Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Sasa baada ya kupokea lile fungu la kwanza
30m, mimi haraka sana nikaenda kupunguza madeni yangu, hata hivyo Hays kwisha,

Na yeye nikamwita kwamba tukae chini ili ile 15m yake tuipangie matumizi ya kwanza kabisa,

Ushauri wangu ilikuwa tununue kiwanja kwanza,

Sehemu ambayo sio ghari sana,
Hapo sasa ndio kimbembe kilipoanza,

Ila kufupisha story nilimwambia basi wewe unataka tuanze na nini? Akanijibu hiyo pesa anataka afanyie biashara wakati ujenzi unaendelea, nikamwambia biashara mbona tumefanya na tunasnguka, hata hivvyo sio mbaya wewe kutaka kufanya biashara lakini ni bora tuwe na kiwanja kwanza,

Kusema kweli zogo lilikuwa kubwa ananipayukia na mimi natumia ubaba wangu sasa kulazimisha, ndio alipoamka kwenye kiti(tulikuwa tumekaa nje na watoto wanacheza hapo nje)

Alichoniambiakwa sauti kuu na kali ni kwamba

TOKA HAPA NA VISENTI VYAKO UNAVYONIPAGA,

Du ! Leo naambiwa visenti, yaani huyu mwanamke nimekopa pesa, nimempeleka ufundi cherehani, nimemfungulia saloon , grocer, mghahawa, dala dala, mtaji wa kuku wa kisasa,

Anaanguka namyanyua, anakopa vicoba anashindwa kumaliza nammalzia,

Nalipa watoto karo kwa mwaka jaribia Mil 6 na bado watoto ndio kwanza wanasafari, kwa nini ananivunjia heshima namna hii?

Kusema kweli sikujua kama niliokota jiwe au mti au ufagio, nimpige nao akawahi kukimbia, na mimi nikaanza kumfukuza, kama sijamrushia kila kitu ambacho mpaka leo sikijui, nikaanguka chini, yeye akaendelea sijui wapi , kusema kweli sikumwona,
Kuangalia nyuma naona watoto, kumbe na wenyewe wakawa wameshika mawe wanataka kunipigia nayo, nikaamka ili niwafukuze nikaenda chini tena , sasa hapo ndio nikaanza kusikia maumivu, na watoto wale kule wamesimama, sasa na wenyewe wanapaza sauti,
KWA NINI UNAMPIGA MAMA YETU SI UENDE KWENU!!!!!

Nitaendelea
Hapa ndo michepuko wananikomesheaga watu🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Tulia uandike story nzima....,Japo story yako ni somo kwa vijana inaboa sababu ya vipande vipande...
 
Mzee umesema ukistaafu una Kama 250m? Naomba nikufariji pindi utakapostaafu umehangaika Sana na majukum ya hapa na pale unahitaji kutulia Sasa na kula mema ya nchi...mi sihitaji kuzaa ucjal

[emoji23][emoji23], baba bado ana mitihani inamuwinda.
 
Ukirudi uje na majibu ya maswali hay, unajua stori nzima tangu umeanza unamuongelea sana huyo mchepuko, sijui ni muda gani ulikua unatumia na mkeo, mkuu hiyo ni laana na ndiyo maana unapitia mengi mabaya, mkeo hakustahili haya, kama ukitaka mke mdogo ungemtambulisha mkeo, haya ni mambo ya karma malipo ni hapa hapa duniani
Usimuhukumu kwanza ngoja amalize kwanza
 
Ila mzee fanya umalize ...unatuletea kiduchu duchu stimu inakata...wengine kurudi Rudi kwenye nyuzi Mara kumikumi mtihani..tuonee huruma
 
Ukirudi uje na majibu ya maswali hay, unajua stori nzima tangu umeanza unamuongelea sana huyo mchepuko, sijui ni muda gani ulikua unatumia na mkeo, mkuu hiyo ni laana na ndiyo maana unapitia mengi mabaya, mkeo hakustahili haya, kama ukitaka mke mdogo ungemtambulisha mkeo, haya ni mambo ya karma malipo ni hapa hapa duniani
Kina pilato Sasa😀😀
 
Mtake radhi baba wa watu.. huyo mwanamke wa pili kamchukulia Kama mke kwake na si mchepuko
Hawezi kuwa mke mdogo ilihali hajamtambulisha kwa mke wake, atabaki kuwa mchepuko, ukweli unauma acha nimkandamizie moto humo humo,
 
Kina pilato Sasa[emoji3][emoji3]
Mchepuko kasha sepa na kibunda cha pesa [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] nyie watu,

ila usikubali kamwe kuishi maisha ya nyumba ndogo hakuna faida zaidi ya kumuumiza mwanamke mwenzako na kuishi kwa kujificha ,umenipa na jina kabisa upilato
 
Mchepuko kasha sepa na kibunda cha pesa [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] nyie watu,

ila usikubali kamwe kuishi maisha ya nyumba ndogo hakuna faida zaidi ya kumuumiza mwanamke mwenzako na kuishi kwa kujificha ,umenipa na jina kabisa upilato
Acha avune alichopanda
 
So sad nimeshuhudia shemeji yangu mkubwa yaani alikuwa na wake 3 lakini uzeeni ni kama hakuwahi zaa wala kuoa. Sasa hivi wadogo zake ndio wanamtunza watoto wana kazi ya kuangalia mama zao tu. Wale wa ni mkubwa wanasema baba yao aliwa neglect wakiwa wachanga sana wakalelewa na mama yao hii ni kweli. Wale wa mke wa pili wanasema baba yao alimpenda mke wa Tatu kwa hiyo hao watoto wa mke wa Tatu ndio watunze baba yao kwa kuwa wao ndio walifaidi pesa zake. Bi mkubwa yuko zake Canada ana kula raha na wanae.
Mungu wangu,
Mengine wala si ya kucheka,
Ngoja nipaze sauti.

WANAUME TUANZE KUJIONEA HURUMA KWANZA SISI WENYEWE NA MENGINE BAADAYE, HALAFU TUWAPENDE SANA NDUGU ZETUWA KUZALIWA,HAO WATAKUFANA SISI,

KUSOMESHA WATOTO SAWA LAKINI USIJIUMIZE FANYA KWA KIASI ,

ANGALIA SANA FUTURE YAKO MWENYEWE KWANZA BAADAYE HUKO MBELE ITABIDI UJITUNZE MWENYEWE
 
Mama mjengo umenipotea wewe, ila ukweli mama mjengo katika vitu navichukia ni michepuko, yani michepuko inapoteza sana ramani ya familia, stress, zinaongeza chuki ndani ya familia yako, ugomvi na mpasuko ndani ya familia yako, halafu pia bado nae lazima awe na mtu wake sasa yani ni mkanganyiko
Lakini usisahau ndio sehemu ya maisha, mwanaume anacyotakiwa kuishi, hiyo ipo toka dunia inaanza, na usisahau binadamu ni mnyama, tunajifaragua tu, tabia zote za wanyama tunazo, kwa hiyo ukiona wanyama wana wake wengi na sisi ndio ilitakiwa tuwe hivyo.
 
Back
Top Bottom