Na hapo uliposema Mungu akakuchukua ndipo pa kuangalia sana,
Maana hilo nimelpata wiki iliyopita tu mahakamani,
Ilikuwa hivi, yeye alitaka kuingiza mambo ya watoto kwenye hii kesi, hasa hasa kuwa mali au nyumba ni ya watoto,
Hakimu akamwambia watoto hawahusiki, watahusika tu kama shauri kingekuwa ni mirathi.,
Sasa hapo maana yake ni nini, siku umeondoka duniani hawa watoto wanaweza kutumiwa na ni mdogo kuja kudai mali ya urithi ya ni mkubwa, kwa hiyo mali zako zote ziuzwe au la mali ulizodhani umemwachia ni mkubwa na watoto wa ni mkubwa watakuja kushtukia wanaitwa mahakamani na watoto wa ni mdogo wapate urithi wao,,
Sasa kama hata wenyewe uliwajengea huko wanaona ni mkubwa kaachiwa maghorofa watakuja kuyadai vile vile, maana kumbe wanahaki hiyo,
Lakini kingine ni nini, huyu bi mdogo anaweza hata kukuondoa duniani kwa njia zake, ili ifunguliwe kesi watoto wapewe chao mapema kama ataona bado unang’ang’ania kuishi tu.
Mambo ni mengi lakini tuwe makini sana