BINTI YANGU
Tafadhari ukimaliza kusoma naomba ushauri wako
Stori inaanzia 2020 mwezi wa saba tulishindwa kuishi pamoja na suluhu ikakosekana tukaachana kwa fujo nyingi kwake yeye mwanamke mixer kunitukania wazazi na kunitishia laana ya mahusiano.as a men niliamua kumuachia kila kitu tulichokua nacho vitu vya ndani japo havikua na thaman kubwa sana ila vilitoshea kugawana au hata kuvichukua vyote kwa7babu nilimtolea mpaka mahali kwao niliamua kuacha yote ayo ili nibaki na aman tu.
Kipindi chote hicho alikua hajajigundua kumbe alikua na mimba changa ambayo ndio mtoto wangu wa pili.Baada ya mwezi mmoja na kama wiki 2 kupita alinipigia simu akanambia yeye ni mjamzito na io mimba ni yangu🙆♂️,kiukwel ilikua ngum sana kuikubali kutokana na jinsi tulivyoachana maana nilikua nampigia mpaka sim nimjulie hali before {mazoea} lakini aliishia kunitukana na kupiga sim kwa wazaz wangu kua mwambieni mtoto wenu asinisumbue kwani tumeshaachana.
Nilikataa kua sio mimba yangu lakini wazazi ndugu na watu wangu wa karibu wakanishauri kua ingekua kweli sio mimba yangu na kwa namna tulivoachana basi asingekua na sabab ya kuniambia kua ni ujauzito wangu ivo nisikatae damu.
Nikakubali nikalea mimba matumizi yote nikazingatia akajifungua kwa shida kidogo kwasabab alikua mbali na kituo cha afya kukodi gari na nn gharama zote izo nilimaliza mwenyew
Malezi yakaendelea ile mtoto anaumwa sijui nguo viatu nilizingatia hata kipindi anamuachisha alimleta nyumbani kwa baba yangu akamuachishia kwetu,kidini mtoto akabatizwa kwa jina langu pia.mtoto akaendelea kukua akiwa mbali na mimi baba.Yule dada akapata mwanaume mwingine akaolewa akazaa nae mtoto mmoja wakashindwana na yule mwanaume nae pia wakaachana.
TATIZO
Kilichonifanya niweke shauri hili nikitaka msaada wa ushauri hata sheria ama busara kwenu ni kwamba ilitoke mtafaluko kidogo mimi na uyo dada kuhusu mtoto alinipigia simu kua anaumwa na yeye hayupo nyumbani kasafiri na aliowaachia mtoto hawawezi kumpeleka hospital yaani anakokaa yeye mpaka hospital ni kama km 6 ivi na nilipo mimi mpaka kufika kule ni kama km 25.
Kwa jicho la kibinadam nilifanya makosa kweli kutokwenda kwa7b za kawaida tu.yote kwa yote homa ya kawaida mtoto alitibiwa na akapona,lakini mamake alikasilika sana kias kwamba hakutaka kusikia chochote kutoka kwangu.
Kwa kutambua kosa langu nikajishusha nikamuomba msamaha sana akanielewa lakina akaniambia kua nanukuu!
Yameisha lakini"Leo acha tu nikwambie ukweli huyu mtoto sio mwanao".
Nikajua kua labda tu ni hasira zikiisha atasema ukweli lakini ni yuko tu serious kua mimi sio baba wa uyo mtoto na anauthibitisho
Nifanyeje