Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

[emoji23] [emoji23] wengi tupo na michepuko,
Tunaangalia wapi tusikosee.

Na wadada/wamama wanaangalia wapi na nini cha kuwafanya waume zao ambao wana michepuko!

Na michepuko wanaangalia na kujifunza jinsi wanavyotakiwa nao kujengewa mijumba na kuachiwa mali za mil100.😀

Humu somo tupu kwa kila angle!
Pia tunajiburudisha tuepukane na hizi frastresheni za mi5 tena.

Everyday is Saturday................................😎
Ha ha kila mmoja anachukua pointi zinamfaa na section aliyopo
 
Wanawake wenzangu naomba niseme kwa maoni yangu kuna wanawake wachawi jamaniii msiombeee watu tuna maushuhudaa meengi hatusemi tumechoka tu.

Kuna wanawake wanaletwa mjini teknikali washavishwa maagano ya kichawi kwamba akifika akikutana na mwanaume mwenye hela amroge amtongoze,ahakikishe anamzalia anamtawala...Ukitazama story ya huyu baba jamani huu ni uchawi live yaani alirogwa akarogeka maana kwa status yake alishindwa kumpata mwanamke kazini kwake huko?kaenda tu kuvamia demu halafu huyo demu ukisoma vizuri alivompata mshikaji Akahma fastaa pale kwa mwenyeji wake. Huyo Dada ni mchawi maana kwa aliyofanyiwa na huyu mwanaume na vituko alivyofanyiwa si akili ya kawaida jamani.

Nawaomba ombeeni sana baba zetu,tuombee sana watoto wa kiume wetu,kaka zetu na zaidi waume zenu..UChawi upo na unafanya kazi na shetani yupo kazini...
Tunaweza shabikia kua amekomeshwa hatujui ndugu zetu wa kiume wanakula vichafu vingapi huko mitaani!Wanawake sisi miongoni mwetu ndo hao hao tunaharibu waume za watu.Jamani usiombe mmeo arogwe Yarrabi 'maji utaita mma'huyu hata kusomesha kasomesha humu hakuna wametelekezwa na wazazi kisa michepuko baba hana time kabisaa yaani na familia...
Kama baba yako hana mtoto nje,au mmeo hana mtoto nje shukuru sana Mungu lakini mke pekee anaejua mumewe alipo ni mjane.
Vita kubwa nje tena sana haijaanza Jana wala juzi wanawake wengi kuliko wanaume
Huyu baba sasa hivi akili inafunguka limbwata halina nguvu tenaa ndo maana anahangaika na ana Mungu wengine wanauliwa ,wanakufa na kudhulumiwa saanaa tu...arudi kwa Mungu apige goti atakaa sawa hajachelewa kwa Mungu bado mpk siku akiitwa maiti

Waswahili wanasema CHEKA SANAAA,ILA OMBA YASIKUKUTE!

Sent using Jamii Forums mobile app
Binamuuuuuuu baeleze baelewe.

Mimi ni bora iwaroge hao hao wanaume wanaoacha ndoa zao na kwenda kuhangaika na michepuko. Lakini michepuko mingi inaroga wake za watu ili wafe then wao ndio waolewe. Imagine mke kajituliza busy analea wanae afu anapigwa kipapai kimoja amazing anakufa anaacha watoto wake wakiwa. Mimi wawaroge tu hao hao wanaoenda kuwatafuta huko nje kwa starehe zao za kijinga

Bado wake wanaoambukizwa magonjwa, kuna wale ambao waume zao wanawachanganya na michepuko hadi wanapata mashinikizo ya moyo.

Kila mtu anywe maji kwa kisima chake jamani. Mara chache sana michepuko inaanza kutamani na kumroga mume wa mwenyewe from nowhere; mara nyingi nyie ndiyo mnakaribisha uharibifu kwenye familia zenu kwa kwenda kuifuata michepuko huko ilipo. Tulieni na wake zenu
 
Yaani kwa heshima niliyonayo kwa mke wangu na upendo Anaonionyesha, ni nguvu tu za Roho mtakatifu ndio zitaniongoza nimtamkie hilo neno, Mimi mwenyewe kama binadamu, naona siwezi
Una heshima kwa mkeo kweli?
 
Ujue nimehisi hata ukute mke mkubwa ameshajua ila amemute tuu. Yaan babangu anijali maisha yangu yote halafu nimpotezee? Kuna shida mahali.

Baba dai Mzee Abdul alisema kuzaa si kupata.
Nachoamini mzee wetu ni kwamba bado hajakubaliana na ukweli kwamba mchepuko haukuwahi kumpenda. Tunamwambia ukweli sisi kama wanawake. Aliona hapa ndo uhakika ndo maana akakazia hapohapo. Angeenda jiua basi. Huyo mchepuko na yeye aliwaza maumivu ya mke mkubwa? Its all about her. Kila kitu anawaza juu yake hawazii mke halali.

Haijawahi kutokea mchepuko akawa na upendo wa kweli angali anajua kbs jamaa ana mkewe halali. Lazima ajipooze. Na tumeona makandolando toka mwanzo anashinda kkoo na wafanyabiashara. Kuna mengine nadhan mzee wetu anamsitiri mchepuko.

Yaani natamani sana aweze pata ujasiri wa kumweleza mkewe kila kitu. Kama wewe ni mchagga njoo tuchukue ukoo mzima tukusindikize na masale[emoji23][emoji23] utasamehewa na utapata amani kabisa.

Mungu amsaidie maana namhurumia sana. Yaani nisivyopendaga stress zaman ningeshajipeleka kwa mke wangu nimweleze kinaga ubaga.

Mapenzi ya namna hii hayajawahi fika kabisa mbali. Hayadumugi. Fedha ikiisha na kila kitu kimeisha.
Mtani umengea umemaliza... Tatizo huyu baba hataki kukubali ukweli kwamba mchepuko haujawahi kumpenda tena anajitahid mno kumkingia kifua!!
 
Ni mkubwa sikuwahi kumtelekeza kamwe, namwangalia kama mboni ya jicho langu, sitaki hata augue, akiwa hata mafua tu roho yangu inaumia sana,
Tofauti yake na yule, ananisifia sana kwa namna nilivyowasomesha watoto wake,
Na namna ninvyoijali familia yake,

Hata miaka tuliyaishi kwenye ndoa anajivunia sana, akiangalia wenzake wakati wa usichana na leo, yeye wanamheshimu,
Na wenzake wengi wameachika huko,

Nampenda vile vile, ni kama yeye ameibeba famili, kuanzia kwenye vishughuli mbalimbali yeye ndio msemaji,Mimi siwezi kuzungumza hadharani, lakini yeye hata watu wapo 1000
Anazungumza
Mtaani kwetu yeye ni leader wa vikundi vingi tu
,
Na akiwa na wenzie ana feel very proud kunitambulisha kwa wenzake

Kuhusu kwamba nilikuwa napika, ni kweli kule naenda, na kwa kuwa watoto hawapo napika mwenyewe, na kwa mazingira ya kule ni tulivu sana, basi muda mwingi , nakula .nakunywa, nalala naoga, nasoma, magazei, naingia mitandao, ya kijamii,
Na muda wote nipo boxer tu

Mpaka wamama wa kule wananishangaa mimi ni mtu wa aina, hata mwanamke siingizi!!!
Kuna kitu kinakukimbiza kwa mkeo? Yaani unaenda kwenye nyumba tupu wakati familia iko mji huo huo? Ni kama unakwenda likizo fulani, kujiweka huru hivi!
 
Binafsi naamini huyu bi mdogo alikuwa na mapenzi na wewe. Mwanamke mpaka kufikia hatua ya kuzaa na wewe kuna sehemu ndani ya moyo wake unakupenda. Kumbuka pia una mke mkuu, upendo wake kwako ulikuwa unakutana na kizingiti cha wewe kuwa na mke, so inabidi pia uvae viatu vyake. Pia duniani hakuna upendo unaokuja bila ya "kisababishi". Kila mtu anampenda mtu flani kwa sababu ya kitu flani. Huo ndio uhalisia. Unaweza kupendwa kwa sababu ya uhandsome wako. Unaweza kupendwa kwa sababu ya urembo wako, usingekuwa mrembo usingependwa. Unaweza kupendwa kwa fedha zako. Hakuna kupendwa bila kisababishi. Kisababishi kikitoweka either utaachwa au utavumiliwa.
Sidhan km alimpenda, huyu bwana alikuwa sponsor ndo walipoanzia na kuzaa hasa mimba ya kwanza ilitokea tu na kwa binti hiyo ilikuwa km daraja la kujiunganisha na sponsor kwa kuwa lazima atalea mtoto. Pili bint alivutiwa na mzee kwa kuwa alionyesha huruma na kumjali jambo ambalo kwa wakati huo ndo alilihitaji.
Kitu ambacho hakujiuliza mwanzo ni hulka ya binti, kitendo cha kuondoka kwa ndugu na kuanza maisha ya kuhaso ni kiashiria kwamba ni mtu wa kujitawala na dizaini hii hutaka uhuru wakishakuwa na hela na huona kuwa na mwanaume wa kumtawala ni utumwa.
 
Msiwe na imani haba kiasi hicho, kisa sijamkosoa mshkaji ndo mnaona ndo yeye na ID fake, sio lazma wote tufanane mitazamo aisee pia tumekulia familia tofaut so kila mmoja ana mtazamo wake akosoe au asahihishe na kumtia moyo mhanga.
Kumtia moyo mtu wa namna hii ni kupoteza muda

Halafu ni mapenzi hayo, wakati unamtia moyo hujui moyoni mwake anafikiria nini

Nikimtazama anatamani sana huyo mwanamke amrudie, wewe umeshatia moyo huku unakuja kusikia wamerudiana
 
Mimi amenishangaza alivyo na ujasiri wa kujivika mizigo, wamejuana kidogo tu kurupu amempangia chumba, mara amemnunulia kiwanja, mara amemuweka miradi eti vya watoto[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]kajitesa sana maisha yake
Hapo bado fainali uzeeni
 
  • Thanks
Reactions: T11
Tatizo mzee anaamini yuko perfect. Namsihi awe na msimamo. Bado ana mapenzi kindakindaki kwa mchepuko. Huoni anaogopa asirudi maan hana ujasiri wa kumtawala. Nataman niombe undugu kwa jamaa halaf huyo mchepuko anikuteee..

Ila na mzee wetu azibuliwe kofi moja atoke usingizini
Dah yaani ana hofia asirudi, anaomba Mungu asirudi, ni kwamba akirudi hana jeuri yoyote

Kwa umri mimi ni mdogo sana ukilinganisha na mleta uzi lakini natamani ningempa stori yangu aone maamuzi huchukuliwaje

Mtu mzima hana kabisa confidence ni suala kusikitisha

Hali hiyo hutokea unapotaka kuachwa na umpendaye lakini kuna wakati lazima uchukue maamuzi

Halafu baadae ndio unagundua kumbe maisha yanaweza kuendelea tu bila yeye
 
Ujue nimehisi hata ukute mke mkubwa ameshajua ila amemute tuu. Yaan babangu anijali maisha yangu yote halafu nimpotezee? Kuna shida mahali.

Baba dai Mzee Abdul alisema kuzaa si kupata.
Nachoamini mzee wetu ni kwamba bado hajakubaliana na ukweli kwamba mchepuko haukuwahi kumpenda. Tunamwambia ukweli sisi kama wanawake. Aliona hapa ndo uhakika ndo maana akakazia hapohapo. Angeenda jiua basi. Huyo mchepuko na yeye aliwaza maumivu ya mke mkubwa? Its all about her. Kila kitu anawaza juu yake hawazii mke halali.

Haijawahi kutokea mchepuko akawa na upendo wa kweli angali anajua kbs jamaa ana mkewe halali. Lazima ajipooze. Na tumeona makandolando toka mwanzo anashinda kkoo na wafanyabiashara. Kuna mengine nadhan mzee wetu anamsitiri mchepuko.

Yaani natamani sana aweze pata ujasiri wa kumweleza mkewe kila kitu. Kama wewe ni mchagga njoo tuchukue ukoo mzima tukusindikize na masale[emoji23][emoji23] utasamehewa na utapata amani kabisa.

Mungu amsaidie maana namhurumia sana. Yaani nisivyopendaga stress zaman ningeshajipeleka kwa mke wangu nimweleze kinaga ubaga.

Mapenzi ya namna hii hayajawahi fika kabisa mbali. Hayadumugi. Fedha ikiisha na kila kitu kimeisha.
Kwa nn mmamshauri amweleze bi mkubwa?. Hapa hatujui ni changamoto gani za kipato au kimaisha bi mkubwa kazipitia hasa kwa namna ambavyo hiyo familia imekuwa kubwa na uhitaji. Wamepita ndugu kadhaa ili kusomeshwa achilia mbali watoto. Vipi kama kuna wakati alimwambia mama tufunge mkanda ilihali upande wa pili nao unatumia kipato hicho cha familia?. Km anauhakika bi mkubwa hakuwahi pitia changamoto za fedha amwambie, lakini kwa simulizi yake kuna wakati watoto walishindwa kwenda shule kwa wakati hapo mlo ndo sijui. Akienda kujieleza anaweza fufua makaburi akapata msamaha wa mdomo halafu mama aka deal na watoto kwamba wameteseka wakati kuna watu walikuwa wanahudumiwa, uzee wake utakuwa wa shida zaidi.
Binafsi namshauri ajipime na hata km itatokea bi mkubwa akawa anajua na akataka walimalize asisimulie mambo yote yaliyotokea.
 
Mie nahisi kama ushauri wako sio realistic kama unavyomtaka mleta mada awe realistic. Haya ni maisha and we live once. Huyo unayemuita "mchepuko" naye ni binadamu na ana moyo wa nyama unaoumia kama binadamu mwingine. Binafsi ndoa ni ule uridhiano wa wawili kuishi pamoja. Hayo mengine ya kanisani au misikitini ni makaratasi tu na formality za kumanipulate ubongo wetu uamini kuwa ndoa ni hicho kipande cha karatasi. Bi mdogo na bi mkubwa wote wana nafasi sawa tu. Wote ni wanawake na wote wamezaa na jamaa. Hicho kikaratasi cha ndoa hakimfanyi bi mkubwa kuwa tofauti na mwenzake. Hebu niambie tofauti ni ipi kati ya bi mkubwa na bi mdogo ukiweka pembeni hicho cheti cha ndoa? Wote ni wanawake, wote wamezaa na wote wanapendwa na mleta mada.
Nakubali sana mzee wa dizonga...[emoji16][emoji16]

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
[emoji23] [emoji23] wengi tupo na michepuko,
Tunaangalia wapi tusikosee.

Na wadada/wamama wanaangalia wapi na nini cha kuwafanya waume zao ambao wana michepuko!

Na michepuko wanaangalia na kujifunza jinsi wanavyotakiwa nao kujengewa mijumba na kuachiwa mali za mil100.😀

Humu somo tupu kwa kila angle!
Pia tunajiburudisha tuepukane na hizi frastresheni za mi5 tena.

Everyday is Saturday................................😎
,[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Daah badala ya kusikitika ngoja nicheke, dada hivi ni sawa na mtu kusema wew ndo mshana jr huku unajua sio kabsa, mimi ndo mimi sina Id nyingine dada maana umekazia mno, au umenipenda maana hisia huelezwa kwa njia nyingi[emoji291]
[emoji1][emoji1][emoji1] Mimi jike na mshana wapi na wapi jamani, Mimi ctaki penda mtu humu JF ma single father kila corner na watoto Kijiji Nani ataka stress
 
Nimepitia ulichoandika mtoa mada na unavyojibu... inaonyesha still unampenda huyo mchepuko na akirudi utampokea kwa mikono miwili. Still uko inlove na yeye
 
Kwa nn mmamshauri amweleze bi mkubwa?. Hapa hatujui ni changamoto gani za kipato au kimaisha bi mkubwa kazipitia hasa kwa namna ambavyo hiyo familia imekuwa kubwa na uhitaji. Wamepita ndugu kadhaa ili kusomeshwa achilia mbali watoto. Vipi kama kuna wakati alimwambia mama tufunge mkanda ilihali upande wa pili nao unatumia kipato hicho cha familia?. Km anauhakika bi mkubwa hakuwahi pitia changamoto za fedha amwambie, lakini kwa simulizi yake kuna wakati watoto walishindwa kwenda shule kwa wakati hapo mlo ndo sijui. Akienda kujieleza anaweza fufua makaburi akapata msamaha wa mdomo halafu mama aka deal na watoto kwamba wameteseka wakati kuna watu walikuwa wanahudumiwa, uzee wake utakuwa wa shida zaidi.
Binafsi namshauri ajipime na hata km itatokea bi mkubwa akawa anajua na akataka walimalize asisimulie mambo yote yaliyotokea.
Mleta mada atamsimulia bi mkubwa yote, akitegemea bi mkubwa amhurumie, aone mchepuko umechanganyikiwa ni mjinga, chizi, bila kujua atakuwa anaharibu..
Hapa kahadithia iwe kweli au uongo, lakini katia watu machungu na hasira, imagine bi mkubwa atakuwa na hali gani??
Labda huyu mke ana roho ya kipekee sana, kabarikiwa, hakasiriki, anamshukuru Mungu na kumtukuza kwa kila jambo.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Back
Top Bottom