Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Ni kweli, siwezi mwanamke ambaye roho yangu haimpendi, siwezi kukaa naye hata Dk moja, ila naye lazima anipende , kama huyu kusema ukweli alinipenda sana, ukiona mwanamke mpaka anakulalia miguuni mpo chini ya mti mnasililiza radio band mbili, huyo ni wako,
Ila awe bado mbichi hawa wakubwa wakubwa wanaweza kuwa na malengo yao
[emoji16] [emoji16] [emoji16]

Nimecheka sana hapo kwenye eti mpo chini ya mti anakulalia miguuni huku mkisikiliza radio yenye band mbili.
 
Hata sasa hivi tupo tunae kanisani,
Alifahamu nina bi mdogo, lakini tena ndio afanye nini na limbwata ndio lilishaingia,

Hii mikasa haifahamu,
Ila alikuja kushangaa kipindi kile bi mdogo ameenda kwa biashara na kupotea majumla, kusema kweli nilikonda mpaka akawa na wasiwasi,

Baadaye akajua ndio kaenda mazima, kwa hiyo kwake ikawa ahueni
 
Pole kaka wanaume tunapitia matatizo mengi ,nimekuhurumia
Hahaa, ndugu yangu, utaendelea asubuhi, mimi nilivyo sasa najiona kama sio mtu,
Sina usingizi, sili, hata nilvyosema naenda kula wala sikula chakula chenyewe kiliungua,

Hawa wanawake hawa we acha tu, Mungu atawageuzia kibao tu, yaani mimi ni mtu wa kukesha kabisa, hata kula sili, kwa shida gani hasa yarabi,?

Haya ngoja nikaoge nijiandae kwenda kazini, labda nitasinzia huko.
 
Wewe ndio una shida alivomaanisha na Mimi nimemjibu in general kwanini mje kunishambulia acheni unafiki aisee, hafu sio kila mtu ana mawivu na kutamani Jambo flani sio dhambi mbona hata yeye alichepuka na mchepuko unamsumbua tu.
Ww mbona unanyoshewa kidole na kila mtu ,acha kufatilia uzi wa watu bidada
 
Tatizo story mmeidandia katikati au hamsomi kwa umakini. Kwa kukusaidia tu ni kwamba kulikuwa na makubaliano ya hiyo hela iwe deposited kwenye account ya bi mdogo. Mnunuzi wa hicho kiwanja na ile nyumba na kila kilichokuwa ndani aliambiwa hiyo hela ataideposit kwenye account ya bi mdogo. Kumbuka hicho kiwanja na nyumba iliyouzwa ilikuwa nyumba aliyojengewa bi mdogo. Please muwe wafuatiliaji wazuri kabla hamjaanza kulaumu.
Wana hawasomi wakaelewa kabisa
 
Ufafanuzi mzuri sana,

Kwa kuwa bi mdogo mpaka leo hayupo kwangu, na haitatokea arudi kwangu tena, kwa sababu nasikia analima mpunga na jamaa, na mama yake mzazi nimeshamweleza,

Naomba kila anaye hitaji ufafanuzi zaidi awe huru kuuliza,

Mambo ni mengi na mimi nimeamua kufunguka,

Tar 4/3 naenda kwenye graduation ya binti yangu anamaliza Form six

Ahsante
 
Kwa hiyo kwa kumpa vyakula vya usiku na mchana....nguo na nyumba ndio umemheshinu mkeo???

Ndugu yangu...

Kwa mtazamo huo watakupiga tu hao wanawake.....
Kutokuheshimu kitu gani, ndoa?

Ninauhakika gani kwamba yeye anaiheshimu ndoa, kwani simpi chakula, iwe cha usiku au mchana, havai? Sijamjengea nyumba? Watoto wako siwasomeshi?

Hivi unafahamu hawa wake zetu wa ndoa na wenyewe wana michepuko yao,?

Tena wenyewe ni mibaya kabisa!
Maana pesa unahenyekea wewe ndio wanalipia guest huko, na wengine mpaka wanawajengea nyumba kawa pesa zako

Hebu nikuulize, kwani hawa wanaoitwa MARIOO ni Nani nani wanawafinance? Ni hawa wake zetu wa ndoa ndugu,

Wewe jifanye mtakatifuuu, henyeka kama punda kumbe yeye anakidumu chake huko,

Akishazeeka anakimbilia kwa watoto wake, unabaki mwenyewe,

Nimeambiwa sana humu nikishazeeka napigwa kibuti, lakini hawajui hata wenyewe wakizeeka huwa tunaomba waende hukohuko kwa watoto wao,
Ananikalia hapa nyumbani kunizibia nafasi tu, wakati mimi nataka dogodogo, alaaaa,

WANAUME EEE, WANAUME EEE,

Tujiandalie maisha yetu binafsi ya uzeeni,
Kama kushikwa sikio tumeshashikwa,

UNASUBILI NINI?
 
Kwa hiyo ulitaka nifanyeje,
Kwanza hebu niambie wewe una mke,
Una umetafsiri nini chakula cha usiku, unafikiri ni ugari?

Nauliza tena unataka nimfanyie nini, au unataka niinyofoe niwe natembea nayo mfukoni
 
Ww mbona unanyoshewa kidole na kila mtu ,acha kufatilia uzi wa watu bidada
Mimi hata dunia nzima ikininyooshea kidole I don't care,siwezi kuwa mnafiki na muongo kwa ninachoamini, misimamo wangu ni ule ule tu, since jamii yetu unafiki ni kiupaumbele kikubwa kuliko chochote, so Mimi sijali wengine wanavotaka nifikirie ka wao. Mimi ni mimi na stick na rules zangu bas
 
Full of Faith,
Ahsante nilishapata ushauri,
Ila kama bado unaushauri mwingine ni vizuri sana, ushauri niliokuwa nahitaji ni ,

1, je huyu mwanamke ana haki zozote kuhusu mali yangu?

2, je akirudi na kusema kuwa pale ndio kwake na akanifanyia fujo nikimfukuza nitakuwa natenda kosa?, kumbuka nimeishaenda polisi kutoa taarifa 3

3, hayo mawili ndio ulikuwa msingi hasa wa kuomba ushauri wenu,

KUMBUKA SIJAWAHI KUFUNGA NDOA NAYE,
NA MIMI NINA MKE WA NDOA YA KANSANI

lakini la mwisho ambalo sijaona ushauri wenu ni je,

WATOTO WANA HAKI YA KUSIMAMISHA NYUMBA ISIUZWE?

Ni hayo tu ndugu yangu.
Asante

Kuhusu hilo jambo la watoto kuzuia nyumba kuuzwa,kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa hawana nguvu hiyo kwa sababu hati ipo kwa jina lako na pia haujafunga ndoa na huyo mke mdogo.

Wataalam wa sheria ya mirathi wanaweza kutusaidia hapa.
 
Full of Faith,
Ahsante nilishapata ushauri,
Ila kama bado unaushauri mwingine ni vizuri sana, ushauri niliokuwa nahitaji ni ,

1, je huyu mwanamke ana haki zozote kuhusu mali yangu?

2, je akirudi na kusema kuwa pale ndio kwake na akanifanyia fujo nikimfukuza nitakuwa natenda kosa?, kumbuka nimeishaenda polisi kutoa taarifa 3

3, hayo mawili ndio ulikuwa msingi hasa wa kuomba ushauri wenu,

KUMBUKA SIJAWAHI KUFUNGA NDOA NAYE,
NA MIMI NINA MKE WA NDOA YA KANSANI

lakini la mwisho ambalo sijaona ushauri wenu ni je,

WATOTO WANA HAKI YA KUSIMAMISHA NYUMBA ISIUZWE?

Ni hayo tu ndugu yangu.
Ndugu ingekua wewe ndyo umemuacha ningemtetea lakini kwakua yeye ndye kalikoroga mwache alinywe hiyo nyumba ina jina lako pangisha au endeleza ila kama ataleta usumbufu badili jina weka la bi mkubwa piga bei hatokua na haki tena na kuhusu watoto uliozaa naye uliwasomesha na wao wanampenda mama syo wewe achana nao watatengeneza future yao kupitia elimu uliyowapa,usimhurumie mtu uliyemtoa shimoni harafu anakuzarau
 
Ww mbona unanyoshewa kidole na kila mtu ,acha kufatilia uzi wa watu bidada
Ndugu ingekua wewe ndyo umemuacha ningemtetea lakini kwakua yeye ndye kalikoroga mwache alinywe hiyo nyumba ina jina lako pangisha au endeleza ila kama ataleta usumbufu badili jina weka la bi mkubwa piga bei hatokua na haki tena na kuhusu watoto uliozaa naye uliwasomesha na wao wanampenda mama syo wewe achana nao watatengeneza future yao kupitia elimu uliyowapa,usimhurumie mtu uliyemtoa shimoni harafu anakuzarau
Love you,
Ahsante sana kwa ushauri, kusema ukweli, namshukuru sana Mungu kwa wazo alilonipa kuomba ushauri humu JF , nimefarijika hasa na nimepata uwezo mpana sana wa kutafakari mambo, nadhani uwezo wangu wa kutafakari mambo ulikuwa mdogo, lakini sasa hivi najiona nina nguvu ya kutoa uamuzi bila wasiwasi,

Nakumbuka mala ya kwanza alipoondoka kama ningepata hili wazo la kuomba ushauri humu, ningekuwa nimeshamsahau, na asngeniumiza kiasi kile,

Ahsante sana
 
Mkuu tuko pa 1.
Miaka hii imeibuka tamaa mioñgoni mwa wanawake inayopelekea mahusiano meñgi kuvunjika, hata mimi niliachwa na mwenzangu ña watoto leo baada ya miaka 3 eti anasema añawataka watoto, nawasomesha shule nzuri but wanawake wamrudieni Mungu
 
Da , pole sana ndugu yangu, huwa inafika wakati naona dunia ya leo neno ndoa halipo, sema tu sisi wanaume tumeumbwa na roho ya uvumilivu sana ndio maana tunaweza kuishi na hawa viumbe,

Ila na sisi wanaume tuna tatizo kubwa maana sisi ndio huwadanganya hawa viumbe,

Hebu niambie huyo mkeo sasa hivi ana maisha gani huko, alishaolewa na je umeweza kumsahau?
 
Back
Top Bottom