Raynavero
JF-Expert Member
- Apr 29, 2014
- 38,378
- 56,047
Hapo ulipoenda kwao na kuchinjiwa mbuzi ndio ulitambulishwa rasmi kama Mme. PoleNILIVOMPATA!
Alikuja mjini DAR akiwa binti mdogo tu na karembo kweli kweli, nikimkuta kwa shemeji yangu mke wa wa rafiki yangu wa kazini.
Baada ya kutoka kazini huyu rafiki yangu aliniambia nimpitishe kwako kuna kitu anachukua halafu tuendelee na mishe zetu, mimi nilikuwa na kagari kangu yeye hana, na mara nyingi alikuwa anapenda kunitumia mimi, na Vibia nikawa navipata vya bure, sasa baada ya kufika kwake shemeji akawa katoka na funguo, ikabidi tumsubiri kwa muda, alipofika hata plan yetu ya kutoka tena ikawa imeishia hapo.
Lakini alikuja na hako kabinti, sasa kukaa tena nyumbani rafiki yangu akaona hapana, akatukaribisha wote kwenye glocery ya karibu na nyumbani, tukanywa pale binti alikuwa hanywi baadaye naye akaanza kidogo kidogo, muda ukaenda na miadi ikaianzia hapo.
Amesoma kiasi, siku hiyo sikuuliza, kaja Dar kufanya nini, nikapewa jibu.
Basi weekend iliyofuata tukakutana na kuelewana zaidi kwenye bar fulani hivi. Na mahusiano yakaanzia hapo!
Mara nikasikia kakorofishana na yule shemeji yangu, na kaamua kupanga chumba chake maeneo ya huko uswahilini. Akanikaribisha, nikamuuliza utawezaje kuishi mwenyewe binti mdogo hivi? Akasema atajua.
Basi nikaona mara akajiunga na wadada fulani hivi kwenda viwanja kufanya vibarua.
Kipindi ameshajua nafanya kazi wapi, sasa kila baada ya siku mbili au tatu nikawa namtembelea kwake, lakini mazingira ya pale kwake yalikuwa hayanifurahishi, kwa sababu kwanza nilimkuta analala chini kwenye mkeka na kagodoro kikuu kuu hivi na jiko la mchina na madumu dumu ya maji.
Kwa kifupi ni kisera sana, sasa kusema kweli niliingiwa na huruma tu, nikamnunulia baadhi ya fanicha, kwa sababu nilimwona kabisa huyu ndio kaamua kuja Dar.
Nilipojitahidi kujiondoa kwenye huo uhusiano kwa kumweleza nina mke, hakutaka kunielewa, nikizidisha siku bila kwenda kumwona nashtukia kaja ofisini. Nikaendelea kununua vitu vyake vya matumizi mpaka chumba kikajaa. Sasa na mimi mdogo mdogo nikawa najisahau nalala kule, lakini mara ya kwanza kabisa kulala kwake alinichezea mchezo, tulipotoka kupata kinywaji nikapitia kwake kidogo, sasa ule uchovu mara kausingizi kakanipitia, hakuniamsha ng’oo kwamba niende nyumbani, kaja kuniamsha karibia kunakucha niende kazini!
Ndio kwa mara ya kwanza nikawa nimelala nje! Nilimwelezaje mke wangu, hiyo ni story ninyingine tuiache.
Sasa mwaka umepita nimenogewa mtoto wa watu ana ujauzito wangu.
Mungu wangu sasa mimi nifanyeje, mume wa mtu tena wa ndoa. Kusema ukweli nilichanganyikiwa, lakini hata hivyo nilikuwa nategemea nini?
Basi baada ya muda akaenda kwao kujifungua na akajifungua salama, nikaenda kumtembelea na kuona wazee. Na nilienda kwa gari langu na rafiki mwingine. Tukalala pale asubuhi nikaona tunachinjiwa mbuzi. Tukala na majirani na ndugu kama 16 hivi walikuwepo, kusema kweli sasa dalili zote kwamba mimi ni mkwe tena wa heshima niliziona pale, ilipofika jioni tukaondoka kwenda kulala mjini yeye bado tukamwacha pale na mtoto wake
Sent using Jamii Forums mobile app