAMA YAO MAZIMA NI NYUMBA TU SAIV INAMFNYA AKUSUMBUE SIKU AKIRUDI AKIKUFA PAMEUZWA ATAJIPANGA UPYA
 
Huyu mwanamke simtaki tena, lakini naona kama anawapambe,

Nipeni ushauri wapendwa,
Maana ninachokiona siku moja huyu mwanamke anaweza rudimentary hapa kwa gia ya watoto
Huyo Bi Mdogo anakumudu. Jambo la msingi, tubu kwa bi mkubwa halafu mkabidhi hati ya hiyo nyumba ( ingawa hatujasikia upande wake wa stori ).

Mpaka sasa sijaona sababu ya wewe kuuza hiyo nyumba, kama ni Kwasababu tu huyo bi mdogo anapajua. Hata ukinunua prngine atapajua Kwasababu ya bond iliyopo kati yako na watoto.
 
Reactions: Cyb
Mkuu ifikie hatua tuwe waelewa, hata kwenye Tamthiliya kuna wahusika wakuu na wadogo wadogo, wanao angaziwa ni wahusika wakuu maana story inawahusu,

Sasa hapa mhusika mkuu ni huyo bi mdogo,amemzungumzia yeye zaid maana ndo mhusika story imemlenga, hivo haimaanish kwa bibi mkubwa kule maisha yamesimama sivyo.
 
Kwani mpaka sasa hati ya kiwanja na nyumba jina gani lililoandikwa?
Na documents zote anazo nani?
Kama katika hizo docs kuna majina yako fanya nenda mahakamani mfanye mpango uuze kiwanja pamoja na nyumba mgawane Mali nusu kwa nusu, haiwezi kuuma kumpatia nusu ya Mali sababu umezaa nae fanya Kama umewapa wanao.
Achana nae rudi kwa mke wako wa maisha
NB:inapoelekea unaweza ukajuta umefanya mauaji ukaishia jela ukajuta maisha yako yote ,vile vile anaweza kukodi genge la wahuni ukauliwa au kufanyiwa kilema wa maisha au ukalogwa ukawa chizi.
Ila yote kwa yote wewe ni mwanaume haswa ni wachache wanaweza kuvumilia hizi mambo wengine wangeshawekeana magunia ya mkaa
 
Huyu mwanamke simtaki tena, lakini naona kama anawapambe,

Nipeni ushauri wapendwa,
Maana ninachokiona siku moja huyu mwanamke anaweza rudimentary hapa kwa gia ya watoto
Mkuu umefika hatua hiyo ya ugomvi na mkeo wa ndoa hajui utaficha hadi lini,vipi akija kushitukizwa huoni utakosa wa kukingia kifua?ushauri wangu nenda umwombe radhi mkeo mkubwa then wachukue watoto mlee nae, achana na huyo hawala alikuonyesha kila makucha na kukutamkia yupo na wewe kimaslahi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…