Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Ha ha kila mmoja anachukua pointi zinamfaa na section aliyopo
 
Binamuuuuuuu baeleze baelewe.

Mimi ni bora iwaroge hao hao wanaume wanaoacha ndoa zao na kwenda kuhangaika na michepuko. Lakini michepuko mingi inaroga wake za watu ili wafe then wao ndio waolewe. Imagine mke kajituliza busy analea wanae afu anapigwa kipapai kimoja amazing anakufa anaacha watoto wake wakiwa. Mimi wawaroge tu hao hao wanaoenda kuwatafuta huko nje kwa starehe zao za kijinga

Bado wake wanaoambukizwa magonjwa, kuna wale ambao waume zao wanawachanganya na michepuko hadi wanapata mashinikizo ya moyo.

Kila mtu anywe maji kwa kisima chake jamani. Mara chache sana michepuko inaanza kutamani na kumroga mume wa mwenyewe from nowhere; mara nyingi nyie ndiyo mnakaribisha uharibifu kwenye familia zenu kwa kwenda kuifuata michepuko huko ilipo. Tulieni na wake zenu
 
Yaani kwa heshima niliyonayo kwa mke wangu na upendo Anaonionyesha, ni nguvu tu za Roho mtakatifu ndio zitaniongoza nimtamkie hilo neno, Mimi mwenyewe kama binadamu, naona siwezi
Una heshima kwa mkeo kweli?
 
Mtani umengea umemaliza... Tatizo huyu baba hataki kukubali ukweli kwamba mchepuko haujawahi kumpenda tena anajitahid mno kumkingia kifua!!
 
Kuna kitu kinakukimbiza kwa mkeo? Yaani unaenda kwenye nyumba tupu wakati familia iko mji huo huo? Ni kama unakwenda likizo fulani, kujiweka huru hivi!
 
Sidhan km alimpenda, huyu bwana alikuwa sponsor ndo walipoanzia na kuzaa hasa mimba ya kwanza ilitokea tu na kwa binti hiyo ilikuwa km daraja la kujiunganisha na sponsor kwa kuwa lazima atalea mtoto. Pili bint alivutiwa na mzee kwa kuwa alionyesha huruma na kumjali jambo ambalo kwa wakati huo ndo alilihitaji.
Kitu ambacho hakujiuliza mwanzo ni hulka ya binti, kitendo cha kuondoka kwa ndugu na kuanza maisha ya kuhaso ni kiashiria kwamba ni mtu wa kujitawala na dizaini hii hutaka uhuru wakishakuwa na hela na huona kuwa na mwanaume wa kumtawala ni utumwa.
 
Msiwe na imani haba kiasi hicho, kisa sijamkosoa mshkaji ndo mnaona ndo yeye na ID fake, sio lazma wote tufanane mitazamo aisee pia tumekulia familia tofaut so kila mmoja ana mtazamo wake akosoe au asahihishe na kumtia moyo mhanga.
Kumtia moyo mtu wa namna hii ni kupoteza muda

Halafu ni mapenzi hayo, wakati unamtia moyo hujui moyoni mwake anafikiria nini

Nikimtazama anatamani sana huyo mwanamke amrudie, wewe umeshatia moyo huku unakuja kusikia wamerudiana
 
Mimi amenishangaza alivyo na ujasiri wa kujivika mizigo, wamejuana kidogo tu kurupu amempangia chumba, mara amemnunulia kiwanja, mara amemuweka miradi eti vya watoto[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]kajitesa sana maisha yake
Hapo bado fainali uzeeni
 
Reactions: T11
Dah yaani ana hofia asirudi, anaomba Mungu asirudi, ni kwamba akirudi hana jeuri yoyote

Kwa umri mimi ni mdogo sana ukilinganisha na mleta uzi lakini natamani ningempa stori yangu aone maamuzi huchukuliwaje

Mtu mzima hana kabisa confidence ni suala kusikitisha

Hali hiyo hutokea unapotaka kuachwa na umpendaye lakini kuna wakati lazima uchukue maamuzi

Halafu baadae ndio unagundua kumbe maisha yanaweza kuendelea tu bila yeye
 
Kwa nn mmamshauri amweleze bi mkubwa?. Hapa hatujui ni changamoto gani za kipato au kimaisha bi mkubwa kazipitia hasa kwa namna ambavyo hiyo familia imekuwa kubwa na uhitaji. Wamepita ndugu kadhaa ili kusomeshwa achilia mbali watoto. Vipi kama kuna wakati alimwambia mama tufunge mkanda ilihali upande wa pili nao unatumia kipato hicho cha familia?. Km anauhakika bi mkubwa hakuwahi pitia changamoto za fedha amwambie, lakini kwa simulizi yake kuna wakati watoto walishindwa kwenda shule kwa wakati hapo mlo ndo sijui. Akienda kujieleza anaweza fufua makaburi akapata msamaha wa mdomo halafu mama aka deal na watoto kwamba wameteseka wakati kuna watu walikuwa wanahudumiwa, uzee wake utakuwa wa shida zaidi.
Binafsi namshauri ajipime na hata km itatokea bi mkubwa akawa anajua na akataka walimalize asisimulie mambo yote yaliyotokea.
 
Nakubali sana mzee wa dizonga...[emoji16][emoji16]

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
,[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Daah badala ya kusikitika ngoja nicheke, dada hivi ni sawa na mtu kusema wew ndo mshana jr huku unajua sio kabsa, mimi ndo mimi sina Id nyingine dada maana umekazia mno, au umenipenda maana hisia huelezwa kwa njia nyingi[emoji291]
[emoji1][emoji1][emoji1] Mimi jike na mshana wapi na wapi jamani, Mimi ctaki penda mtu humu JF ma single father kila corner na watoto Kijiji Nani ataka stress
 
Nimepitia ulichoandika mtoa mada na unavyojibu... inaonyesha still unampenda huyo mchepuko na akirudi utampokea kwa mikono miwili. Still uko inlove na yeye
 
Mleta mada atamsimulia bi mkubwa yote, akitegemea bi mkubwa amhurumie, aone mchepuko umechanganyikiwa ni mjinga, chizi, bila kujua atakuwa anaharibu..
Hapa kahadithia iwe kweli au uongo, lakini katia watu machungu na hasira, imagine bi mkubwa atakuwa na hali gani??
Labda huyu mke ana roho ya kipekee sana, kabarikiwa, hakasiriki, anamshukuru Mungu na kumtukuza kwa kila jambo.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…