Naomba Ushauri: Mwanamke wangu ananiambia mtoto si wangu

Naomba Ushauri: Mwanamke wangu ananiambia mtoto si wangu

Kote uko anatmia majina yangu ndio af wendawazimu inawezekana maana ata mi simuelew kawaje
Basi, we assume tu ni wako maana utakachopoteza kama si wako na ukamtunza ni kidogo kulinganisha na utakachopoteza kama ni wako na usimtunze. Ila usilazimishe kumtunza kupitia mama, wewe hakikisha ada zimelipwa, mtoto ana bima kama inawezekana n.k
 
Nyie Bado mnapendana, afu Bado hamjakomaa kwenye, game ya ndowa,
Sasa mmeshatengana na umeambiwa mtoto sio wako ss unatakaje? SI uendelee na maisha yako?
Ushauri jibebishe, akiingia kwenye mfumo mjaze mimba! Japo hapo [emoji817] Bado mnapendana!
wanapendana ?!! hakuna bana

kilichopo jamaa anampenda DEMU
ila hiyo demu hakuwahi kuwa na upendo kwa jamaa
yaan alionaga alikosea sana kuingia mahusiano na mshikaji
7bu demu anafeel jamaa sio hadhi yake yaan ile kuwa nae ni kma alimuonea huruma tu
ndio mana vimbwanga ubabe hauishi kumletea jamaa since wapo wanaishi pamoja na mpak sasa
Yaan huyo demu anajua FIKA kuwa huyo jamaa kwake apindui
na demu anajua kucheza na akili ya jamaa
yaan kamfanya boya wa kumtatulia shida zake na ndio maana huyo demu akipiga simu kwa jamaa ni mpk akiwa na shida tu

ngoja nimpe Ushauri jamaa

hipo hivi MWANAMKE katika maisha yake huwa anapenda mara 2 tu
wakwanza ni yule wa mwanzoni tunaitaga FIRST LOVE ( huyo FIRST LOVE sio lazima awe amemtoa bikira sometime bikra za wadada zinatokaga kizembe tu)
so namaanisha yule alompemda kweli mwanzoni mwanaume wa kwanza kumpenda
mara nyingi huyu uishia kumtenda sana na sasa wanawake wengi ndo huwa makauzu 7bu moyo wa kuoenda huwa washaupoteza kabisa hso demu anakuwa hana upendo kam akiingia katika mahusiano basi ni kwa ajili ya kitu furani
yaan anafata kitu sio mapenzi
ndio ilivyotokea kwa jamaa huyo demu hakuwa na mapenz nae alifata tu kitu furani kwa wakati huo

wa pili ni yule ambaye wakati ataamua sasa anataka kuolewa kuanzisha familia
kwanza hapa uelewe ninaposema ANATAKA KUOLEWA na sio wewe umempenda unataka UMUOE
demu akiwa anataka kuolewa kuanzisha FAMIRIA
huwa anaamua kuolewa kwa kwa mtu anayemuona yeye anafaa ndio mana usishangae mwanamke kaolewa na mtu ambaye hukudhania kama anageweza kuolewa nae angekuwa nae na NDOA anaifurahia tena na familia anaipambania kabisa NDOA yake

Tofauti mahusiano mengine ambapo unaweza kumpenda mdada ukamuoana anafaa kuwa mke kwa 7bu ana sifa zote za kuwa mke and yes ni wife matilio haswa lakn shida yeye ajakuelewa wewe
So ukaforce sana umuoe kwa ushawishi wa aina mbalimbali
mpk akakubali ndoa
sasa hapo inakuwa wewe umelazimisha umuoe ila yeye hakutaka kuolewa na wewe au hakutaka kuolewa muda huo
Mara nyingi NDOA za hizi huwa na misukosuko sana 7bu upande mmoja ndio ulihitaji hiyo NDOA au mahusiano
sasa mahusiano ya hvyo au ndoa ndio huwa kama hivi mshikaji demu akishakuchoka anafanya visa 7bu hakuitaka ndoa na wala hakukupenda
ila wewe uliforce sana kwa ushawishi wa vitu au mamboa kadhaa na yeye akafata ushawishi wa kitu fulani kuingia katika NDOA au mahusiano

Sasa mkuu wewe uliforce sana mahusiano na huyu demu ulimsaidia sana ulimtatulia sana shida zake yote ulifanya kutaka kumuonesha namna gani unamjari na Unampenda na unahitaji kufanyanae maisha
lakikini kiuhalisia huyu demu hakuwa amekukubari ni vile tu ulikuwa unamzingatia sana maokoto na shida zake ulikuwa unazitatua kwa haraka

wewe chakufanya kata mawasiliano kata huduma
wazazi wakiuliza sana wapige chenga wakikaza waambie kuwa alikuambia mtoto si wako na ushahidi anao hvyo hukuona 7bu ya kuendelea kuangaika na mtu asie na shukrani

nina uhakika atakutafuta akiwa na shida
hauna haja hata ya kupigizana nae kelele wala kuuliza habari za mtoto
we muendee mikausho mikali sana
na sioni 7bu ya kutupa pesa kwenda kupima DNA 7BU ameshakuambia si wako so una haja ya kuangaika kuuliza uliza kama ni kweli au sikweli ama anatania nk au kutaka huo ushaidi we mwache abaki nao mwenyewe
siku zote wanasema mwanamke ndio hujua mtoto ni wa nani

so piga mishe zako NUNUA GARI KALI PIGA PAMBA KALI UNYUNYU WA UKWELI piga misosi haswa nenda GYM km utakuwa na nafasi then chukua PISI matata sana uenjoy maisha mkuu
UUMBAJI HAUJIRUDII ENJOY KILA NUKTA YA MAISHA YAKO huyo KIBWENGO MMOJA asikufanye ukaiona DUNIA CHUNGU wakati walimbwende wapo kibwena mkuu

ila usisahau SALA NA KAZI na kutoa SADAKA
 
Hawa Viumbe wanahitaji wapimwe akili
Matatizo na hiz kesi zimekuwa kwa kasi kipindi hichi
Hii sio hali ya kawaida
Lazima kutakuwa kuna kitu kwa Wanawake wa siku hizi
 
Nilikataa kua sio mimba yangu lakini wazazi ndugu na watu wangu wa karibu wakanishauri kua ingekua kweli sio mimba yangu na kwa namna tulivoachana basi asingekua na sabab ya kuniambia kua ni ujauzito wangu ivo nisikatae damu.


Yameisha lakini"Leo acha tu nikwambie ukweli huyu mtoto sio mwanao".

Nikajua kua labda tu ni hasira zikiisha atasema ukweli lakini ni yuko tu serious kua mimi sio baba wa uyo mtoto na anauthibitisho

Nifanyeje
Unauliza kabisa ufanyeje na umeshaambiwa mwana si wako?

Yaani ulikataa mimba mwanzo kabisa hadi ukawekwa mtu kati na nduguzo ambao hata hivyo walikushauri kwa busara tu si kwamba walipima DNA na kuupata uhakika kabla ya kukushauri, halafu leo hii unaambiwa mwana si wako unashangaa na huamini amini! Wonderful.

Na kuthibitisha ulivyokufa ukaoza kwake hupindui (bila shaka ndio sababu alikutawala), mwanamke mlishaachana akaolewa kwingine akaachika pia, lakini huku umetuandikia "mwanamke wangu" tena kwenye heading kabisa!
 
Mpuuzi wewe, ushaambiwa mtoto sio wako ushauri wa nini tena 🤷,
Mnatokaga wapi nyie vijanaume.
Hapo katangulizs mapicha kibao umengangana tu na hilo nungayembe.
Ungekua karibu makofi ingekuwa ushauri wangu.
Pumbavu sana
 
Nyie Bado mnapendana, afu Bado hamjakomaa kwenye, game ya ndowa,
Sasa mmeshatengana na umeambiwa mtoto sio wako ss unatakaje? SI uendelee na maisha yako?
Ushauri jibebishe, akiingia kwenye mfumo mjaze mimba! Japo hapo 💯 Bado mnapendana!
wewe ndio una point afate huu ushauri.
 
BINTI YANGU

Tafadhari ukimaliza kusoma naomba ushauri wako

Stori inaanzia 2020 mwezi wa saba tulishindwa kuishi pamoja na suluhu ikakosekana tukaachana kwa fujo nyingi kwake yeye mwanamke mixer kunitukania wazazi na kunitishia laana ya mahusiano.as a men niliamua kumuachia kila kitu tulichokua nacho vitu vya ndani japo havikua na thaman kubwa sana ila vilitoshea kugawana au hata kuvichukua vyote kwa7babu nilimtolea mpaka mahali kwao niliamua kuacha yote ayo ili nibaki na aman tu.

Kipindi chote hicho alikua hajajigundua kumbe alikua na mimba changa ambayo ndio mtoto wangu wa pili.Baada ya mwezi mmoja na kama wiki 2 kupita alinipigia simu akanambia yeye ni mjamzito na io mimba ni yangu🙆‍♂️,kiukwel ilikua ngum sana kuikubali kutokana na jinsi tulivyoachana maana nilikua nampigia mpaka sim nimjulie hali before {mazoea} lakini aliishia kunitukana na kupiga sim kwa wazaz wangu kua mwambieni mtoto wenu asinisumbue kwani tumeshaachana.

Nilikataa kua sio mimba yangu lakini wazazi ndugu na watu wangu wa karibu wakanishauri kua ingekua kweli sio mimba yangu na kwa namna tulivoachana basi asingekua na sabab ya kuniambia kua ni ujauzito wangu ivo nisikatae damu.

Nikakubali nikalea mimba matumizi yote nikazingatia akajifungua kwa shida kidogo kwasabab alikua mbali na kituo cha afya kukodi gari na nn gharama zote izo nilimaliza mwenyew

Malezi yakaendelea ile mtoto anaumwa sijui nguo viatu nilizingatia hata kipindi anamuachisha alimleta nyumbani kwa baba yangu akamuachishia kwetu,kidini mtoto akabatizwa kwa jina langu pia.mtoto akaendelea kukua akiwa mbali na mimi baba.Yule dada akapata mwanaume mwingine akaolewa akazaa nae mtoto mmoja wakashindwana na yule mwanaume nae pia wakaachana.

TATIZO
Kilichonifanya niweke shauri hili nikitaka msaada wa ushauri hata sheria ama busara kwenu ni kwamba ilitoke mtafaluko kidogo mimi na uyo dada kuhusu mtoto alinipigia simu kua anaumwa na yeye hayupo nyumbani kasafiri na aliowaachia mtoto hawawezi kumpeleka hospital yaani anakokaa yeye mpaka hospital ni kama km 6 ivi na nilipo mimi mpaka kufika kule ni kama km 25.

Kwa jicho la kibinadam nilifanya makosa kweli kutokwenda kwa7b za kawaida tu.yote kwa yote homa ya kawaida mtoto alitibiwa na akapona,lakini mamake alikasilika sana kias kwamba hakutaka kusikia chochote kutoka kwangu.

Kwa kutambua kosa langu nikajishusha nikamuomba msamaha sana akanielewa lakina akaniambia kua nanukuu!

Yameisha lakini"Leo acha tu nikwambie ukweli huyu mtoto sio mwanao".

Nikajua kua labda tu ni hasira zikiisha atasema ukweli lakini ni yuko tu serious kua mimi sio baba wa uyo mtoto na anauthibitisho

Nifanyeje
Nadhangaa sana mtu anayepambania custody ya mtoto
 
Umesumbuka kweli kumlea Binti ila Bado ujawekeza muda mwingi na pesa nyingi kama wengine wanaokuja kushtuka mtoto sio wake ameshamsomesha mpaka chuo huko na ajira mtoto ameshapata

Kwahiyo kuachana na huyo mtoto ni jambo sahihi na rahisi kwako kwa wakati uliopo ufate maisha yako na upambane kwaajili ya watoto wako wengine
Ningeshauri upime DNA ya siri...siku ujifanye unamchukua kisha upime DNA ndio itakuwa suruhu..ukipata nywele zake inatosha
 
Back
Top Bottom