Naomba ushauri: Mpenzi wangu ana tabia ya uongo

sam green

Senior Member
Joined
Feb 21, 2020
Posts
184
Reaction score
274
Habari kaka zangu na dada zangu katika jukwaa hili,

Nahtaji ushauri, nimekuwa na mpenzi wangu ambaye mara nyingi anakuwa muongo sana hataki kuweka mambo yake wazi, japo sio sana. Sasa hili ndio babu kubwa, kuna siku amepata safari walisafiri na dada yake. Siku hiyo alioamba nauli tulikwazana sikumpa wakasafari alivyofika kule nikamtafuta nikamuuliza akasema nauli amekopewa na dada yake, kwahiyo ana mdai.

Ilivyofika siku ya kurudi nikatuma nauli ya kwake na ya kumlipa dada yake hatimaye wakarudi lakini akatuma sms eti usimwambie dada kama umenitumia hela, nkapgwa na butwaa ikabidi nimtafute dada yake na kumueleza yaliyopo dada yake akaniambia siku ya safari ya kuenda hawakutumia nauli walipanda gari la kanisa bure ila nauli walitoa wakati wa kurudi na hakumpa hela dada yake alitoa ya kwake tu

Ni hayo machache japo yapo na mengine, mnanishauri nin? Juu ya hili nataka kumuacha lakini nikikumbuka tumetoka mbali sana mpaka tumefka hapa. Nina miaka miwili kwenye mahusiano mpaka sasa

NB: Nilipanga aje kuwa mke wangu hapo baadaye lakini tabia yake ya kutokuwa muwazi ina kera mara kadhaa nimemwambia ajitahidi asiwe ana danganya lakini bado.
 
Ushafanya maamuzi unayoyajua, unachokitaka ni justification tu.
 
Kuishi na mtu muongo & mlaghai unahitaji busara ya hali ya juu..!

Huwa sipendi watu wa aina hii na sijui kwanini, na nikigundua kuwa huyu ni mbabaishaji nakata mizizi haraka sana.

Mkuu inatakiwa ujipange haswa uangalie kwa jicho la kiume kama huyo mpenzi wako ana faida kwako au la.. maana sisi watafuta maisha tunahitaji mke ambae yupo makini kwenye ushauri, mwenye fikra chanya, awe na wivu na mali yako na asipende anasa.

Jaribu kuchunguza kwanza, uangalie kama ukimuweka ndani atakusaidia vipi kupigana na changamoto za maisha, epuka kuoa tapeli wa mapenzi, kitega uchumi (yeye anavuna kwako tu).
Yangu ni hayo..!

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Uongo ni tabia,na wala usifikiri kuwa kwa kumuonya au kumkaripia ataacha tabia hiyo,kama kweli unampenda ili awe wako wa maisha,fanya maombi maalumu Mungu aweze kumbadilisha,kinyume cha hapo usitegmee muujiza...
 
Shukran saana kwa ushauri
 
Toa mali,ingiza mali
 
Bado Inaonekana hujakomaa kwenye mahusiano mkuu....relax
 
Hizi kesi mpeleke kwa washenga au wazazi
Sasa Sisi hapa tufanyeje??
 
Uzinzi na umalaya ni kipaji kama ilivo kucheza mpira au basket ball na inaonekana mapema kama vipaji vingine tu toka udogoni ndio maana mkiambiwa mchague wa kuzaa naye mnakuwa na jazba na hasira,serikali hawezi kuingilia vipaji vya watu its in human nature.

WHERE THERE IS A WHEEL, THERE IS A WAY!!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ukimuona mtu muongo, awe mume au mke, awe boyfriend au girlfriend basi tambua unaibiwa wa maneno na vitendo.

Na ndiyo maana malaya wote ni waongo waongo na rafiki ya uongo ni wizi. Kwa kifupi mtu muongo ni malaya na mwizi
 
Kaka UNALIWA. umepanga kuoa.. mwenzako anakuona mobile atm
 
Nashauri zungumza nae tararibu tena, ila wakati huu mpe na vifungu vya biblia....
 
Kwa kisa hicho naona ni utoto tu wamsumbua akishajua kujitafutia kwa jasho lake hutosikia hizo story.....

Labda kama kuna mengine makubwa zaidi ya hiyo story.
 
Mlikwazana ukagoma kutoa nauli maana yake hata hiyo safari hukuiafiki, mwinzio katumia mbinu zake kaenda hiyo safari ulipo mtafuta kakwambia nauli alikopa, kirahisi tu ukatuma nauli ya kurudi ukalipa na deni, huenda ulituma na yakutolea..!!

Hapa panaonesha udhaifu wako, unaweza kuamua jambo ila huwezi kulisimamia, alipaswa kukopa na yakurudia maana hiyo safari kajiamulia mwenyewe.

Kukudanganya kuwa amekopa na hajakopa maana yake alikuwa na shida na pesa, hata ukija muuliza kwanini uliongopa atakwambia alikuwa na shida ya pesa, je Hiyo shida hakuwahi kukwambia kabla? ulitatuwa au ulizinguwa!!

Inawezekana wewe kutoa pesa mpaka uongopewe hivihivi hutoi, kama ni hivyo badirika.
Unachoweza kufanya Kwa ajili yake fanya as long as kipo ndani ya uwezo wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…