Naomba Ushauri: Mwanamke wangu ananiambia mtoto si wangu

Naomba Ushauri: Mwanamke wangu ananiambia mtoto si wangu

Joined
Sep 1, 2025
Posts
45
Reaction score
44
BINTI YANGU

Tafadhari ukimaliza kusoma naomba ushauri wako

Stori inaanzia 2020 mwezi wa saba tulishindwa kuishi pamoja na suluhu ikakosekana tukaachana kwa fujo nyingi kwake yeye mwanamke mixer kunitukania wazazi na kunitishia laana ya mahusiano.as a men niliamua kumuachia kila kitu tulichokua nacho vitu vya ndani japo havikua na thaman kubwa sana ila vilitoshea kugawana au hata kuvichukua vyote kwa7babu nilimtolea mpaka mahali kwao niliamua kuacha yote ayo ili nibaki na aman tu.

Kipindi chote hicho alikua hajajigundua kumbe alikua na mimba changa ambayo ndio mtoto wangu wa pili.Baada ya mwezi mmoja na kama wiki 2 kupita alinipigia simu akanambia yeye ni mjamzito na io mimba ni yangu🙆‍♂️,kiukwel ilikua ngum sana kuikubali kutokana na jinsi tulivyoachana maana nilikua nampigia mpaka sim nimjulie hali before {mazoea} lakini aliishia kunitukana na kupiga sim kwa wazaz wangu kua mwambieni mtoto wenu asinisumbue kwani tumeshaachana.

Nilikataa kua sio mimba yangu lakini wazazi ndugu na watu wangu wa karibu wakanishauri kua ingekua kweli sio mimba yangu na kwa namna tulivoachana basi asingekua na sabab ya kuniambia kua ni ujauzito wangu ivo nisikatae damu.

Nikakubali nikalea mimba matumizi yote nikazingatia akajifungua kwa shida kidogo kwasabab alikua mbali na kituo cha afya kukodi gari na nn gharama zote izo nilimaliza mwenyew

Malezi yakaendelea ile mtoto anaumwa sijui nguo viatu nilizingatia hata kipindi anamuachisha alimleta nyumbani kwa baba yangu akamuachishia kwetu,kidini mtoto akabatizwa kwa jina langu pia.mtoto akaendelea kukua akiwa mbali na mimi baba.Yule dada akapata mwanaume mwingine akaolewa akazaa nae mtoto mmoja wakashindwana na yule mwanaume nae pia wakaachana.

TATIZO
Kilichonifanya niweke shauri hili nikitaka msaada wa ushauri hata sheria ama busara kwenu ni kwamba ilitoke mtafaluko kidogo mimi na uyo dada kuhusu mtoto alinipigia simu kua anaumwa na yeye hayupo nyumbani kasafiri na aliowaachia mtoto hawawezi kumpeleka hospital yaani anakokaa yeye mpaka hospital ni kama km 6 ivi na nilipo mimi mpaka kufika kule ni kama km 25.

Kwa jicho la kibinadam nilifanya makosa kweli kutokwenda kwa7b za kawaida tu.yote kwa yote homa ya kawaida mtoto alitibiwa na akapona,lakini mamake alikasilika sana kias kwamba hakutaka kusikia chochote kutoka kwangu.

Kwa kutambua kosa langu nikajishusha nikamuomba msamaha sana akanielewa lakina akaniambia kua nanukuu!

Yameisha lakini"Leo acha tu nikwambie ukweli huyu mtoto sio mwanao".

Nikajua kua labda tu ni hasira zikiisha atasema ukweli lakini ni yuko tu serious kua mimi sio baba wa uyo mtoto na anauthibitisho

Nifanyeje
 
Nyie Bado mnapendana, afu Bado hamjakomaa kwenye, game ya ndowa,
Sasa mmeshatengana na umeambiwa mtoto sio wako ss unatakaje? SI uendelee na maisha yako?
Ushauri jibebishe, akiingia kwenye mfumo mjaze mimba! Japo hapo 💯 Bado mnapendana!
Sio kwel mimi nina maisha yangu mengine na nishaoa mwanamke mwingine kinachoniuma nimesumbuka sana kumlea uyo binti af saiv kirahis tu sio mwanangu kvp an
 
Sio kwel mimi nina maisha yangu mengine na nishaoa mwanamke mwingine kinachoniuma nimesumbuka sana kumlea uyo binti af saiv kirahis tu sio mwanangu kvp an
Umesumbuka kweli kumlea Binti ila Bado ujawekeza muda mwingi na pesa nyingi kama wengine wanaokuja kushtuka mtoto sio wake ameshamsomesha mpaka chuo huko na ajira mtoto ameshapata

Kwahiyo kuachana na huyo mtoto ni jambo sahihi na rahisi kwako kwa wakati uliopo ufate maisha yako na upambane kwaajili ya watoto wako wengine
 
Eephiwww!!!
FB_IMG_1739301569383.jpg

Nipumue kwanza,nitarudi kushauri.
 
Umesumbuka kweli kumlea Binti ila Bado ujawekeza muda mwingi na pesa nyingi kama wengine wanaokuja kushtuka mtoto sio wake ameshamsomesha mpaka chuo huko na ajira mtoto ameshapata

Kwahiyo kuachana na huyo mtoto ni jambo sahihi na rahisi kwako kwa wakati uliopo ufate maisha yako na upambane kwaajili ya watoto wako wengine
Ahsante sana familia
 
Sio kwel mimi nina maisha yangu mengine na nishaoa mwanamke mwingine kinachoniuma nimesumbuka sana kumlea uyo binti af saiv kirahis tu sio mwanangu kvp an
Kama uliweza kuacha vitu vyote, ulivyotafuta nae na kuanza moja unashindwa VP kukausha gharama za kulea huyo mtoto ambae sio wako?
 
Sio kwel mimi nina maisha yangu mengine na nishaoa mwanamke mwingine kinachoniuma nimesumbuka sana kumlea uyo binti af saiv kirahis tu sio mwanangu kvp an
Kama kinachokuuma ni gharama ulizotumia kulea huyo binti chukulia kama umetoa sadaka kisha piga mwendo. Ila kama unaamini kweli ni damu yako mpimeni mtoto dna.
 
Back
Top Bottom