Unahofu ya bure kabisa. Km nyumba ina hati yako wewe ndie mwamuzi. Kisheria ni mali yako. Amua upendavyo km ataona haki yake imekiukwa aende mahakamani.Nilibadili nakaweka majina yangu,
Haina majina ya watoto tena
Mimi naona wewe ndio hauko sawa. Jifunze kuongea na wakubwa na jifunze kusikiliza na kushauri vizuri,ukicomment soma tena kama lengo ni kushauri,kukasirisha au kukera.Ndio Hilo ni funzo kwa wanaume I wonder stress zao wanimalizia mimi
Wewe unaongelea ndoa gani? Ndoa ya serikali hapo tayari wala haina shaka.
Hahaaa over my dead body, hamu zikiisha kila mtu a mind business zakeSasa unatakiwa uliabudu kulitukuza na kulitumikia
Nitazidi kuandika ninachoamini as long as sivunji sheria za JF na nchi na Niko huru. So nitazidi kuandika lolote ninslojiskia hayo maoni yenu ni beliefs na perceptions za watu Wana ni view. In short I do what I wantMimi naona wewe ndio hauko sawa. Jifunze kuongea na wakubwa na jifunze kusikiliza na kushauri vizuri,ukicomment soma tena kama lengo ni kushauri,kukasirisha au kukera.
Kwa umri wako unamengi ya kujifunza. Utajifunzia wapi kama sio kwa changamoto za watu? ( wewe unahukum).
(na hii comment utaijibia shit)
Asante kwa ufafanuzi.Kisheria kama mtoa mada alifunga ndoa ya kwanza kanisani basi huyu mwingine hata angeishi nae miaka mia ni kimada. Serikali haitachukulia huyu mwingine kama mke. Isipokuwa watoto wa huyu mwanamke wana haki kupata sehemu ya mali ya baba yao.
Kibaya zaidi hati imeandikwa kwa majina ya mtoa mada labda ingeandikwa kwa majina yao wote. Kifupi mtoa mada ameshika mpini.
Changudoa atakuleteaje mimba?Na changudoa atakuletea mimba nyumbani,
Kama hutaki hayo mambo acha kabisa kudeal nayo
Kwa nini uhangaike na machangu,
Na ukiacha tunajua wewe ni mwanaume suruali,
Hivi kwa akili yako unafikiri tupo hapa duniani kwa ajili ya nini ndugu,
Mimi nilishajitambua, kuwa, hapa duniani tupo kwa ajili ya vitu 3 tu,
1- KULA
2- KWENDA CHOONI
3- NGONO
basi, vingine vyoteeee ni mbwembwe tu!!!!
Bhututu, ahsante sana,Unahofu ya bure kabisa. Km nyumba ina hati yako wewe ndie mwamuzi. Kisheria ni mali yako. Amua upendavyo km ataona haki yake imekiukwa aende mahakamani.
Ukiamua kuuza uza. Hati yako utampa mnunuzi,itie sokoni hio nyumba.
Am blessed kwa huu ushauriNimesoma story mwanzo mwisho. Wewe ni mwamba aisee. Hongera zako.
Inavyoonekana ulisha tengena au ulimtelekeza bi mkubwa kwa hiyo huna mke kwa sasa.
Hii ndo sababu unapata shida.
1. Unamuona huyo bi mdogo ndo mke wako. Maana bi mkubwa hayupo.
2. Huwezi kuachia nyumba maana utakosa pa kukaa.
3. Umeshaingiwa na uoga wa kutafuta mwanamke mwingine ili yasije yakatokea kama yaliyotokes kwa huyu bi dada.
4. Watoto wako wa mke mkubwa uliwatelekeza hivyo ni ngumu kwao kukisaidia.
5. Uliweza kufanya hayo yote enzi za JK na sasa hizi zama za Magu maisha yamekuwa magumu huwezi kufanya mambo makubwa kama awali.
Kama hizo assumption hapo juu ni sahihi. Nakushauri
1. Rudisha mpira golini. Anza upya. Achana na huyo bi mdogo, achana na hao unao waita watoto wako wa bi mdogo. Waachie nyumba. Uondoke zako. Kama wakiuza shauri yao au wakipangisha shauri yao. Usijipe pressure. Umeshawatoa mbali, hapo walipo fika acha wajimalizie wenyewe.
2. Ita watoto wako wakubwa. Waambie ukweli wa mambo kama ulivyotiririka hapa. Wao wataamua cha kufanya. Kama wana busara watawa sulihisha na mama yao familia irudi kama zamani. Kama wakiwa wajinga achana nao. Wewe waambie tu basi.
3. Nadhani bado unafanya kazi. Unaweza kupanga kwa muda huku ukivuta nguvu za kuja kujenga nyumba ya uzeeni.
4. Tulia kidogo baadae tafuta mtu mzima mwenzako myamalizie maisha yaliyobaki pamoja.
Ushauri wenu ni muhimu sana.
Umri wangu ni miaka 50, nimeoa mke kanisani huu ni mwaka wa 25 naishi naye na tumejaliwa watoto wanne, wa kwanza na wapili wamemaliza tayari chuo kikuu na wa tatu yupo chuo kikuu mwaka wa pili. Wa nne kamaliza kidato cha 4 mwaka jana, katikati hapo miaka 18 iliyopita bahati mbaya nikajiingiza kwenye mahusiano na binti wa miaka 20 wakati huo na akapata ujauzito, nilipomwambia nimeoa ili aitoe mimba ile na kwa kuwa bado ni binti mdogo anaweza kupata wa kumwoa, alikataa katakata. Na mimi kwa kuogopa maana alinitamkia kuwa atajiua kama nitamlazimisha kutoa mimba na kuwa yupo tayari kuishi na mimi kama mke wa pili na ujauzito ule hawezi kutoa kamwe.
Niliendelea kumshawishi atoe, matokeo yake akakimbia akaenda kwao mpaka akajifungua huko.
Lakini kiufupi zaidi, alirudi tena na kunitafuta na kunitishia kumwambia mke wangu, hivi ninavyoandika ilibidi nirudishe nyuma majeshi na kuanza kuishi naye kama mke wa pili.
Nilimpangishia chumba na maisha yakaendelea, baada ya muda alipata mtoto wa pili, wote ni wa kike, baada ya muda nilianza kuwasomesha kuanzia chekechea mpaka sasa hivi wa kwanza anafanya mtihani wa form Six mwaka huu na wa pili anafanya wa form 4 mwaka huu na wote wamesoma shule za Private toka chekechea mpaka sasa hivi na kwa wastani kila mmoja alikuwa ananigharibu 2.5m hasa shule za msingi mpaka secondary. Hapo bado michango mbalimbali na usafiri, kwa maana walikuwa wanasoma mikoani.
Baada ya kumpata mtoto wa kwanza akiwa kwenye chumba cha kupanga, niliona sina budi watoto wangu na mimi binafsi niwe na uhuru maana maisha ndio yalishaanza hivyo, na mimi upendo tayari ulishaingia na kuona ni maisha kama maisha mengine.
Ndipo nilipoamua kununua viwanja, kama unakumbuka miaka ile ya 2000 nadhani kuanzia 2006 serikali ilipima viwanja 20,000 maeneo mbalimbali ya DSM, mimi nilichukua viwanja viwili, wakati ule nakumbuka kimoja nilinua 1,800,000 na kingine 1,300,000 ml. Ukubwa ni sq m 1200 na 1000. Kimoja kikubwa nikamjengea nyumba ya mgongo wa tembo, vyumba 2 na sebule katikati na choo kizuri cha nje, nikaacha eneo kubwa tu kwa ajili ya kujipanga na kujenga nyumba kubwa baadaye, kumbuka huo ni mwaka 2007 alipohamia hapo au tulipohamia hapo.
Baadaye nimfungulia biashara ya saloon, akafanya kama miaka 2 vibaka wakaingia nakuiba kila kiatu, nikaona isiwe shida nikamfungulia mghahawa ambao ulikuwa na vitu 16 na meza nne kubwa, bado na wenyewe haukufanya kazi vizuri, nikamfungulia grocery ya bia na kuweka kila aina ya kinywaji kwa kutumia viti na meza za mghahawa.
Nayo haikufanya kazi vizuri, nikamnunulia Hiace iliyotumika tayari kama dala dala.
Na yenyewe usimamizi ukawa mgumu.
DA NITAENDELEA, MAANA DA SIPO VIZURI KABISA KIAKILI NI NIMECHANGANYIKIWA SASA HIVI.
SEHEMU YA 2
MUENDELEZO WA TUKIO HILI SOMA HAPA CHINI:
SEHEMU YA 3
SEHEMU YA 4
SEHEMU YA 5
SEHEMU YA 6
SEHEMU YA 7
SEHEMU YA 8
SEHEMU YA 9
SEHEMU YA 10
SEHEMU YA 11
SEHEMU YA 12
SEHEMU YA 13
SEHEMU YA 14
SEHEMU YA 15
SEHEMU YA 16
SEHEMU YA 17
SEHEMU YA 18
SEHEMU YA 19
SEHEMU YA 20
SEHEMU YA 21
Ahsanteni sana wapendwa, ushauri wenu,
Mmekuwa ni msaada mkubwa sana kwangu,
Kiujumla nitambua wapi nilikosea,baada ya ushauri wenu mzuri sana nimejifunza mengi sana ambayo nilikuwa siyafahamu hasa kwenye mambo ya mahusiaona,
Kwa wale waliokuwa na wasiwasi kuwa hiki kisa sio cha kweli, niwatoe wasiwasi huo kuwa ni cha KWELI hasa.
Uamuzi wangu wa mwisho baada ya ushaui wenu ni kupiga nyumba bei na kujenga nyingine kwa ajili ya Watoto,
Na sehemu ya kuijenga ni kati una nyumbani kwetu kijijini lakini mjini sio kijijini
Nimeamua niijenge huko kwa sababu mbili
Kwanza nimeamua nikistaafu kunako majaliwa nitahamia huko kijijini
Pili, sitaki mama siku aje arudi na kukaa nao huku tena na kufaidi tena nyumba ya guys kwa mgongo wa watoto
Vile vile ikiwa kule, itakuwa rahisi kuwa nao, na wenyewe wajione ni sehemu ya ukoo wetu kule karibu zaidi
Kwa hayo machache Ahsanteni sana.
Ombi kwa MODE,
Naomba nisamehe sana, najua kuna sehemu nilikosea, na ukanifungia,
Lakini ni mhemko ulinipatia sina tabia hizo za kihuni
Ahsante sana kwa kunielewa
DuhLooking For Your PM.
Sawa nimekuelewa,Sijaona mtu yeyote alisema huyu mtu kalogwa ila ki uhalisia mwanaume ambaye hadi mke anaye tena na shule kaenda HAWEZI kufanya mambo ambayo huyu anko wetu anaelezea kafanya...
Kwenye maisha hasa sisi wanaume hamna kutu kitakutoa nje ya mchezo/maisha kama ukikurupikia wanwake hovyo Hasa narudia tena hasa kama tayari umeshapata maisha yako mazuri...
Mazoea na michepuko tutapata wapi??????hamnaga mke mdg ambaye hujamuoa HAYUPO narudia tena HAYUPO..
Mi nilishasema kama kulogwa LABDA na mke wangu wa ndoa walau nitakuwa na kusema nilimuoa nilijua ananipenda kumbe tapeli kaniloga ila hawa wanwawake wa pembeni formula yao ni km ni mhm kuwa nao basi nikifikisha mwezi na mchepuko basi ni kama nimefikisha miaka 10.
Jmn plan yeyote ya maisha panga na mkeo ukioa mwanamke haeleweki panga mwenyewe.sasa mtu unaanzaje kupanga maisha na mwanamke wa nje????Ili iweje???narudia tena anko umelogwa na shukuru dawa inaisha Nguvu.
Yaani hapa bro elimu yako haijakusaidia kabisa...
Hlf huna maamuzi magumu hii nayo shida kubwa sasa sijui ndo madawa.Tulikuwa tunapendana no no no hiyo kauli ya tulikuwa tunapenda ni bora u bet kwa mkeo wa ndoa tutakuelewa huwezi kupendana na mwanamke wa nje HAIPO.
Mwanamke ni kiumbe mmoja dhaifu sana kwa muonekano LAKINI hamna kiumbe anajua kusuka mkakati kwa kutumia akili yake na hisia zake zote km mwanamke.
Jamani hivi wanaume wenzangu hamuogopi?mtu anakubali kuolewa na mwanaume kisa pesa na anakaa nae miaka 10 huku akiwa na tabasamu usoni mpk siku mwanaume anafirisika ndo anakuja kugundua kumbe mwanamke niliyekuwa nae miaka 10 ndoani hajawahi kunipenda alikuwa anapenda mali zangu...Dont underestimate mwanamke kabisaaaaa hasa nilinapokuja swala na mahusiano USiThubutu...koma kabisa .Mwanamke ana attack kipindi ambacho anajua atashinda pambano kamwe hakurupuki kabisa.
Mfano utashika pesa zako utamdharau mkeo mixer matusi na michepuko nje nje yeye yupo busy kukusamehe,kwa upumbavu wako unamuona mjinga hana pakwenda sasa mapombe yako yamekupelekea umepata kisukari nguvu ya kwenda kazini huna na madeal yote yameisha,pesa huna pale sasa ndo mwanamke anaku attack.Pale ndo utajua mwanamke ni nani? pale ndo utajua mwanamke alikuwa anakuchukuliaje hahahaa bro kuwa makini na mwanamke sio dhaifu moja kwa moja.Usiombe ujue nguvu ya mwanamke kipindi ana ku attack kutoboa hiyo vita ni kazi sana wengi wetu uwaga tunakufa tu mapema.
Sasa kwenye mahusiano yako na huyu mwanamke hukutakiwa hata kufika huko kote...
Ulipaswa
1.kuvunja mahusiano kusomesha watoto.
2.Naungana na wengine kumwambia mkeo ukweli tu “mama nimebolonga huko nahisi maji yamefika shingoni nisamehe,sina jinsi yakutatua hili tatizo peke yangu bila kukushirikisha wewe nimeshindwa mke wangu nisamehe”
Mazoea ya mda mrefu na mchepuko yanakufanya umuone mkeo km f.ara flani hivi au zezeta hivi lisilo na mvuto sasa pata matatizo ndo utajua yupi mkeo kweli,yupi mchepuko
All in all,Uza nyumba gawa mafungu matatu 1/3:1/3:1/3.chukua chako,watoto chao weka bank na mke mpe chake.
Hapo utakufa mapema zaidi,OndokAAAAAAAA
Full of Faith,Pole sana kiongozi kwa changamoto na hongera kwa uvumilivu na ujasiri.Nina imani humu utapata ushauri mzuri sana.
Naomba kufahamu unataka ushauri kwenye jambo gani hasa kwa sababu uzi umezungumzia Mke mkubwa,Mke mdogo,watoto na mali.