Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Kuna kitu cha kujifunza kwa sisi wanaume.

Japokuwa wanaume wa sampuli hii wapo, Ila mtoa mada umekuwa udhaifu sana.
Labda kama limbwata lilihusika.
 
Afiche kwa sababu gani,huyu bwana uandishi wake hauna mtiririko mzuri sana kitu ambacho simshangai kwa kuwa hatungi kitabu. Inavyoonekana Bi mkubwa hambani sana,na pia kazi ya jamaa inamfanya anaweza kumpanga Bi mkubwa kuwa anatoka kikazi ila anakuwa na mishe zake. Hilo la kazi amezungumzia kwenye uzi huko juu
Sawa unaweza kusema kazi inamsaidia kupanga namna ya kuhudhuria kwa mchepuko

Lakini hiyo inawezekana kwa wanaotoka point A na kwenda point B tuu, yaani unatoka kwako unaenda nyumbani kwa mwanamke au guest/Lodge/Hotel sio utaratibu rafikir kwa anayetoka anakwenda kwa mwanamke anayeishi nae kama mke yaani wanatoka, wanazurura, wanafanya shopping, wanakwenda site nk kwani huko mabarabarani hakuna watu wanaomjua wakafikisha taarifa nyumba kubwa?

Ndio shida ya kuficha ficha mambo lazima uache maswali
 
Mkuu tuliza akili hapo anamuongelea mke mkubwa wapo wote nyumbani lkn watoto toka wapate kazi yeye wamempa 120000 tu ila mama yao kila siku anabadili nguo kwa pesa za watoto.
Sio kweli kuna mahali anasema watoto wake mpaka sasa wamemtumia 120000 tu lakini mkewe anasikia tu mara nguo mpya mara nini
 
Ahsante,
Tatizo nalo wapambe, maana ukishatangaza tu
Nauza wapambe hawa hapa, mala nyumba ina mgogoro mala nini, maana uuzaji wa nyumba ni mgumu, bora uuze gari
Najiuliza tu, unaweza mpangisha mtu afu ukaogopa kumpa notes ya kutoka????
 
Lakini unanichamba bure kabisa, tena kwa kuziamini hisia zako,
Umekasirika sana kwa kitu ambacho sio kweli kabisa

1,mimi sikuwahi kumuacha mke wangu hata kidogo,
2. Mimi sijawahi kugombana na mke wangu kiasi hata cha kukataliana tendo la ndoa
3.haya amekuja kuyajua kwa uhakika zaidi watoto wakiwa form na std 7
4 ukiangalia miaka hiyo ndio kipindi nimeanza kusumbuliwa huko nje,kwa hiyo ndio upendo ulizidi sana kwa bi mkubwa
5. Watoto kunitumia hiyo laki, kwanza huwa najiuliza wanitumie zaidi ili nifanyie nini
Mimi nina pesa yangu, viwanja natoka na mama, na anachangia kununua kinywaji ingawa mimi sio mywaji sana, bia mbili tu chali,

Najua wanamtumia mama yao, na uzuri wakati mwingine akitumiwa ananiambia,

Na akisha tumiwa nitaona nguo mpya hapo
Na mwenyewe anafurahi na mimi natafurahi kumwona mke wangu kapendeza na anakuwa kijana zaidi

Sijawahi kununua boxer wala fulana za ndani, vyote nashtukia zipo kabatini, na zile za zamani anatupa, tena wakati nakasirika anatupa zikiwa bado nzuri kabisa

Kiujumla hajawahi nichukia wala sijawahi mchukia
Turudi kwa watoto kutonitumia pesa, walishaona sizishobokei pesa zao, kwa sababu hawajui wanitumie kiasi gani ili nilizika, mimi nina pesa yangu ya kunitosha
Lakini wakati mwingine wadogo wanawapiga mizinga huko, unaona tu dogo karudi nyumbani na shati jipya , hapo si wanakuwa wamesaidia,

Mimi ninachohitaji kwao ni usafiri tu, na wameshaniahidi kunako majaliwa kama hawajajenga wanisuprise na usafiri,

Kwa hayo machache kuwa na amani tu
Ukiona mtu anaeleza sana asivyo na shida ujue kuna walakini

Nguvu kubwa inatumika kupaka rangi hali ya nyumba kubwa

Mtu mwenye nafasi hii anawezaje kucharuana na malaya(samahani) hadharani mpaka watu wanatoka kuchungulia, mpaka uongozi wa mtaa unawachoka?

Ni uongo, na kama ni kweli kuna nati haijakaa sawa upstair
 
Mkuu una familia nzuri sana zaidi ya watu wanavyofikiri. Uzuri umejitoa sana kwao,Mungu akusaidie umalizana na huyo Bi mdogo salama,kitu ambacho kiko wazi utashinda hiyo vita kwani umeshikilia mpini
Unajijibu sio[emoji1][emoji1]
 
Baki na hati ya nyumba...mtafute wakili wako asimamie hili kua nyumba haita kaa iuzwe ni ya watoto...waachie watoto nyumba kiroho safi tena mkabidhi mama yao watoto wakiwepo na wakili pia awepo...baada ya hapo endelea kusomesha wanao...huyo mwanamke vunja nae mawasiliano ya kimapenzi kabisa...yabaki mawasiliano ya kuhusu kulea watoto....usitake kujua anatoka na nani au ataishi na nani kwani umesha amua kuachana nae...nyumba ibaki kua yako ila wanao waishi hapo...hebu fanya hivyo.
Ushauri mzuri sana
 
Mkuu tuliza akili hapo anamuongelea mke mkubwa wapo wote nyumbani lkn watoto toka wapate kazi yeye wamempa 120000 tu ila mama yao kila siku anabadili nguo kwa pesa za watoto.
Uwe unasoma story katikati ya mistari
 
King,
Nimeshazungumza kuhusu bi mkubwa, ni kweli baadaye sana alifahamu,
Tokea mwanzo nilisema huu uzi sitaki sana kumzungumzia,
Shabaha ya uzi ni bi mdogo, sasa nimejikuta nalazimishwa mpaka kufahamu mambo ya bi mkubwa,

Kiufupi hana tatizo na mimi, sasa kama ananichekea mdomoni tu mimi sijui
Kama ananitegea kunifanyia kitu mbaya, vile vile sijui, siwezi kuingia kwenye moyo wake

Nachoona tupo happy tu
Ameshakubali hali halisi tunaishi,
Hakuna anachokosa yetu uzima I mwake

Kama mnataka nifunguke zaidi kuhusu bi mdogo nitaendelea kadri nitakapokuwa nakumbuka mambo ya ovyozaidi

Kwa taarifa bado sijafunguka kuhusu vikao zaidi ya 8 tulivyokuwa tunaitisha, alikuwa anazungumza nini

Kwa nini alianza kuniita huyu hataki wageni

Majirani na marafiki zake walikuwa na tabia gani, na nini kiliwapa

Polisi.ustawi wa jamii, mahakama, ofisi za kata

Pote huko walikuwa Na mchango gani kuokoa huu uhusiano Na nini udhaifu mkubwa kabisa upo huko hapana nikashangaa hivi kweli wapo serious kabisa na matatizo ya watu au wapo kwa ajili ya kupiga soga tu, na kutaka kujua matatizo ya watu kiumbea

Mama ni mengi,
Na mwisho kwa ajili ya kumbukumbu zangu za baadaye, haya ni maandishi ambayo itabidi niyahifadhi kitaalaam ili niweze kutumia baadaye

Hasa tukifikia kipindi cha kupelekana mbele zaidi,

Ninachoshukuru kila tunapoendelea na michango na maswali, nashangaa nakumbuka mambo ambayo nilishayapotezea, Ahsante sana

Ila kumbukeni tu,

HII NI TRUE STORY
SIO TAMTHILIA

hata mimi kuna kipindi ninapokuwa mwenyewe nikifikiria haya matukio, iwe kwenye usafiri, ofisini, chooni, naoga, huwa nacheka sana,

Maana huo siamini kama haya mambo yanaweza kunitokea mimi na nikaendelea kuishi

Watu wengi sana wameshajiua kwa maana kama kama haya
Mwitore kaka you are very strong.Hao wanaokukejeli hawajui maisha,wanatakiwa wajifunzr.
Vijana wengi wanaishi kwa mijimama au nyumbani kwao,wanatarajia wakiwa na miaka 40 wawe na majumba.
Wadada wengi humu wamezalishwa wanalea watoto peke yao kwa sababu ya viburi,dharau na kejeli.They have lost focus ya maisha.Hawaoni mwanga wowote mbele kaz yao nikukukatisha tamaa.
Makundi hayo achana nayo ukiweza usiwajibu.Masna hujaja,hapa kushindana wao wanataka mshindane.Ukifuatilia wanakuita muongo,mjinga mpumbavu unapaswa kuwaacha watuelezee wao ukweli na mpaka namba ya kiwanja wanakijua kwa ujuaj wao.
 
Kama ulisha invest kule kama mimi nilivyoinvest ingukuwa wewe ungefanyaje?
Halafu kumbuka serikali ipo na sheria zipo!
Umeinvest km mke ama km mchepuko! We no boya ata aliyokufanyia ni kidogo sana subiri jamaa ake aje akuue ukose vyote
 
Kuhusu single mom.. kuna wanaowasema vibaya hapo juu. Haihusiani na mada yako

Pili... naomba tena uelewe... HUJAWAHI KUPENDWA NA HUYO MALAYA. Kwanini hutaki kukubali? Yaani mimi mwanamke nakuambia ukweli halafu unakataa? Umewahi ona wapi MCHEPUKO akampenda mume wa mtu mapenz ya kufa kuzikana pasipo mali? Yaan from nowhere tuu eti hina maisha, huna mbele wala nyuma halaf eti mwanamke akubali kuwa spare wakati anajua kina mainchick? Tena achilia ndoa tu. Tukiwa wapenzi na nikajua kuna main basi jua nakuigizia. Huo ndo uhalisia. Ameanza kubadilika BAADA YA KUPATA ALICHOKITAKA. hakuna cha mashost wala nini. Tena lishamba kweli. Cheap kabisa.

Kwa nyumba uza kabisa nakusupport... hii hela tia kwenye akaunt ya mkeo yote halafu wewe ndo ufate nyuma. Acha huu ujinga. Hapa hakuna complications zozote. Hakuna mapenz yoyote hapo.

Ila kila nikiimagine jinsi hilo limchepuko lilivyo lishamba nashindwa kbs kutamatisha... unayo makosa yako na mchepuko unayo yake kuingilia maboma ya watu. Nachosema ashukuru tu me si nduguyo. Ningekabamizaaaaaa...
Mungu azidi mbariki Mother house...
Upo vizuri
 
Kuchambwa lazima. Muhimu mnooo... maana unafanywa zoba.

Naomba nikuambie... acha kbs kujisemea eti una hela nyingi... hakuna kitu kitamu kama cha kupewa mzee wangu. Baba yangu ana jimudu vyema. Lakini vile vidogo nampatiaaa.... heheheeee yaanii anaona rahaaa. Usituongopee hapa. Yaan hakuna kitu raha kama kutunzwa. Yaan mashati alonunua babangu ameyatelekeza anavaa yangu. Na anasema malaika wangu ameninunulia haya ili nivae. Na yamepauka anayapenda balaa. Wewe hutaki hizo raha? Hakuna kitu kibaya kama kutengwa na familia. We rudi tu kwa mkeo ndo la msingi. Yaan rudi. Mwanao hata akakupa elf 10 ni tamu sana. Hela yako mwenyewe haina mzuka kama ya wale ambao wanakijali wewe na unawajali... rudi kundini.
Nimekupenda bure pendo kwa kuwa hujaegemea upande mmoja, ushauri uliotoa kwa huyo mzee baba lazima auzingatie, vinginevyo itakuwa sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Hakika sikio la kufa halisikii dawa
 
Back
Top Bottom