Naomba Ushauri: Mwanamke wangu ananiambia mtoto si wangu

Sawa ndugu
 
Kote uko anatmia majina yangu ndio af wendawazimu inawezekana maana ata mi simuelew kawaje
kwani aliwahi kuwa tofauti?
Unajua huwa mnapambana na wishes na uhalisia!
Unampenda huyo mwanamke bado na unatamani sana angekuwa tofuati na alivyo!
Lakini huyo ndiye yeye.
Sasa acha kujitesa na mtu unaona kabisa hata waliodhani wewe umekosea nao wamejikuta pale pale!.

KASEMA MTOTO SIO WAKO, MWAMINI! endelea na mengine!
 
Dna ya nn demi? Kama sio wako na hakukwambia acha maisha yaendelee what if ww baba angepima dna na kukuta ww sio mwanae?
Kuna ambao wanahisi watoto sio wao lakini hawana la kufanya. Mwanamke akikwambia kwamba huyu mtoto sio wako hapo ni 50/50 chance.
Mtoto ana haki ya kumjua baba yake halisi hata kama kuna baba mwingine anamlea.
 
Nimekupata vilivyo kaka ahsante sana
 
Amina kaka ahsante sana
 
Ukweli ni kwamba wanaume wengi wanalea watoto sio wa kwao bila kujua. Ningeshauri serikali ya Tanzania iweke mazingira rafiki ya uwazi na ukweli ili watu waweze kupima DNA muda wowote wanapohitaji.
Sawa maadam ahsante
 
Mwanamke anasemaga ukweli akiwa na hasira au amelewa zingatia hilo ili ukae mbali na stress.

Zingatia Jogoo hatunzi kifaranga
 
Wenzio wanabambiwa watoto we unaambiwa si wako, huoni kuwa mke wako anakupunguzia majukumu ya kutunza mtoto? Hebu jiridhishe kama si wako kweli, kapime DNA
 
Msikilize mbeba mzigo,yeye ndo anajua ulikua mzito ama mwepesi na aliutoa wapi,
 
Pole mkuu,ila mtoto kweli sio wako ameshasema wewe fanya maamuzi
 
Kwangu hio ingekua imeisha.

Kwani ndio mtoto wako wa ngamia mpaka umng'ang'anie mkuu.

Ukishupaza shingo Yako iyo. Atakua anatumia kama silaha ya kukuchapia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…